Mnasema vijana hawachangamkii fursa? Wakati mnapiga pesa

Mnasema vijana hawachangamkii fursa? Wakati mnapiga pesa

mirindimo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
1,155
Reaction score
2,704
Hii inatia hasira sana hizi hela zimeliwa kama muchwa bila huruma yaani zimepigwa vikundi hewa hivi viko vya kutosha watu wameingia front wakapita na hizi pesa bila aibu
===

Vikundi hewa 30 vyakopeshwa fedha za halmashauri Mwanza Bilioni 4.9 zayeyuka
Imebainishwa kuwa jumla ya vikundi hewa 30 vya wajasiriamali wenye ulemavu, vijana na wanawake katika halmashauri za Mkoa wa Mwanza vimekopeshwa fedha huku jumla ya Sh bilioni 4.9 zilizokopeshwa kwa vikundi hivyo zikiwa hazijarejeshwa.

Pia Watumishi wa Serikali katika Halmashauri hizo wamejikopesha fedha kinyume na sheria za mikopo hiyo huku baadhi ya vikundi vikipewa mikopo wakati havijamaliza kulipa mikopo ya awali .

Hayo yamebainishwa leo Aprili 25, jijini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu katika kutoa fedha za mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya ujasiriamali kutoka katika makundi maalumu huku akiwataka wote waliohusika kwenye ubadhilifu huo kulipa fedha hizo Sh bilioni 4.9 ndani ya miezi mitatu kuanzia leo.

Mhandisi Gabriel amesitisha utoaji wa mikopo kwenye halmashauri zote za mkoa huo kwa siku 30 kuanzia leo Aprili 25, ili elimu ianze kutolewa ya kanuni, taratibu na sheria za utoaji wa mikopo hiyo lengo likiwa ni kuimarisha usimamizi wa fedha na kutathmini utekelezaji wa kanuni hizo kutoka kwenye serikali za mitaa.

“Kwa miaka mitatu tunadai Sh bilioni 4.9 tukiendelea kutoa mikopo tutaongeza deni kubwa na bado kanuni na taratibu tumezikiuka lengo ni kuimarisha taratibu na kanuni za utoaji mikopo, sio mambo yanakwenda tu kama fedha hizi hazina mtu, hii sio zawadi wengine wanasema hii ni fedha ya serikali tuile tu, fedha ya serikali inalindwa kwa kanuni na sheria unapoitumia na unapokopa usiirejeshe unamzuia kijana, mwanamke au mtu mwenye ulemavu mwenzako asinufaike.

“Tutaendelea kufuatilia taarifa kwa kina ili vikundi ambavyo havijajulikana viko wapi waliohusika kuvipa fedha watatusaidia kuvitafuta na ikibainika ni vikundi hewa wahusika waliotoa mikopo watachukuliwa hatua mara moja ikiwemo kurudisha fedha hizo pia naelekeza halmashauri zote ziweke mpango huo wakurugenzi na wakuu wa wilaya watoe mpango kazi wa kurejesha fedha hizo ambazo marejesho yamekuwa muda mrefu sana,"amesema Mhandisi Gabrieli.
 
Kuna Mkuu wa Wilaya nahis huko Arusha Jana kasema

Vijana wachangamkie Fursa ya Filamu ya Royo Tuwa
 
20220421_075608.jpg
 
Back
Top Bottom