Mnapotengana mnawapa mzigo mzito watoto sio tu wakiwa wadogo bali hata wakiwa watu wazima

Mnapotengana mnawapa mzigo mzito watoto sio tu wakiwa wadogo bali hata wakiwa watu wazima

Athari za mdomo mchafu wa mke kwenye ndoa
1.Chanzo cha wanaume kuweka breki bar badala ya kumaliza Kazi au kuchelewa kurudi nyumbani, mme upoteza mda achelewi kurudi Ili ajenge confidence feki kupitia pombe Ili ajisaulishe kelele za mke.
2.Mme kuchelewa kurudi nyumbani na kuwahi alfajiri Sana kuondoka nyumbani kwa kisingizio cha kuwahi kazini au foleni.
3.Mme kushinda bar
4.Tatizo kubwa la nguvu za kiume chanzo ni kauli chafu au makelele ya mwanamke, tendo ni hisia uendana na utulivu wa akili.
5.Mwanaume kuwa na michepuko hapa anatafuta faraja,
6.Wanaume wengi kukimbia nyumba na kwenda kupanga au kuanza maisha kwingine.
7.Mabosi kuwa wakali au wanoko maofisini wote hawa ukali wao chanzo ni ndoa zao zinashida, boss mkali ni muoga ana shida anajifichia kwenye ukali kuficha yanayomsibu nyumbani kwako, kudili na boss mkali jifanye mjinga kuwa fala mnyenyekee atakuwa rafiki yako utakula mema ya nchi, ukitaka kushindana nae lazima akufyatue, maboss wakali wamevurgwa nyumbani ni wa kuwaonea huruma.Tiba usishindane nae.
8.
 
Kuuza nafsi yako au nafsi yako kuchukuliwa na shetani
 
Watoto tuliolelewa na mama wa kambo tunajua wenyewe tulichokutana nacho utotoni,,, mama wa kambo wa kwanza alikuwa ananipiga sana sijui kwa vile nilikuwa siwezi hata kumkimbia?

In short mimi na bro alikuwa anatuchukulia kama wanyama,,, niliuugua mapunye kichwani kwasababu nilikuwa siogeshwi. Mzee mwenyewe alikuwa mtu wa safari safari sana,,, halafu sasa akirudi maza anajifanya anatujaliii ila akitoka tu mateso yanaanza.

Tulilala mazingira mabovu sana kama watumwa, ila Mungu alitusimamia,, siku moja mzee alijifanya anaondoka kwenda safarini halafu baada ya siku mbili akageuka,,, alichokutana nacho huku nyuma siku hiyo ndiyo ukawa mwisho ndoa na yule mama.

Huyu mama mwingine yeye,, alitoka kwenye familia ya wake wengi alijitahidi kidogo,,ila wakija wajomba zetu kutupa hai wanapikiwa vyakula vya hovyo kabisa makusudi. Ila wakija kaka zake hata kama anapita tu wala halali home anachinjwa kuku,, yaani pirikapirika ileee mgeni kaja home.

Aisee jamani wewe sikia tu mziki wa mama wa kambo! Huwa natamani kuandika hata kitabu kwa niliyoyapitia. Mimi wanangu wote mama yao ndiyo atalea mpaka nione wanajielewa ndiyo mtu mwingine wife anaeza kumwachia.
Kama unawasiwasi na malezi ya mwanao nyumbani take care sana,,,watoto wanakutana changamoto nyie acha tu.
 
Yes kuna Umri ukifika hiyo ndio mbinu muhimu ya busara lakini pia yenye faida Kwa familia hasa watoto.

Lakini kama bado haujafika mbali, na bado hamjachuma Mali na nguvu bado unazo hapo option ni kupiga chini tuu
Hiyo Kwa wenye Imani ya Dini si Sawa,inamaana Una halalisha zinaa wazi wazi.

