Mnaosema bandari imeuzwa tunaomba mtueleweshe imeuzwaje, na kwa kiasi gani

asante mkuu. umeweka mambo in a "nutshell" ila wabwabwaji hawana logic kama hizi kazi yao ni kupinga tu.
 
jibu hoja sasa
Hakuna hoja , kila kitu kiko kwenye the so called mkataba, asome huo mkataba, asitake kutafuniwa. Kama hawezi kusoma na kuelewa, basi ndiyo maana nasema haya yako nje ya uwezo wake wa kufikiri. Seems na wwe nadhani ni mlolongo huo.
 
baadhi ya watu ni waongo hatari

Sent from my CPH2371 using JamiiForums mobile app
 
asante mkuu. umeweka mambo in a "nutshell" ila wabwabwaji hawana logic kama hizi kazi yao ni kupinga tu.
Logic Gani mkuu .?
Yaani huoni KUWA hakuna mkaraba ambao umewahi kusainiwa na Serikali ukalinufaidha Taifa zaidi ya kulipa hasara.!?

Amini usiamini Nabii Wa Tanzania ni Nyerere na KARIME.
TANGANYIKA Nabii wake ni Nyerere na Zanzibar nabii wake ni Karume .
Kila nchi na kabila duniani Ina asili yake na watu ambao Mwenyezi Mungu aliwapa uwezo Wa KUWA na maono mapana ya kuiona baadae ya Taifa hilo. Wenzetu waliotangulia katika Mataifa Yao waliwaita manabii . Na akavunisha KUWA ni manabii Wa Dunia Nzima . Lakini ukifuatilia Vizuri Hao Hao ndio wanaokiuka Yale Hata Hao manabii Wa Dunia waliyoyasema .
MWALIMU Nyerere alisema Rasilimali za Tanzania wasipewe Wageni Kwa watu Wa Kizazi hiki kutokana na Elimu Bado Iko chini . Ndio kuna maprofesa lakini jiulize Kuna maProfesa wangapi ambao WAKO WAKO vizuri kuanzia kitaaluma ,kimaadili , kiimani, kimaono ,kibiashara ,kauli zao , falsafa zao na Uzalendo wao?
Au ni Hawa wasomi na wataalam wabinafsi ambao wakishapata vyeti wanarelax na kupewa pombe na wanawake na kuangalia namna ya kujiongezea masalahi na vikao Ili wapate pesa wakajenge majumba Kwa ajili ya kurethisha Watoto wao bila kujali kuwa wamepewa dhamana ya kusimamia rasilimali na mapato ya nchi Maskini na kuleta maendeleo Kwa Taifa lililowasomesha ?

Lakini nini tatizo Kwa wasomi Hawa waliopo?
Tuliosoma CUBA tunafahamu wazi KUWA Kizazi hiki Kwa asilimia kubwa ni zao la wizi Wa mitihani kuanzia masekondari, wizi Wa kura , udanganyifu kwenye ajira n.k.
Hata hivyo Bado tunawashukuru Kwa sababu wametusogeza mbele kidogo japo Kwa kupotea potea njia na kupapasa pasa kama vipofu.
Hiví hauamini KUWA Hata maprofesa waliopo kwenye maamuzi ya kisiasa hawawezi kamwe kusimama kwenye majukwaa wakati Wa kampeni na Kupiga porojo na kampeni zao Kwa Lugha nyingine mbali na Kiswahili.? Yaani kamwe hawana uwezo Wa kusimama kwenye jukwaa na Kutumia nusu Saá kuekezea mipango na mikakati ya maendeleo wanayokusudia kuifanya Kwa Lugha nyingine .Sasa watu kama hao ni lazima wataingizwa chaka kwenye mikataba ya kimataifa na hawatakua na muda mzuri Wa kwenda kufungua kesi kwenye mahakama ya kimataifa endapo mikataba itakiukwa. Mikataba ikikiukwa hawana habari Maana wao wameshiba na Watoto wao.
Falme za Kiarabu hakuna Demokrasia lakini WanaSharia Kali na Mila zao ni Kali ukilinganisha na Tanzania ambapo hatujui tunasimama wapi. Watu Wa Tanzania Bado wanapendeleana bila kujali Uwezo Sio tu Wa kitaaluma lakini pia maadili. Watu wanakutana baa na kupeana KAZI Kwa sababu ya Kununuliana pombe au Kwa sababu TU ya ngono. Kizazi hicho lazima kiwaze starehe tu na kupata pesa za starehe Kwa wizi. Hizi ni Tabia tu ambazo zinaondoshwa Kwa adhabu Kali inayoumiza na kufedhehesha.
Je, Serikali yetu inawaadhibu wanaochukua Mali za umma na kuhamishia majumbani mwao? Hiví kumdhibiti MTU uliyemteua nayo inahitaji Wawekezaji kweli?
Pale bandarini watu wanagawana Mapesa kama karanga na rushwa na kupindisha mapato kuingia mifukoni mwao na inajulikana na Mali zao zinajukana lakini watu walipeana Kwa kujuana na kisiasa na Wanasiasa ni Wa Kwanza kuhujumu mashirika ya umma Sasa hakuna Wa kumfunga Paka Kengele. Matokeo yake Mali za Watanzania wasio na hatia awanapewa wageni huku waliohujumu wakiwa wanakula bata na familia zao. Wageni nao wakipewa wanaiba wanapeleka kwao mana wanajua KUWA ni nchi ya kula Kwa urefu Wa kamba .


