Mnataka kumbebesha Hayati Magufuli madhambi yenu?

Ni kipi ameandika kisichoeleweka hapo ww, nimemjibu ninavyotaka Mimi, sio unavyotaka ww. Kama ulikuwa unamuona Magufuli ni kiongozi Bora, Kuna walioona Kaburu Pieter Botha alikuwa mzuri na mzalendo kwa nchi yake.
Yaishe mkuu🙌🙌
 
Na ukakoma kwani Sasa hivi hakuna watu katili tena. Au anaendeleza ukatili akitokea ahera madukani.?
Kinachowatesa ni chuki binafsi dhidi ya Magufuli. Hakuna mwenye hoja za maana.Mimi toka nakua naona CCM wanaiba Kura tena kuna watu wanapotezwa. 2001 watu walikimbia makazi Zanzibar na kuwa wakimbizi lakini mtu anakuambia hakuna uchaguzi mbovu kama wa 2020.Huwa sijui wanatumia references gani.
 
Kwamba hatujui wizi katika uchaguzi kabla ya 2020, na uhayawani wa 2020? Ni hivi, kabla ya 2020 kulikuwa na wizi kwenye chaguzi, 2020 haikuwa wizi katika uchaguzi, Bali dhalimu magu alipora mchakato wa uchaguzi.
Kwahiyo before 2020 hakukua na udhalimu?
 
Ndiyo CCM hiyo. Na kila awamu ina watetezi wake wasio na haya wala kuona ubaya wake.

Lishakuwa jinamizi lenye sura na maumbo tofauti tofauti. Wanaokosoa mauaji ya Mwangosi, bomu Arusha (CDM) na mauaji Zanzibar (CUF/ACT) hawaoni ubaya kwa yaliyowapata kina Lissu, Akwilina, Lwajabe, na Gwanda. CCM ile ile inayowalaani CHADEMA na kuwaombea kifo usiku na mchana!
 
Siamini ni wewe kweli umeandika hivi au hii ID anatumia mwanao kwa sasa??

Hivi huamini kuwa kulikuwepo na umwagaji damu wa kutisha kwenye uchaguzi 2020 especially Zanzibar ambapo kuna picha sidhani kama itapendeza sana nikiziweka hapa kwa sababu za "utu" hasa kuwakumbusha machungu waliopotelewa na ndugu zao achilia mbali waliopotezwa bila kujulikana na hawa wale waliotimkia huku majuu kunusuru maisha yao!

Magufuli hujiulizi kwanini katika historia ya chaguzi za vyama vingi kwa mara ya kwanza huduma ya internet ilizimwa tangu October 28 hadi November 3 , 2020.

I really doubt kama huyu ni MM ninayemfahamu au hii ID anatumia mwanao???
 

Sijashuhudia chaguzi za Tanzania nikiwa nchini tangu 2000 ila ile 2020 japo hata huko nyuma teknolojia haikuwa kubwa ila 2020 live live kura tulizokuwa tunaambiwa ni za kuingizwa kwenye mabegi zilionekana mtandaoni.

Hii ni uthibitisho na motive behind ya kuzimwa internet kwa siku 5 !

Ni ushahidi tosha asilimia 83% alizojipa Magufuli huenda hakufika hata nusu ya kura za kutangazwa mshindi.

Hili ni doa kubwa sana kwenye utawala wake na haliwezi kufutwa kirahisi kama mnavyodhani.

Leo hii katika bunge lile haramu aliloacha kuna haramu namba 2 yaitwa Covid 19! Wabunge wasio na chama na bado ni wabunge, very ridiculous.
 
Na walimu ni watu wa hovyo sana, wametumika sana mbwa-mbuzi hawa 2020.
Ndio mana hawaongezewi wala kuboreshewa maslahi hili wabaki kuwa watumishi watumwa.
 
Huyo kiongozi bora anapatikanaje?
 
