Speedaf ndio cainiao, mizigo inachukua maximum wiki 2 inakuwa imefika Tanzania, changamoto inaanzia hapa Tanzania, wakala wao ndio wanachelewesha kusambaza mizigo. Utakuta mzigo una zaidi ya wiki 1 upo Tanzania ila mteja hujapigiwa ukaupokee, kwa hiyo unasubiria mpaka upigiwe. Mimi nilishachukua namba ya wakala wa eneo langu, kwa hiyo mzigo nikiutrack na kuona umefika, nampigia kumuuliza kama ameshauchukua ananiambia nikauchukue. Speedaf wako bomba kuwahi kusafirisha mizigo kutoka China mpaka Tanzania, sema changamoto kidogo ipo kwa hawa mawakala wa Tanzania.