Mnaotamani kuja Dar es salaam hii ndio dar yenyewe je! Mtaiweza?

Ungemwambia dereva asimamishe gari uchukue sandal yako sa mbona uliiacha
 
Mtu wa mkoani anaweza kuishi popote, hata hao wa Dar wengi wao walianza kuwa wa mikoani
Ila watu wa Dar sasa ndio inabidi muulizwe, maisha ya mikoani mtayaweza? Wengi wenu wanakaa kidogo mikoani wanashindwa wanarudi Dasilama 😆😆
Mikoani ni "ushenzini" kwa watu wa Dar
 
Nakumbuka kipindi kile Jonh Kijazi interchange haijajengwa pale ubungo tuliganda kwenye Mataa kuna Mzee mmoja alikua na lafidhi ya kisukuma " hii ndiyo mwendokasi? Siyoni hata huo mwendokasi wenyewe.
 
Usafiri wa kawaida tu ila kuna namna serikali inafeli , pia kama mtu hana ramani yakufanya huko daslamu bora abaki kijijini achunge mbuzi tu, kuliko kujaza ushuzi kwenye huo usafiri wa uma.
Unajua kijijini kazi ni kuchunga mbuzi tu acha kukalili watu wanapiga mishindo ya kutisha vijijin huko
 
Nikijaga dar pesa nyingi natumia kwenye usafiri ni boda tu
 
Acha kutisha watu
 
Hzo ni ng'ombe au wanyama gani uko daslam, apo zinabidi zimwagiwe maji kwa juu kila baada ya kilometres 10 kupunguza joto zisije zikafa
Kumbe ndio sababu huwa najiuliza hizi ng'ombe kwa nini zinaogeshwa kwenye gari?. Na mara nyingi zinasafirishwa kuanzia jioni sababu mchana temperature inakuwa tofauti na jioni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…