Mnapofanya Maendeleo msisahau kushirikisha ndugu zenu hata Kama mna ugomvi

Kuna Mtu mmoja naye alikuwa anajenga Nyumba yake ilifikia hatua ya kupauwa ghafla akawa haonekani wala hapatikani kwenye Simu, mmoja wa mafundi wake ambaye ni Mzee akaweka Bati baadhi ya vyumba akahamia, bahati mbaya Nyumba yenyewe ilikuwa kwenye eneo ambalo halistahili kujengwa zilipobomolewa Nyumba nyingine na yenyewe ikabomolewa.
 
Duuuh
 

Manzile:

Rafiki yangu alifiwa na baba yake, wakiwa msibani alitokea mzee mmoja aliyejitambulisha ni rafiki ya marehemu, alimwambia jamaa yangu ( ambaye ndiye alikuwa kaka mkubwa ) baada ya mambo ya msiba kumalizika waonane.

Baada ya msiba alipokwenda kumuona alimchukua mpaka Goba, na kumuonyesha eneo kubwa tu, na kumwambia jamaa yangu, kuwa Marehemu alimwomba amnunulie miaka mingi, lakini kila akimwambia afanye kitu alikuwa anasema subiri, Mzee huyo alitoa nyaraka zote na kumkabidhi jamaa yangu.

Kwa kifupi wanafamilia hawakuwa na rekodi yoyote ya shamba hilo katika mali za marehemu,, watoto waligawana, na pia kumjengea mama yao katika shamba hilo. Watoto na mke wa marehemu walikuwa hawajui chochote! Ni wema tu wa huyo Mzee kuirudisha mali kwa wahusika!

Hivyo mambo haya yapo!
 
Ukiona mtu kafanya jambo kwa siri ujue si kwa kupenda bali imemlazimu kufanya. Kwa familia nyingine ni bora waone matokeo kuliko mchakato wenyewe.
Inawezekanaje familia ikawa na chuki Kufikia kiwango hicho?
 
Mkuu Mungu akubariki, ebu pambana pitia maelekezo ya mdau ya kufatilia no yake ,wenda alishakufa ,na ameacha familia ipo inaangaika ,unaweza saidia sana
 
Sijui Kwa Nini watu wanakuwa na ujinga wa namna hii
Sio ujinga,unao mke unampenda vizuri unakuletea watoto sio wako.unakuta huko ndugu nao walikukataa ulikuwa mtoto haramu.
Mambo ni mengi hii dunia,kama hayajakukuta shukuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…