Swali linakuja lipi ni Bora kuenda kinyume na Mungu au kuamua kuachana na kila mtu apate mwenza wa Maisha,ambayo yatampendeza Mungu
 
Good!
Naongezea:
1. Ugumu wakati wa kuwatembelea wazazi. Inatokea wazazi wapo mikoa tofauti tofauti au mkoa mmoja ila sehenu tofauti tofauti; na wote wanataka kuwaona wajukuu wao. Hiyo adha ya safari usipime!
2. Baadhi ya changamoto zinapaswa kutatuliwa kimila; Kwa baadhi ya makabila Mila fulani hukamilika zijifanywa na wazazi wote; ikiwa wameachana, adha ni Kwa watoto
 
Hapo nimewashauri wasioamini Mkuu
 
Ahsante Sana Mkuu Kwa nyongeza.
 
Divorce Repercussion is very huge!!
Si kitu Cha furaha hata kidogo, utautesa uzao wako na utawatesa Hadi kwenye ndoa zao.
Divorce isn't funny at all, sikia kwa mwenzio.
 
Divorce Repercussion is very huge!!
Si kitu Cha furaha hata kidogo, utautesa uzao wako na utawatesa Hadi kwenye ndoa zao.
Divorce isn't funny at all, sikia kwa mwenzio.
Hii spirit ni kumuomba Mungu akusaidie ujizuie nayo,baada ya divorce wengi huja kujutia maamuzi yao.Ni SAwa na usingle parents ukiuanza hata uzao wako utakuwa hivyo hivyo
 
Kosa kubwa Sana la wengi ni kukiuka mkataba wa ndoa, ingefaa watu waweke wazi tabia zao zote uchumbani bila kuzificha maana hata ukizificha tabia zao Ili uingie ndoani zitaonekana na utaachika, Ili kuepuka laana ya talaka msifiche tabia zenu kwa wenza kama ni mzinzi show, kama ni mwizi, mlevi, mtukanaji, una hasira, nk sio unakuwa malaika Ili uingie kwenye ndoa ugeuke shetani kwa tabia ngumu maana pana watu Wana tabia ngumu Sana kuishi nao sababu ya malezi mabovu ya wazazi wao, unamlea mtoto vibaya anaenda kuwa kero kwa mwenzake hadi anaona nyumba ngumu anakimbia kumbe chanzo ni malezi yako mabovu.
Ewe mzazi huyo uliye nae sio mwanao ni mke na mme wa mtu mtarajiwa mlee vyema usipeleke kilio, maumivu, kifo, magonjwa kwa mwenzake, maana mtoto umleavyo ndivyo atakavyokuwa.
 
Hili bandiko langu limefanya niwaze kuhusu ndoa.

Ubinafsi wa wazazi hufanya mtoto alelewe na mzazi mmoja.

Wacha nikupe nyingine hii.
Watoto wengi wanaolelewa na mzazi mmoja pia hua na kasumba ya kuona kila mtu anapaswa kumsaidia iwe upande wa baba au mama hivyo kupelekea wajomba, mashangazi, bibi, babu na ndgu wengine kushiriki katika ukuaji na masomo yake.

Akifanikiwa huyu huo mzigo anaokua nao unakua si wa kitoto, watoto wa waliomsaidia nao watataka asaidie wenzie.
Acha tu ndg! Hata aliyetoa tu ushauri, aliyenunua kalamu ya bick (@ TSH. 50/-) anataka msaada wa kusomeshewa mwanae.
Wazazi walitelekeza mtoto kwa ndg wanamgombania awauguze, kusaidia wadogo zake, n.k
 
Acha tu ndg! Hata aliyetoa tu ushauri, aliyenunua kalamu ya bick (@ TSH. 50/-) anataka msaada wa kusomeshewa mwanae.
Wazazi walitelekeza mtoto kwa ndg wanamgombania awauguze, kusaidia wadogo zake, n.k
Acha tu mwanangu ni vizuri mtoto alelewe na baba na mama yake labda wawe wamefariki.

Hii ya kuwaachia ndgu unawapa mzigo watoto.
 
Back
Top Bottom