Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

wezi sana hao MKUU mm huwaga nawasikia sana mnavyo danganywa .kweli wajinga mjini hawaishi
 
Du! Yaani jamaa wametoa ushuhuda wa mafanikio balaa, mpaka nimeingia line. Lakini.......
 
Kuna jamaa yangua alianzaga kwa mbwebwe of making a milloons..dahhh tukaenda aiseee adi tukaanza kutumia bidhaa wenyewe.hahahahahhh hao watu kama wale wa promotion zu.wanakutia ujinga ukijaa tu umekwenda na maji.
 
maoni gani sasa kwan sisi tunajua semina yenu? We tulia upate ulichofata.
 
Wanajamii napenda kuwauliza maswali kadhaa juu ya mada niliyoitaja:-
  1. wadau humu jamvini wanaojua juu ya hizi bidhaa za "forever living" wauzaji wake wamezagaa kila mahali, kwenye mabasi, mitaani, nk. Kuna nini ndani yake?
  2. halafu ukishakuwa mteja wa muuzaji mmoja kama mara kadhaa anaanza kukuomba ujiunge uwe muuzaji. Eti yeye kwa kupata mtu akajiunga kama muuzaji mpya anapandishwa cheo. Ni nini undani wa siri hii?
  3. bidhaa zao zina akisi mmea wa "aloe vera". Najiuliza pia mmea huu sijasikia sehemu yo yote duniani maarufu kwa kilimo cha "aloe vera" kama ilivyo kwa chai, kahawa, ndizi, miwa, nk. Ni sumu gani hii wanayotumia?

nawasilisha kwenu kwa usaidizi
 
Hizi bidhaa za USA ni hatari sn, refer Monsanto agricultural products, watu wengi wa kanda ya kaskazini wanajua hii kampuni ya kuuza mbegu za kilimo, dunia nzima haitakiwi, imebaki Tanzania ndio bado tunatumia bidhaa zao
 
Angalia. Usije ibiwa, yaani apande cheo kwa wewe kununua na kujiunga? Cheo gani? Ugumu wa maisha huu unawafanya watu kujitoa fahamu.
 
GNLD & FLP ni matapeli wa hali juu. Pia wanadumaza akili za watu.
 
Hivi unapokuwa ndani ya forever living unakuwa umeajiriwa au umejiajiri mwenyewe?? pili mpaka sasa bado nashindwa kuilewa hii biashara kila nikijitahidi wapi kwa mwenye kuifahamu vizuri hii biashara naomba anielezee kiundani kuhusu hii kampuni
 
Kama umejiunga itakula kwako biashara ngumu hatari hasa kupata wateja rafiki yangu alikuwa kwenye hiyo forever yakamshinda na wanakuwaga na stori tamu kukuvutia u join mara utakua bilionea
 
Back
Top Bottom