Kama akina Cliopa Msuya ,Kighoma Malima, Mramba na Sasa Mwigulu Nchemba wametusogeza basi kipo Kizazi kitakachotupeleka mbele na KUFANYA Mapinduzi makubwa . Kizazi kilichopo chini ya miaka 18 miongoni mwao Kuna watakaotuvusha miaka 20 ijayo Mbele. Kuna kizazi baba Wa Taifa hili alikiona kinakuja . Ni Kizazi chini ya miaka 18. Miongoni mwao wapo waliosoma mitaala ya Cambridge, English medium, Arabic language, Chinese Language n.k . Hawa wameanza kuisoma Computer na mitandao wakiwa nursery school. Hawa watoto na wajukuu zetu ni Kizazi cha Mapinduzi nakubwa yajayo. Hawa watoto na wajukuu Zatu hawana Tofauti na Watoto Wa Kihindi, Kiarabu ,Kizungu,kichina n.k. Watatushangaa sana KUWA tulishindwa kulinda rasilimali zetu Kwa ajili ya wajati wao Ili washindane na Kizazi Cha Dunia Nzima .

Sina Imani na mikataba inayowekwa na Hawa watu wanaotumia Sheria na Katiba iliyopo kujinufaisha mana wanajua hakuna Wa kuwauliza na miaka 20 mbele Wengine watakua makaburuni ,hawana Cha kupoteza mana Katiba zinawalinda. Wamechoka kutorosha wanyama kutumia ndege na Sasa watatumia Meli kusafirisha mpka miamba na udongo WETU wenye rutuba watuachie udongo ngumu.

Sina Imani nao Kwani Tulipogundua Gesi tuliambiwa tutapata pesa nyingi mpaka patafunguliwa Akaunti maalumu Kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Yako Wapi .? Badala yake tumerudi kwenye Kodi mpaka ya Majengo Kwa wapangaji Wa nyumba na vibanda vya kuza mchicha Barabarani kupitia Tanesco.
Walipouza Migodi kule Geita walituambia tutakua namba Moja kuuza dhahabu na tutapata pesa nyingi na uchumi utapaa. Watu waliporwa Ardhi Yao na Wengine kupoteza maisha . Walionufaika ni watawala. Wawekezaji wanajua KUWA watanzania ni wabinafsi hivyo Hata ikiundwa Tume kuchunguza inahongwa kirahisi na kutoa ripoti ya uongo .
Watatuibia watakwenda kujenga Dubai. Bora tuibiwe na wanyiramba,wachaga,Wahaya ,Wazaramo, Wamakonde,wasubi, wajita,waluguru ,wagogo n.k wajenge Tanzania na mzunguko utawafikia Wengine .
Viwanda vya sementi vipo Zaidi ya Saba vikubwa na tuliambiwa sementi itashuka Bei mpaka Elfu 6 lakini inapaa tuu Tofauti na ile inayotoka Nje.

