Mnaosema bandari imeuzwa tunaomba mtueleweshe imeuzwaje, na kwa kiasi gani

kiroka

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2018
Posts
358
Reaction score
1,887
Huu mjadala wa kwamba bandari ya Dar imeuzwa na nyingine zote zimeuzwa unakolezwa sana.

Tuondoe u-CCM na u-CHADEMA naomba kueleweshwa kua bandari imeuzwaje, kwanini nataka kueleweshwa.

Kabla ya bunge kupitisha na kuridhia mkataba wa serikali kuingia ubia na Dubai maneno yalikua mengi kua bandari imeuzwa lakini baada ya kumsikiliza Mbarawa naona mnazidi kunichanganya.

Serikali wamesema suala la ulinzi na usalama wa bandari bado utabaki chini ya vyombo vya ulinzi vya nchi yetu Tanzania, swali je hatuviamini vyombo vyetu?

Dubai wanapewa baadhi ya gates wafanye operation, kama sijaelewa nimesikia kua kwenye ubia huu hawa Dubai hawapewi bandari nzima wanapewa baadhi ya gates lkn nyingne wataendelea kufanya kazi TPA je hapa bandari imeuzwaje.

Mamlaka za serikali zote zitakuepo bandarini, serikali imesema mamlaka zote za serikali kama TPA na TRA zitaendelea ku oparate bandarini yaani hakuna kitu watafanya bila TRA na TPA kujua in short ni kuwa TRA itaendelea kukusanya cha kwao na TPA nao halikadhalika, tuelewesheni hapa tumepigwaje.

Ajira, serikali wanasema ajira za Watanzania zilizopo bandarini zitalindwa na kutaongezeka nyingine ubaya wa hawa Dubai uko wapi na hapa tutapigwaje?

Serikali inasema imeamua kufanya ubia ili kuongeza ufanisi katika utendaji, hapa ni kupunguza siku za meli kutia nanga kutoka siku nne mpaka wastani wa siku moja na nusu.

Sisi kama nchi tumepambana tumeshindwa ku oparate kwa ufanisi wa kimataifa kwa muda mrefu tumeamua kutafta watu wengine watuongezee technology tupate Zaidi nao wapate.

Wamesema kama kutatokea mgogoro Dubai na Tanzania watakaa meza moja kuzungumza, sheria zitakazotumika kumaliza mgogoro ni za Tanzania na sehemu ya kufanyia usuluhishi imetajwa tunaogopa nini, tufafanulieni?

Wamesema hawa jamaa kama wakiweza kufanya vizuri huko mbeleni watapewa bandari nyingine wakishindwa sisi Tanzania tunaweza kumpa mtu mwingine, hapa shida iko wapi?

Tunaomba tupewe darasa la bure wenzetu kua tutapigwaje huko mbeleni.
 
Kwa malipo ya Sh ngapi tufanye hiyo kazi? Biashara ya Makinikia tulibishana hivi hivi, kiko wapi?
Tutalipana kulungana na jinsi mzigo utavoingia hapo shda iko wap
 
Dubai wanapewa baadhi ya gates wafanye operation, kama sijaelewa nimesikia kua kwenye ubia huu hawa Dubai hawapewi bandari nzima wanapewa baadhi ya gates lkn nyingne wataendelea kufanya kazi TPA je hapa bandari imeuzwaje
1. Wapi inasema hivyo kwenye makubaliano?
2. Wanapewa hizo baadhi ya gates, kwa muda gani?
3. Hako kapeewe kenyewe kakoje? Je, ni kuazimwa, kukodishiwa, kuajiriwa, kubinafsishiwa, kuuziwa, au niaje?
4. Tukiona hawafanyi kazi nzuri, tunawezaje kuvunja mkataba?
 
Tutalipana kulingana na mzigo utavoingia
 
1. Wapi inasema hivyo kwenye makubaliano?
2. Wanapewa hizo baadhi ya gates, kwa muda gani?
3. Hako kapeewe kenyewe kakoje? Je, ni kuazimwa, kukodishiwa, kuajiriwa, kubinafsishiwa, kuuziwa, au niaje?
4. Tukiona hawafanyi kazi nzuri, tunawezaje kuvunja mkataba?
Kama ungeisikiliza hotuba ya waziri ungeelewa wametaja gates wanazopewa kwa sasa na huu ni mwazo wameeleza cover tu ya kinachoenda kufanyk na ndio maana wabunge wamesem ikiwezekn kila mkataba utakaoingiwa uletwe kwao wadadavuw kipi ni kipi
 
Hayo maelezo uliyosikia bungeni ni sawa lkn umeyaona kwenye mkataba wenyewe, mkataba ulishatoka na hakuna anayejitokeza kuukanusha, utata huko hapo.
 
