Pole sana,,muhimu ni kukubali kwamba hiyo ni hatua tu na itapita. Hakuna kitu au jambo ambalo linadumu milele. Hali zote ambazo tunapitia katika maisha huja na kuondoka. Kuna majira kwa kila jambo. Ikubali hiyo hali lakini usipambane nayo. Amka asubuhi, fanya mambo mengine yaliyo kwenye ratiba yako. Angalia yaliyo ndani ya uwezo wako. Usilazimishe kufanya jambo ambalo lipo nje ya uwezo wako. Jipe nafasi na uiche akili ifanye kazi kwa ku-relax. Hata kama unaona dakika chache baadae hutakuwa na uhakika wa kufanikisha kupata chakula, usipaniki kwa kutaka kufanikiwa katika hilo. Tulia na panga akili vizuri. Usifikirie sana kuhusu mambo yaliyopita. Wakati ni sasa, ishi, vumilia, jipange na utashinda. Nina rafiki yangu ambae amepitia magumu sana, japo hayajaisha lakini alipokubali kwamba ni wakati tu utapita, angalau uso wake unaanza kung'aa tena. Zaidi ya yote, Mungu wa mbinguni akutunze na kukupa faraja na maarifa yapitayo mawazo ya wanadam ili ufanikiwe tena. Barikiwa!