Tatizo lenu mnaujua ukweli ila mmekariri au hamjaelewa mada kwasababu tu mmeona mstari unaosema “kuna tecno bora kuliko Samsung”
Unaweza kukuta mtu anatumia iphone 6 lakini anaponda balaa Tecno spark go 2022......... yaani kwake brand ya Tecno ni kichefuchefu
Hapa hatulinganishi simu kwa miaka iliotoka(Samsung atashinda) hapa watu wanaongelea kwamba hakuna Tecno inayofaa kutumika wakati wanatumia Samsung za miaka ya nyuma na wanajiona bora kuliko Tecno za kisasa zilizo boreshwa
Mleta mada kaleta sifa za Tecno phantom wakati tupo mwaka 2023, ndio tukamwambia atafute hata spark za sasa ni bora kuliko midrange za zamani za sumsang....... hamtaki kabisa kusikia huu ushauri
Kwenu samsung hata miaka 10 nyuma itabaki kuwa bora kuliko Tecno yoyote ile