Mnaowalea watoto wa kike bila kuwafundisha kazi za nyumbani mnawaandalia mazingira gani wakiwa wakubwa?

Wazazi wanawaandalia unemployment
 
Dunia inabadilika lakini wewe hubadiliki. Yale mambo ya kizamani siku hizi yanapotea. Umejuaje hajui kusonga Ugali wakati wewe hujui? Na kama unajua kwa nini hukusonga au hukumwonyesha namna ya kusonga?
 
Sawa mkuu naona wewe endelea huko nyumbani kwako uwe unamfulia mke wako nguo, uwe unampikia mke wako, uwe unapiga deki, uwe unampokeza kupika kwenye misiba yeye awe anaenda na wanaume kuchimba kaburi, pia wezi wakija liwe jukumu lake kukulinda wewe.
Hujaweza kujenga hoja ya kimantiki na ya kidhahania bila kumhusisha mtu moja kwa moja?

Huu ni udhaifu katika uwezo wako wa kujenga hoja. Pia ni logical fallacy ya "ad hominem".

Unashindwa kujadili hoja, unaenda kumjadili mtu.
 
Dunia inabadilika lakini wewe hubadiliki. Yale mambo ya kizamani siku hizi yanapotea. Umejuaje hajui kusonga Ugali wakati wewe hujui? Na kama unajua kwa nini hukusonga au hukumwonyesha namna ya kusonga?
Automatically jukumu la kupika ni la mwanamke kama ilivyo kwa mwanaume kukabiliana na wezi nyumba ikivamiwa, not the other way around
 
Hujaweza kujenga hoja ya kimantiki na ya kidhahania bila kumhusisha mtu moja kwa moja?

Huu ni udhaifu katika uwezo wako wa kujenga hoja. Pia ni logical fallacy ya "ad hominem".

Unashindwa kujadili hoja, unaenda kumjadili mtu.
Jioni isjafika weka simu pembeni, wahi sokoni ukanunue nyanya na nazi, ukifika home toa mbuzi uikune naze, uvae kanga uingie jikoni, upepee kigae kiwake umpikie mkeo, usisahau kumpashia maji ya kuoga.
 
Automatically jukumu la kupika ni la mwanamke kama ilivyo kwa mwanaume kukabiliana na wezi nyumba ikivamiwa, not the other way around
Haya ni mawazo ya dunia ya kijima.

Dunia ya leo, si ajabu kukuta mwanamke ni mixed martial arts champion kaolewa na mwanamme ambaye ni professional chef.

Wanasaidiana kazi vizuri tu bila prejudice za gender roles.
 
Jioni isjafika weka simu pembeni, wahi sokoni ukanunue nyanya na nazi, ukifika home toa mbuzi uikune naze, uvae kanga uingie jikoni, upepee kigae kiwake umpikie mkeo, usisahau kumpashia maji ya kuoga.
Bado unaishi kwenye ulimwengu wa kukuna nazi na kupasha moto maji ya kuoga.

We have heaters for that, unafungua bomba hata dakika haifiki maji yashashika moto.

Ndiyo maana tangu awali nilisema hatuwezi kuelewana.

Tunaishi dunia mbili tofauti kabisa na sioni hata haja ya kuendeleza mazungumzo haya na wewe.
 
Hii ni jamii ya kiafrika na Mwanamke lazima ajue kupika na mila na desturi lazima zizingatiwe. mambo ya Gender roles na bla bla za usawa hao wenye nazo wenyewe kila siku talaka na balaa zingine kama hawana akili nzuri.
 
mabinti wa siku izi ukimwambia ishu ya kupika anakwambia kwani wew huna mikono ya kupika.
Yuko sahihi wewe ndie unakuwa umekosea kuoa ungeenda kuoa kijijini kwenu.Umezaliwa porini unakomaa kuoa mtoto wa mjini ambaye maisha yake yote kazi zote zinafaywa na Houseboy na House girl ikiwemo kufua nguo zake

Ungeoa saizi Yako mliyekua naye huko maporini vijijini kwenu usingekuwa na haya malalamiko

Kaajiri house boy na house girl wafanye hizo kazi
Makosa Yako fua mwenyewe na yeye atafua zake.Tena kajitahidi kama unaona Hadi nguo zake anafua kakuvumilia sana kwao hajazoea Hilo.Kutoongeza kesi fua mwenyewe nguo zako.

Kosa lako Kwa kutooa huko porini kwenu
 
Mwaume lazima ujue kazi zote..ila mwanamke kushindwa kujua hata

Apende asipende.........askuna anayelazimisha bali anashauriwa kuwa na hizo life skills muhimu.

Akitaka aache mbona wako wengi tu na hawafanyi na life linaendelea.

Kwanini wewe unataka kuamini Mwanamke akijifunza kupika ni mfumo dume?

Sasa hapo mfumo dume uko wapi?
 
Hii ni jamii ya kiafrika na Mwanamke lazima ajue kupika na mila na desturi lazima zizingatiwe. mambo ya Gender roles na bla bla za usawa hao wenye nazo wenyewe kila siku talaka na balaa zingine kama hawana akili nzuri.
Nimegundua Africa tunaishi maisha mazuri sana pamoja na umaskini wetu.

Wanawake wetu wanatupa raha sana na sisi tu awapa raha saba.
 
Kwani wapi nimesema mwanamke akijifunza kupika ni mfumodume?

Nimesema kupika ni life skill, kila mtu anatakiwa kujua, mwanamke, mwanamme.

Nimesema habari za kufanya kazi ya kupika kuwa ni kazi maalum ya mwanamke ni habari iliyopitwa na wakati, ni mfumodume.

Unaelewa tofauti kati ya mawili hayo?

Unaweza kufuatilia mantiki ya hoja yangu kwa nuance?
 
Mtoto/Mtu yeyote yule anapaswa kujua kuandaa chakula kwa sababu kula ni jambo la lazima.
 
Ndo hivyo bongo Bado sana!
Hawawezi kukuelewa
 
Kufua jmn isiwe issue
Kuna mashine sikuhizi😅
Kupika ,wote tujue,ya kesho hatuyajui!
 
Ndo maana ndoa zinageuzwa ajira na wanawake. Toa pesa ufanyiwe kazi zote. Huna pesa piga nyeto
Sisi jamii zetu tumehalalisha ndoa kuwa ni ajira.

Tena utumwa kabisa, ndiyo maana mwanamke ananunuliwa kwa mahari.

Na mwanamme anategemea mwanamke ampikie, tena anasema kabisa "nimepata jiko".
 
Binti yangu nahakikisha anajiwrka dunia ya mbele. Namfundisha namna ya kuwa na followers wengi kwenye social media na faida zake. Hayo mambo ya ujima eti mtoto sijui ajue kupika, kufua wafundisheni watoto wenu. Sisi tunasonga mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…