B6C0E689-ECCA-40BA-AC32-BFAF2D8B7471.jpeg

Hiyo Ro-Ro inapokea meli kama hizo, biashara ikichanganya hapo kwa nchi zinazotumia hiyo bandari. Kitengo icho tu kinaweza tengeneza ajira 200-500 mpya za madereva kama lengo ni kuitoa meli in 24 hours.

Hayo magari yanashushwa na watu, ndio maana kwa kufikiria future increase in volumes; kabla ya bandari kuchanganya wana jenga multi storey car park. Ni madereva kibao wanapata ajira.

Hiyo inaenda kuuwa biashara ya private car yards na storage charges za kishamba.

Mtu anaepinga huo mradi ajaipata bado bigger picture; ni mradi unaoenda badili namna ya kuendesha bandari kabisa.

Ndio maana wanafikiria na mbele kuziboresha Port zingine za kanda ya ziwa zinazotumiwa na nchi nyingine. Kuongeza inflow na outflow ya shipping inventory za aina zote ili volumes za kutoa mizigo ziwe kubwa pia.

Mimi sio shabiki wa mama vileee; ila hapa kaupiga mwingi. Kilichobaki ni kupata good terms.
 
Hayo maelezo uliyosikia bungeni ni sawa lkn umeyaona kwenye mkataba wenyewe, mkataba ulishatoka na hakuna anayejitokeza kuukanusha, utata huko hapo.
Hakuna mkataba mpaka sasa hyo ni makubaliano yanayotupelek kweny mikataba na hiv tunavyoviona ni sehem ndogo mistar mmoja tu usomwe ukiwa na vifungu vingn
 
Kama ungeisikiliza hotuba ya waziri ungeelewa wametaja gates wanazopewa kwa sasa na huu ni mwazo wameeleza cover tu ya kinachoenda kufanyk na ndio maana wabunge wamesem ikiwezekn kila mkataba utakaoingiwa uletwe kwao wadadavuw kipi ni kipi
Wewe uliyemsikiliza waziri si ujibu maswali yangu kwa kuwa umemwelewa huyo waziri!
 
Safi sana..
Kwanza tunashukuru kama alivyosema bw Zitto Kabwe Kwa kupeleka mkataba bungeni.
Maswali yako mengi. Lakini tuanze na haya mepesi.

Ukomo wa mkataba....(tafadhali kina Mbarawa wasiseme uhai wa mkataba utategemea ufanisi wa DP WORLD).

Wenzetu wanaingiza hela kwa kiasi gani iwe Kwa miundo mbinu vifaa utaalamu nk.

Hicho kilichosainiwa Oct 2022 ni nini?! Na kwanini kilisainiwa kabla ya kuletwa bungeni?!

Twajuwa TPA wanahitaji msaada wa kuendesha bandari Kwa njia nyingi. Kwanini DP World?! Kwanini wamekataliwa Namibia USA na baadhi ya nchi nyingine?!

Maswali mengine yatafuata kama mkataba utawekwa wazi kwa sisi raia kwa Kiswahili
😠😡🤬
 
Huu mjadala wa kwamba bandari ya dar imeuzwa na nyingine zote zimeuzwa unakolezwa sana

Tuondoe uccm na uchadema naomba kueleweshwa kua bandari imeuzwaje, kwanini nataka kueleweshwa.

Kabla ya bunge kupitisha na kuridhia mkataba wa serikali kuingia ubia na Dubai maneno yalikua mengi kua bandari imeuzwa lakini baada ya kumsikiliza mh Mbarawa naona mnazidi kunichanganya

Serikali wamesema suala la ulinzi na usalama wa bandari bado utabaki chini ya vyombo vya ulinzi vya nchi yetu Tanzania, swali je hatuviamini vyombo vyetu?

