Wildlifer
JF-Expert Member
- May 12, 2021
- 1,884
- 5,235
Uwezo wa akili wa mwanadamu unapimwa kutokana na ufanisi katik kupambana na mazingira ili aweze kusurvive. Kwa msingi huo kila mtu ana akili kwa context ya mazingira yake. Mfano, huyo Muisrael sababu yeye ni jamii ambayo imeteswa, imetengwa na kuuliwa, so walihitaji kufanya waliyoyafanya ili waweze kusurvive. Na sasa anaishi middle east ambapo yupo kwenye hostile area, so inabidi apambane kwa kuwa na teknolojia za kumlinda dhidi ya mashambulizi mfano Iron Dome sababu ndio hitaji la mazingira yake au awe na silaha kali za kuwashambulia maadui zake, ndio maana anatengeneza silaha za masafa marefu kama hizo Ballistic Missiles.Tatizo ni kwamba kila mtu unayeona amefanya mambo makubwa chimbuko lake ni huko.
Ukitaja watu matajiri au wenye ushawishi na wenye uvumbuzi wa teknolojia chimbuko lao ni Israel.
Hivi unajua teknolojia ya Artificial Intelligence ilivyopindua meza kwenye masuala ya uendeshaji mitambo?
Unajua mvumbuzi wake ni asili ya wapi? Mark Zuckerberg unajua asili yake wapi?
A Journey to the smart world: Ifahamu teknolojia ya Artificial Intelligence na utendaji wake wa kazi
Nb. Siwaabudu Israel
Pia muhadzabe anayeishi kule Singida naye anaakili za kuishi katika mazingira yake, hivyo anateknolojia yake ya kutengeneza mikuki imara ya kuwindia na kuweza kwenda mbali (hii ndio Ballistic Missiles yake) ,sasa huyu awe na Iron Dome ya kazi gani wakati mazingira hayajamlazimu? Huyo myahudi unayesema ana akili, ukimuweka Porini Amazon, hawezi kuishi hata siku mbili, lakini mtu wa kabila la kayapo aliyeishi hapo miaka zaidi ya 1,000 atakuwa na akili zaidi yake. So, akili kila jamii inazo, na haipo iliyo bora kuliko mwenzake. Ukisema myahudi anaakili kuliko muhadzabe sababu ametengeneza Iron Dome, ni sawa na kusema simba ana maarifa zaidi ya samaki kisa tu anaweza kupanda mti.