Kweli.
Kuna stress ikikupata hata hamu za mapenzi huzipati. Na unaweza ukalichukia hilo tendo kabisa.
Kila kitu unachopendelea kukifanya huo wakati kinakuwa hakikupi furaha tena.
Hauwezi kusema utoke uende disko au sehemu ya starehe maana hata ukifika huko hata pombe hazipiti na mziki hauusikii.
Kukaa na watu napo unaona ni tabu.
Ilinipata hii hali. Ilikuwa sitoki kitandani na haimaanishi kwamba nilikuwa nina usingizi, hapana. Ni kulia tu, na kumeza antidepressant. Ikafika hatua nazo zikafeli.
Hii hali haitaki ufanye chochote. Kula ni kwa kujilazimisha na hapo kinakukaba. Simu ndio kabisa hautaki hata kuishika maana hamna cha kufurahisha huko. Nisiongelee nilikaa siku ngapi bila kugusa maji (lol). Nilikuwa kama kichaa. Sitoki ndani na siogi. Niliwaza hadi kufanya drugs. Bila kusema mara ngapi nilitamani kufa.
OP, chochote unachopitia, tafuta mtu uongee naye kabla hali haijawa mbaya.