Mnatuchukua vijana kutulimisha JKT, Ajira zikitokea mnaajiri watoto wenu

Mnatuchukua vijana kutulimisha JKT, Ajira zikitokea mnaajiri watoto wenu

[emoji25][emoji25]Inaumiza sana watoto wa maskini wanaenda kupigwa KNock Out
 
Ahahahah
Mtamkumbuka Kikwete.
Shetani la ukosefu wa ajira hapa nchi lilikuja na Magufuli. Samia anajitahidi kuajiri lakini Ngoma ngumu maana ana ummati wa vijana wa jiwe na vijana waliohitimu katika uongozi wake.
Magufuli kaharibu nchi ingawa wajinga humwabudu kila siku.
Mtanyooka mbona.
Kipindi cha Kikwete polisi, Magereza au fire wakija kuandikisha vijana jkt ili wawaajiri vijana tulikuwa tunakimbia . Leo hii hata sungusungu wakienda kuandikisha vijana jkt vijana watauana
Kikwete gani mkuu? Miongoni mwa utawala wa hovyo kuwahi kutokea TZ ni utawala wa huyu mzee. Hizo ajira unazosema mlikua mnazikimbia makambini ni mwaka gani mkuu? Wakati ni miaka ya 2010's watu walikua wakijazana ama uhuru au taifa ama sabasaba kwa ajili ya usaili wa hizo taasisi ulizotaja.
 
Hakuna hata mmoja anaelazimishwa kwenda JKT, ni sisi wenyewe kwa nia zetu tunaenda. Achana nazo hizo mkuu, njoo Ruaha huku kitunguu kimekubali laana. Pia tunajiandaa kwenye kulima mpunga Ubaruku kule.

Ajira ni chache ila kazi zipo nyingi sana.​
 
Back
Top Bottom