Mnatumia njia gani kukabiliana na msongo wa mawazo (stress)?

Mnatumia njia gani kukabiliana na msongo wa mawazo (stress)?

Siku ya jana,leo na sijui hiyo kesho itakwendaje napitia msongo mkubwa sana wa mawazo najaribu kujiliwaza na kujifariji pamoja na kujichanganya na watu ila nikikaa kidogo na kufikiri najikuta na rudi katika huzuni na mfadhaiko wa nafsi sio siri nakosa raha na hamu ya vitu vingi naomba mbinu ya kujikwamua
Kama kuna mtu alishapitia hali hii naomben msaada. Pia mimi sio mlevi wala situmii kileo chochote.
Dah pole sana, Mimi pia huwa napitiaga kipindi kama hicho, huwa sitamani kufanya chochote lakini baada ya muda hali hiyo huwa inaisha, always time heal, jipe muda tu itaisha.
 
Niko na hiyo hali sasa, najitibu kwa kuangalia series mwanzo mwisho. Ratiba yangu iko hivi, nikirudi job saa kumi na mbili nakoga na washa TV naweka series hadi nachukuliwa na usingizi. Movies, series ndio kilevi nikipendacho.

Nimenza na breaking bad, nimemaliza, black list, sasa naangalia shooter. Hii miezi ya mwisho wa mwaka kwangu mara nyingi inakuwa poa ila mara hii msala umeanza Oktoba mwanzoni hadi sasa. Nimejaribu kusolve na nashukuru njia hii ya kuangalia series imeniondolea stressess na imenipa muda wa kutafakari changamoto zangu nizitatue vipi.

Nashauri tafuta kilevi chako ulewe nacho, naomba unifahamu tafadhali, sikushauri unywe pombe tafuta kilevi chako.

Karibu
 
Hebu tuambie ni kitu gani kinacho kusababishia wewe msongo wa mawazo
 
napanda 'street fighter' Civilian moja iko njema sana, hairembi, uyoo mpaka Tabata, nagonga sana Makange na smoothies za kutosha

narudi mpaka Gomes, nasubiria 'Konde Boy' TATA, uyoo mpaka home, napiga kimoja nalala
Oa wewee
 
Swali, salio pray pray pray harder wallahi mawazo na stress zinaisha kama huna dini fanya meditation
 
Swali,Salio pray pray pray harder wallahi mawazo na stress zinaisha kama huna dini fanya meditation
Nashukuru ndugu najitahid kuswal napata relief kwa mda tatizo mawazo yakinijia najikuta napata mfadhaiko tena sio siri usiku nauogopa maana ndo mda unakuwa peke yako ninachoshukuru Mungu sijafikia stage yakukosa usingiz
 
Fanya maisha yako rahisi na ondoa kutaka visivyotakikana wala kufikiri visivyofikirika. Stresses nyingi zinaletwa na usasa utokanao na ubepari na kutamani usichoweza au kuataka kupata kingi au kujipa haki hata usipostahiki.
Asante sana ndugu stress zinazonikabili hazichangizwi na tamaa ya kitu chochote kuna mambo natakiwa kuyatatua yananipa utata sana njia zipo ila pengine ndo ninaweza nikawa najichimbia shimbo kabisa
 
Pole moja ya vitu hatari sana ni msongo wa mawazo nakushauri usitumie kilevi chochote,bange au madawa ya kulevya.
Asante sana nashukuru siko kwenye kundi hilo japo napata msukumo mkubwa sana ila najitahid naamini nitavuka hii hali
 
Back
Top Bottom