Mnaotumia TECNO smartphone, ni aina ipi unatumia unajisikia raha ya simu?

Mnaotumia TECNO smartphone, ni aina ipi unatumia unajisikia raha ya simu?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] basi watu wanavyo paparikiaaa, kuna mtu juzi kaacha kununua Samsung, kanunua Tecno ya macho 3, namtazama nasema hii
Huyo bado ana tongotongo yaan nichukue spark 10c af kuna samsung A series kali tu ukiachana na S series ambayo ndio top
 
Kuna mwanaJF alisemaga kutumia TECNO ni ujasiri wa hali ya juu sana, ni sawa na kujikata na kisu shingoni. Huwa nakaangalia katecno kangu ka batani, naishia kutabasamu tu.
Mkuu tupa hiyo tekno, kuna siku itakulipukia, utaitia ktk huzuni familia.
 
TECNO spark 3 ujue sitakaa nikakusahau kabisa maishani mwangu,ulinifanya nikailaani kabisa brand ya TECNO na wakati huo ndo ww ulikua wamoto kabisa sokoni,narudia Spark 3 umesababisha hata mtu akisifia sijui Camon 20 kuwa ni nzuri naona kama ananidanganya 😥,na kwa kipindi kile unaingia sokoni ulikua na sura na umbo na muonekano matata sana,mtu akikukamata mkononi bila cover anaonekana kashika simu kali sana,kenyewe kadogo dogo,kembamba,ki portable cha ukweli ila wiki ya kwanza kabisa kukutumia ukaanza mawenge ukiwa bado piru kabisa,dah spark 3 kuba ba'ako kabisa ww
 
Mbona sielewi. Yaani mi nataka maelezo na sifa kutoka kwa watu walotumia. Mazuri yake na mabaya yake. Na inanini na nini?
Hakuna kitu hapo mkuu,simu iko nyuma ya muda sana,hapo tafuta hata mchina wako wa 250k anamkalisha huyo,simu 1/2 gb ROM?,simu battery 3000 amp?,duh!...
 
Hata Sony sio mbaya, LG n.k ila sio Tekno, infinix na wajomba zake, hizo sio timu, ni takataka.
Kuna mwamba alinunua infinix mpya kabisa na receipt ya EFD kapatiwa😂,mziki ukaanza baada ya mwezi,chuma inazima na charge iko 70%+,akiiwasha inaleta mwanga mweupe kwenye kioo na haibadiliki,hapo unakuta alikua anatizama movie chuma imechemka mshale wa joto unasomea red😂,ila hilo tatizo linakuja kuisha lenyewe baada ya kama 2hours,chuma inakua imepoa,kesho tena hivyo hivyo hadi jamaa akaiingiza sokoni,ikatangaziwa dau mjinga mwingine akaingia cha kike kuinunua😂
 
Hivi mtu inakuaje unaingia mfukoni unanunua tecno, itel, infinix, vivo n.k unless uwe mwanafunzi au ndo smart yako ya kwanza.

Heri Samsung ya laki mbili kuliko tecno ya laki 3 au 4.
Mkuu
Ondoa Vivo kwenye list yako tafadhali
 
Back
Top Bottom