JKT lengo lake kubwa sio kutoa ajira bali ni kumjenga kijana kwa kumpa mafunzo ya awali ya ulinzi na usalama, kumfundisha kazi na ukakamavu haya ya kutumika kama chujio la ajira ni secondary aims Kama vile ambavyo lengo la elimu ni kutoa ujinga na sio ajira, Ajira itakuja baada ya kutoa ujinga.
Cha msingi unapokuwa JKT jaribu kuigeuza kama fursa kwako fanya kazi ,kuwa mbunifu, acha uvivu na kufuata mkumbo, kuwa mdadisi show them why they have to take you utapata tu hizo nafasi tena nafasi nzuri tu mkuu, Wako vijana wenye uthubutu na ambao wapo vizuri upstairs Serikali inawahitaji hasa kwenye kada za ulinzi na usalama.
Tatizo letu huwa tunakumbuka shuka na kushakucha ingawaje sipingi kuwa connection zipo na hii ni kila sehemu kwenye kila sector ndio mfumo wa dunia mkuu.
All in all usikate tamaa omba kila nafasi zikitoka na mtangulize Mungu.