..kama kuna madaraja ya uhalifu wa kisiasa Magufuli na genge lake wako daraja la juu kuwazidi wenzao.

..kwa mfano, shambulizi dhidi ya Tundu Lissu, unaanzaje kumtetea Magufuli kwa ushenzi wa kiwango kile?
Shambulizi la Tundu Lissu lilikuwa baya na ni sawa na shambulizi la Dr. Ulimboka na akina Kibanda, hata hivyo finally Hawa wote wapo hai. Lakini Shambulio baya zaidi ni lile mfano la General Kombe, Mwangosi na Dr. Mvungi maana Hawa walishambuliwa Hadi kufa Tena enzi zisizokuwa za JPM.
 
Hoja ya ajabu sana hii. Yaani JPM kwa kuiba, kupora, kutesa na kuua wakosoaji wazi wazi (juu ya kapeti) basi anakuwa Rais bora sana kwa vile alikuwa transparent; hakuwa mnafiki kama hawa wengine!

Kama hayo ndio machaguo yaliyobakia kwa Watanzania chini ya CCM basi CCM ni msiba mkubwa sana wa taifa hili. A real national TRAGEDY!
 
Hawa jamaa wanadhani tumesahau Nini kilifanyika kwakuwa vyombo vya habari vilidhibitiwa. Ama wanadhani kwakuwa wao wamesahau, basi na sisi tumesahau.
 
Kama bajeti ipo, mshinikizeni afute huo uchaguzi. Ni wapi Mimi nimeonyesha kuwa na imani na huyo Samia, au kuamini hizo hadaa zake? Ninachojua Samia Hana siasa za kipuuzi kama dhalimu Magufuli fullstop.
Huyu dhalimu amesha set standard za nchi mtanyooshwa kwa principle za dhalimu kwa miaka 100 ijayo

Kwa Sasa ni utekelezaji tu
 
Nimezungumzia mtazamo wangu mkuu.
Japo kiuhalisia CCM imeoza kuanzi shina mpaka matawi.
Hata jae malaika akiingia CCM atakua shetani tu.
Ila kwa marais wote bora Magufuli aisee kwanza alijitahidi kiutendaji pili alikua transparent sio kama hawa wengine UNAFIKI MWINGI MAPAMBIO KIBAO KUJIPAKA MAFUTA KWA MGONGO WA CHUPA.
 
Mara kadhaa huwa napenda sana kusoma michango yako hakika huwa unafanya vizuri sana,lakini hili la jambo la the state Mimi binafsi huwa naona kama history za vijiweni tu.

Kwa maana kwamba taifa lipo katika hali mbaya sana hasa kwa wasio nacho,Kazi ya hiyo the state nini hasa ? Wapo kwa malengo ya nani na kwa faida ya nani.

Maana naona hao hao ndo majizi na walinda wezi.
 
Wale jamaa huwa wanakosa meno kiutendaji kwasababu ya katiba iliyopo!yaani wameona katiba ndio ingewasaidia ,lakini tatizo upinzani NAO wanafika bei wakiahidiwa mkate wanafyata!!

Karata ya mabadiliko Huwa ni vyama pinzani na wananchi,Sasa pale upinzani unapoanza kulegea kisa nusu mkate ndipo na wale jamaa juhudi zao zinapata dosari hasa utekelezaji wake!!

Njia pekee unayobaki ni kifo,Sasa kifo hakileti tafsiri nzuri kwenye jamii!!

Mimi ningewaelewa upinzani kama wangestiki na hakuna uchaguzi kama hakuna katiba mpya na tume huru!ningewaelewa!

Hilo lingekua chachu kubwa ya mabadiliko makubwa nchini!!

Hao jamaa wapo japo hawaonekani kuwa wapo na KAZI Yao ni kubwa,japo kazi zao Zina changamoto coz wakati mwingine wanakua kwenye presha ya Katiba na sheria!

Katiba na Sheria zinalinda Sana walioshika hatam kuliko Raia na maslahi yao!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…