Mnatumia njia gani kukabiliana na msongo wa mawazo (stress)?

Pole professor,

Binafsi ikifika mahali kiasi Cha stress zinasababisha kushindwa kabisa kupiga kazi (nafikiri nimeeleweka), hapo ndugu waanze kupewa taarifa wajiandae Kwa msiba.
Asante The Monk.
Sasa hivi haiwezi kukutokea maana unajua namna ya kupambana na hiyo hali.

Thank you for helping me through my depression Dear. Asante kwa kuwa na mimi katika hicho kipindi.
 
Asante The Monk.
Sasa hivi haiwezi kukutokea maana unajua namna ya kupambana na hiyo hali.

Thank you for helping me through my depression Dear. Asante kwa kuwa na mimi katika hicho kipindi.

Ahsante Professor,

Maisha Yana mambo mengi na mawimbi ya Kila namna yanatupiga sote Kwa nyakati tofauti tofauti. Uzuri kadri tunavyopambana nayo, ndivyo tunaimarika zaidi.
 
Tiba kuu ya msongo wa mawazo kwangu ni kuwaza neema zingine nilizopewa kulinganisha na tatizo linalonikabili.

Nawaza kwamba kila kitu si kitapita,mbona mwaka juzi nilipata tatizo fulani nikawa na stress but now limepita ? Aaah basi na hili litapita.

Huwa najipa moyo kwa namna hii na huwa nafanya mambo yote yaliyo kwenye ratiba zangu
 
kuwa positive sio tatizo,kinachoumaga ni ile merry-Go-around
ni kama upo kwenye Maze, hutoki kila siku tatizo ni hilo hilo tu
 
Mimi niliwahi kwenda barabarani usiku majira ya saa 8 hv nikakuta kuna mzee homeless amelala nje ya fremu ya duka, nikamuomba tuzungumze....akakubali nikaamua kumshirikisha matatizo yangu mtu asiye nifahamu....niliongea vyote bila kuficha chochote, huwezi amini yule mzee alinipa ushauri mzuri sana pengine nisingeweza kupata hata kwa washauri wenye taaluma zao, nilichojifunza tusiwadharau wasio nacho...wengi wana hekima na akili sana sema ni vile tu maisha yao yamekuwa hivyo yalivyo lakini hii dunia ina siri kubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…