Ni siku ya leo nimekumbuka nikiwa kwenye mahusiano hapo miaka ya 2015 na binti moja mrembo, mapenzi yalinoga sana lakini baada yakuanza kuishi nae niliona mapungufu mengi sana, la kwanza kabisa alikuwa hajui kupika yani ugali sometimes unakuwa mbichi halafu hata hajishughulishi kuongeza mboga za pembeni wakati vitu vipo vya kutosha stoo, mambo ya kunishuguhulikia usafi wangu mwanaume wake kama kunifulia nguo nayo ni mpaka iwe vuta nikuvute tena jeans anafulia brush!!, Kwakweli taa nyekundu iliwaka kichwani suala la ndoa likafutika kabisa.
Kumuandaa mtoto wako wa kike kujua kuishi kwenye ndoa za kiafrika ni jukumu ambalo wazazi hasa mama hapaswi kulilazia damu,
Kuna wazazi tunawaona kwamba wakiwa na vijipesa basi wanamleta house girl amsaidie mtoto wa kike kazi ambazo inabidi azifanye yeye ili ziwe mazoea ya kumjengea uzoefu ya msingi ya kuwa mke anaeweza kuishi ndani ya ndoa za kiafrika.
Tutofautishe vitu viwili, kuna kufanya kitu kwa kuweza baada ya kujifunza na kufanya kitu kwa mazoea, unaweza ukajifunza leo hii kupika hata kupitia youtube ama goole lakini itachukua muda mrefu sana kujenga mazoea ya kupika, ila kama umeshazoeshwa tangu mtoto si kwamba tu unaweza lakini umepata uzoefu mwingi sana na tayari imeshakua ni mazoea, unapika bila kuhisi uchovu wala hujivuti, una enjoy kupika inakua sio shughuli bali hobby.
Sasa tukija kwa watoto hawa wanaolelewa kitamthilia inakuwa ngumu sana mwanaume wa kiafrika kumuoa maana sisi wanaume wa kiafrika suala la kwanza kwenye kuoa huwa "tunavuta jiko" hivyo vingine huwa ni vya ziada tu vikiwemo elimu, uzuri, n.k. na ukikosea ukifanya vinginevyo ujipange!! Jiko ndio kazi kuu ya mwanamke akiwa ndani ikifuatiwa na usafi wa mme wake kuanzia kumfulia nguo zake mpaka soksi, na majukumu mengine kama usafi wa nyumba, n.k.
Unakuta binti wazazi wake hawakumfundisha wala kumzoesha shughuli za kupika, matokeo yake huku kwenye ndoa anazidisha chumvi, wali boko, ugali mbichi, n.k. vinaanza kuwa kero, na hata kama anajua kupika anakuwa hana mazoea, anapika kwa kujivuta vuta sana, badala ya kujiongeza asubuhi amuandalie mme wake hata viazi vya kuchemsha yeye anaweka mkate tu, siku ya jumapili mmepumzika myumbani yeye wala hajishughulishi kupika anasonga ugali na mchicha wakati stoo kuna mchele wa kutosha, friji kuna nyama ya kutosha, yani anaona kupika pilau ni kazi nzito sana, Mwanaume anaanza kumuona mzigo tu.
Kufua nguo za mmewe wala hana muda anampa huse girl sababu huko kwao nae alikuwa anafuliwa ama hakuzoeshwa, ni mambo yanayotia aibu maana huu sio uafrika wetu, haijalishi hata kama mwanamke ana cheo kizito ni lazima amfulie mme wake nguo zake hizo ndio mila zetu waafrika tangu na tangu,