Dubai wanapewa baadhi ya gates wafanye operation, kama sijaelewa nimesikia kua kwenye ubia huu hawa Dubai hawapewi bandari nzima wanapewa baadhi ya gates lkn nyingne wataendelea kufanya kazi TPA je hapa bandari imeuzwaje

Mamlaka za serikali zote zitakuepo bandarini, serikali imesema mamlaka zote za serikali kama TPA NA TRA zitaendelea ku oparate bandarini yaan hakuna kitu watafanya bila tra na tpa kujua in short ni kua tra itaendelea kukusanya cha kwao na tpa nao halikadhalika,tuelewesheni hapa tumepigwaje

Ajira, serikali wanasema ajira za watanzania zilizopo bandarin zitalindwa na kutaongezeka nyingine ubaya wa hawa Dubai uko wapi na hapa tutapigwaje

Serikali inasema imeamua kufanya ubia ili kuongeza ufanisi katika utendaji, hapa ni kupunguza siku za meli kutia nanga kutoka siku nne mpk wastani wa siku moja na nusu,

Sisi kama nchi tumepambana tumeshindwa ku oparate kwa ufanisi wa kimataifa kwa muda mrefu tumeamua kutafta watu wengine watuongezee technology tupate Zaid nao wapate

Wamesema km kutatokea mgogoro Dubai na Tanzania watakaa meza moja kuzungumza, sheria zitakazotumika kumaliza mgogoro ni za Tanzania na sehemu ya kufanyia usuluhishi imetajwa tunaogopa nini tufafanulieni

Wamesema hawa jamaa kama wakiweza kufanya vizuri huko mbeleni watapewa bandari nyingine wakishindwa sisi Tanzania tunaweza kumpa mtu mwingine hapa shida iko wapi.

Tunaomba tupewe darasa la bure wenzetu kua tutapigwaje huko mbeleni
Hakuna ubia Wa 100%.
Hatuwahitaji Tena CCM kwenye nchi hili .

Hawa Wanaweka mawakala wao watakaowadhamini Ili waendelee kukaa madarakani Kwa kuiibia nchi na kwenda kujenga na kuishi Dubai ,Jiji la mabilionea Wa Dunia.
Watawala na viongozi Wa CCM na baadhi ya wabunge wameshahakikishiwa KUWA watakua wakazi Wa Dubai.

Hawa Dubai ni mawakala Wa Nchi za magaharibi. Wanajua wanachofanya Duniani.

Watanganyika na waafrika tuamke .

Lengo lao ni kumwondosha Mwafrika Duniani kabisa au kuwaacha waafrika Wachache wenye ubinafsi mkubwa Wa kuuza Kila kitu alimradi wavae Kanju,SUTI, na Kaniki na shanga Kwa wake zao.

Hiví tatizo la nchi yetu ni Wawekezaji au ni kuwa na Wasomi wezi na wabinafsi walioamua kushirikiana na wageni kuibia nchi.?

Hiví tunasimesha Watoto WETU Ili wakawe watumwa Wa Waarabu na wazungu kwenye nchi yetu?

Hiví hatuoni vita itakayokuja ya wajukuu WETU kuuana Kudai uhuru Wa kumiliki mipaka na uchumi Wa nchi yetu?

Kwa nini tuache Maradi Wa Bandari ya Bagamoyo hakafu tugawe Bandari ya Dar es salaam Bure Kwa Waarabu ambao kimsingi wanakuja kwenye nchi ya kijamaa ,isiyo na Dini .Tuliwakataa Wachina wajamaa Wenzetu wasio fungamana na Dini yoyote halafu tunawapa Waarabu wanaifungamana na Dini moja tuu na pia wanafungamana na Nchi za magharibi hasa Marekani.

Iko wazi kabisa Hawa ndio watakaotumika kuleta chokochoko kwenye nchi yetu Kwa manufaa ya nchi hiyo na Marekani. Marekani na Washirika wake walikua wanaitamani sana Tanganyika Sasa wamepata pa kuingilia ,Zanzibar walishaichukua na kuifanya iwe maskini kupitia Muungano usioeleweka .
Watatuvuruga kirahisi sana Kwa Sasa .

Marekani Sasa tumeshawapa nchi kupitia mawakala wao amabao ni nchi ya Falme za Kiarabu Wakiamua kutuvuruga kidini watafanikiwa Kwa haraka kuingiza sílaha wakiamua kutuvuruga kiuchumi watafanikiwa Kwa haraka ,wakiamua kutuvuruga kisiasa wameshafanikiwa.