Viwanda vingi vikauzwa tukaambiwa vitafufuliwa na wawekezaji . Matokeo yake tunaagiza mpaka majembe ya mkono,makwanja ya kufyeka , Mapanga na visu kutoka china wakati Babu zetu walitengeneza majembe na mapanga na mikuki Kwa kuyeyusha vyuma.

Tumelogwa na Wanasiasa Kwa manufaa Yao.
 
Nipo kwenye kijiwe cha kahawa,wananchi wanasema wana hakika bandari haijauzwa kwa sababu wamesikia kwenye redio,wanasema kama imeuzwa hela kachukua nani?
 
Nipo kwenye kijiwe cha kahawa,wananchi wanasema wana hakika bandari haijauzwa kwa sababu wamesikia kwenye redio,wanasema kama imeuzwa hela kachukua nani?
Fedha wamegawana waliotuuza
  1. Mbarawa na dada yake kutoka Zanzibar
  2. Wabunge wa chama tawala na spika wao
 
Tumepata taarfa uku nje kuwa waarabu ni watu wafujo na kuharibu nchi ya watu
 
Hivi kwanini sisi wenyewe tumeshindwa kuisimamia hiyo bandari?
Walioko madarakani wana uwezo mdogo wa akili, maarifa na mtazamo?
Hao wanaobinafsishiwa walizaliwa na huo utaalamu?
Je watu wetu haawawezi kuwezeshwa wakafanya kama hao waarabu hata kama ni kwa muda mrefu?
 
Je, wewe umeusoma huo Mkataba wa Ushirikiano, unaitwa "Intergovernmental Agreement (IGA)" ambao Mbarawa alisaini kwa idhini ya Rais SSH?

Serikali wamesema suala la ulinzi na usalama wa bandari bado utabaki chini ya vyombo vya ulinzi vya nchi yetu Tanzania, swali je hatuviamini vyombo vyetu?
Kama vinaamika iweje Merelani Serikali ya Awamu ya Tano ilijenga ukuta! Hujasikia tuhuma za wanyama kama Twiga kusafirisha wakiwa hai?

Dubai wanapewa baadhi ya gates wafanye operation, kama sijaelewa nimesikia kua kwenye ubia huu hawa Dubai hawapewi bandari nzima wanapewa baadhi ya gates lkn nyingne wataendelea kufanya kazi TPA je hapa bandari imeuzwaje

Una ushahidi wowote wa aina hiyo ya Mkataba ambao umetusaidia kiuchumi?

Wamesema kama kutatokea mgogoro Dubai na Tanzania watakaa meza moja kuzungumza, sheria zitakazotumika kumaliza mgogoro ni za Tanzania na sehemu ya kufanyia usuluhishi imetajwa tunaogopa nini tufafanulieni
Usome huo Mkataba "Article 20"

Wamesema hawa jamaa kama wakiweza kufanya vizuri huko mbeleni watapewa bandari nyingine wakishindwa sisi Tanzania tunaweza kumpa mtu mwingine hapa shida iko wapi.
Soma huo Mkataba "Article 5"
 

Attachments

Ohh hapo shida ni waarabu na pia ni waislam
 
Du wee jamaa umejazi mavitu kichwani yasio kichwa wala miguu ebu pungu chuki na angalia jambo kwa upana wake na iweke huru akili yako
 
Bureeeeee kabisa milelee
 
Wamepewa, hawajauziwa
 

Wanaiongelea mkataba haujakaa vzuri law maslahi na usalama wa nchi sio hayo maoni yako mbwiga wewe.
 

Katumiwa kiasi tu kwny mpesa yupo tayr kusaliti
 
Bandari kwa kweli haijauzwa na wala haitauzwa ILA tumewapa bure DP world kwa kuwa wenye DP world ni wajomba zetu.

Wewe utadhubutu kumuuzia kitu mjomba wako, kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…