Mnaosujudu Israel, ni kipi hasa kinachofanya mlione ni taifa lenye watu wenye akili zaidi duniani?

Uwezo wa akili wa mwanadamu unapimwa kutokana na ufanisi katik kupambana na mazingira ili aweze kusurvive. Kwa msingi huo kila mtu ana akili kwa context ya mazingira yake. Mfano, huyo Muisrael sababu yeye ni jamii ambayo imeteswa, imetengwa na kuuliwa, so walihitaji kufanya waliyoyafanya ili waweze kusurvive. Na sasa anaishi middle east ambapo yupo kwenye hostile area, so inabidi apambane kwa kuwa na teknolojia za kumlinda dhidi ya mashambulizi mfano Iron Dome sababu ndio hitaji la mazingira yake au awe na silaha kali za kuwashambulia maadui zake, ndio maana anatengeneza silaha za masafa marefu kama hizo Ballistic Missiles.

Pia muhadzabe anayeishi kule Singida naye anaakili za kuishi katika mazingira yake, hivyo anateknolojia yake ya kutengeneza mikuki imara ya kuwindia na kuweza kwenda mbali (hii ndio Ballistic Missiles yake) ,sasa huyu awe na Iron Dome ya kazi gani wakati mazingira hayajamlazimu? Huyo myahudi unayesema ana akili, ukimuweka Porini Amazon, hawezi kuishi hata siku mbili, lakini mtu wa kabila la kayapo aliyeishi hapo miaka zaidi ya 1,000 atakuwa na akili zaidi yake. So, akili kila jamii inazo, na haipo iliyo bora kuliko mwenzake. Ukisema myahudi anaakili kuliko muhadzabe sababu ametengeneza Iron Dome, ni sawa na kusema simba ana maarifa zaidi ya samaki kisa tu anaweza kupanda mti.
 
Kwa nini wawape Israel hizo pesa kwa nini wasiwape Tanzania ama Kenya. Tuanzie hapo...
Kwasababu nchi inayoongoza kuwa na wayahudi wengi duniani ni Marekani na ndio matajiri wakubwa. Huko hapo?

God bless and protect Israel.
 
hivi wayahudi na waarabu tifauti yao nini?
 
hata mtu mweusi pia kapitia mengi e.g ukoloni na biashara ya utumwa
 
hivi wayahudi na waarabu tifauti yao nini?
They are cousins....

Tofauti yao ni damu tu....babu Yao mmoja....baba zao tofauti....

Waarabu ni kizazi cha Ismaili....
Wayahudi ni kizazi cha Issack...

Lugha zao zinafanana(Aramaic ,Hebrew and Arabic).....

Tamaduni zao zinafanana.....

Imani zao zinafanana na tofauti ni ndogo sana.....

Yetzer ha-tov(good will)
 
wayahudi wana nidhamu ya maisha kivipi?
 
hata mtu mweusi pia kapitia mengi e.g ukoloni na biashara ya utumwa
Sawa.....

Mtu mweusi hajapitia UTUMWA NA UKOLONI kwa muda mrefu.....

Wayahudi wamepitia utumwa miaka mingi mno(400 years) karne kibao nyuma.....

Wayahudi wamepitia UKOLONI karne nyingi mno....WARUMI waliwafanya vibaya mno....WAHISPANIOLA waliwafanya vibaya mno.....WAGIRIKI waliwafanya vibaya mno......

Wayahudi wamekuwa maadui na waonevu wa kila RANGI......

Yetzer ha-tov
 
na ni wazuri kweli kweli
 
hata waarabu pia hiyo wanayo
...ndio maana nikakuambia kuwa wanafanana ila tu tofauti Yao iko hapa.....

Waarabu wameitunza tamaduni yao bila ya kupata misukosuko......walibaki kwao majangwani kwa muda mrefu...majangwa ya kutoka bahari ya shamu mpaka mito ya Tigris na Euphrates......

Wayahudi walitunza tamaduni zao mikononi mwa Hitler na Himmler huko katika makambi ya mateso na mauaji(Bergen ,Auswitchz &Birkenau).....kwa kuwa waliishi na tamaduni tofauti ,ikawaongezea UPEO MKUBWA MNO KUSHINDANA RACES nyingine....
 
bila shaka waarabu ni wengi kuliko wayahudi....wanazaliana sana.vipi kuhusu hao makabila mengine ya Israel
 
bila shaka waarabu ni wengi kuliko wayahudi....wanazaliana sana.vipi kuhusu hao makabila mengine ya Israel
Waarabu wanaonekana kuwa wengi kwa kuwa WALIBAKI BARA ARABIA toka mwanzo wao.....

Wayahudi wengi sana walisambaa duniani....Kuna damu ya kiyahudi nyingi sana ULAYA YA MASHARIKI(URUSI SANA)....Spain ,Italy ,Portugal ,Amerika ya Kusini (Brazil ,Argentina ,Honduras ,Chile , Uruguay ,Colombia etc....

Afrika hii imejaa....Ethiopia ,Zambia,Nigeria na Zimbabwe....

India na far east......
 
hivi hawa waarabu wa bongo walifikaje hapa bongo?
 
hivi hawa waarabu wa bongo walifikaje hapa bongo?
Wako WAYEMENI(mabulushi) hawa waliingia miaka mingi nyuma baada ya karne 7 kuchukua MIKOKO, NA BIDHAA NYINGINE mwambao mwa Tanganyika na visiwa vya Zanzibar na Pemba.....Baadae wakawa wanaleta bidhaa kama nguo ,uturi na vyombo vya vigae......

WAOMANI....hawa waliingia baadae kabisa....nao walifanya biashara nilizoainisha hapo juu....wakanogewa na KUPIGANIA kuyatawala maeneo ya mwambao mwa TANGANYIKA ,Zanzibar na Oman....waliyachukua na kuwa chini yao baadaye SULTAN WAO akayageuza kuwa MAKAO YAKE MAKUU......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…