Kwa Kizazi hiki Cha kina Makamba Jr waliofaulu mitihani Kwa wizi Hatuwezi kufaidika na wawekezaji Kwa nchi yenye Sheria legelege na katiba legelege kama ya kwetu . Hata wangekuja wawekezaji kutoka Mbinguni .
Tunapinga ni kuwapa Wageni rasilimali zetu wakati tumewekeza kwenye elimu Kwa watoto WETU Kwa kiwango chenye matumaini ya kuja kubadili baadhi ya mambo hasa suala la uadilifu na uwajibikaji. Sasa kuwapa Wageni Kila kitu mpaka Bandari ni kukiri KUWA watanzania na vizazi vyetu vijavyo Hata Kwa Karne Nzima ijayo watakua hawana uwezo Hata Kwa kukusanya mapato kwenye nchi Yao na kujenga Bandari na kuisimamia wenyewe.

Tumeuzwa pamoja na Ulinzi Wote .
Nchi Sasa ni Mali ya Matajiri na familia ya Mtawala Wa Falme za Kiarabu .

Walianza na Loliondo na Sasa wamechukua Bandari. Wanaelekea kuchukua usalama Wa nchi mana watakuja kusema KUWA hawana Imani na Ulinzi na usalama Wa nchi yetu . Watatuletea military base ya Marekani pale kigamboni. Sasa nchi ni Mali ya mfalme wa kule Falme za Kiarabu chini ya udhamini Wa CIA ya Marekani . Falme za Kiarabu ni Nchi isiyo na Demokrasia lakini ni Rafiki Mkubwa Wa Marekani.
 
Duuu mbona umejaza vitu vingi saana kichwani
 
Huu mjadala wa kwamba bandari ya dar imeuzwa na nyingine zote zimeuzwa unakolezwa sana

Tuondoe uccm na uchadema naomba kueleweshwa kua bandari imeuzwaje, kwanini nataka kueleweshwa.

Kabla ya bunge kupitisha na kuridhia mkataba wa serikali kuingia ubia na Dubai maneno yalikua mengi kua bandari imeuzwa lakini baada ya kumsikiliza mh Mbarawa naona mnazidi kunichanganya

Serikali wamesema suala la ulinzi na usalama wa bandari bado utabaki chini ya vyombo vya ulinzi vya nchi yetu Tanzania, swali je hatuviamini vyombo vyetu?

Dubai wanapewa baadhi ya gates wafanye operation, kama sijaelewa nimesikia kua kwenye ubia huu hawa Dubai hawapewi bandari nzima wanapewa baadhi ya gates lkn nyingne wataendelea kufanya kazi TPA je hapa bandari imeuzwaje

Mamlaka za serikali zote zitakuepo bandarini, serikali imesema mamlaka zote za serikali kama TPA NA TRA zitaendelea ku oparate bandarini yaan hakuna kitu watafanya bila tra na tpa kujua in short ni kua tra itaendelea kukusanya cha kwao na tpa nao halikadhalika,tuelewesheni hapa tumepigwaje

Ajira, serikali wanasema ajira za watanzania zilizopo bandarin zitalindwa na kutaongezeka nyingine ubaya wa hawa Dubai uko wapi na hapa tutapigwaje

Serikali inasema imeamua kufanya ubia ili kuongeza ufanisi katika utendaji, hapa ni kupunguza siku za meli kutia nanga kutoka siku nne mpk wastani wa siku moja na nusu,

Sisi kama nchi tumepambana tumeshindwa ku oparate kwa ufanisi wa kimataifa kwa muda mrefu tumeamua kutafta watu wengine watuongezee technology tupate Zaid nao wapate

Wamesema km kutatokea mgogoro Dubai na Tanzania watakaa meza moja kuzungumza, sheria zitakazotumika kumaliza mgogoro ni za Tanzania na sehemu ya kufanyia usuluhishi imetajwa tunaogopa nini tufafanulieni

Wamesema hawa jamaa kama wakiweza kufanya vizuri huko mbeleni watapewa bandari nyingine wakishindwa sisi Tanzania tunaweza kumpa mtu mwingine hapa shida iko wapi.

Tunaomba tupewe darasa la bure wenzetu kua tutapigwaje huko mbeleni
Akili yako haiwezi kuelewa haya maana huna mental faculties zinazoweza kukuweka katika ku decipher vitu kama hivyo
 
Back
Top Bottom