Now back to you super idiot
LIKUD.
Graduatism sickness ni ugonjwa mbaya kuliko ukimwi. Imani ya kwamba ukiwa graduate basi unastahili kipato fulani hata kama huna kazi ni UPUMBAVU (ukimind nipeleke mahakamani).
Namna yako ya kusema kwamba kwa graduate laki sita ni fedha za kuzipata kwa siku, ni sawa na kusema kuwa maafisa wote wa serikali kwa level ya TGS D ni mataahira kwa kuwa wamekubali kufanya kazi kwa mshahara wa shilingi 349,270 kwa mwezi ambayo ni karibu nusu ya hiyo laki sita.
Unapozungumzia mafanikio, basi ni suala la ulipokuwepo awali na ulipofika. Huyo anayejisifia kuwa amefika Nairobi ni haki yake. Sijui ni nini cha kushangaza hapo kwa mama Tupele aliyekuwa anauza vitumbue kwenye mavumbi pale vingunguti akiinuka kiasi cha kuwa na biashara inayomfanya asafiri hadi Nairobi.
Hauna haja ya kuwatukana watu kwa kuwa umekosa courage ya kufanya wanachofanya. Wewe kaa na makaratasi yako ya degree lakini wenzako wana namna yao pia ya kutafuta mafanikio. Network Marketing haijaanza Tanzania, imetokea huko kwa waliokufundisha DEGREE badala ya JANDO NA UNYAGO, na inaendelea si kwamba imesimama.
Pale Arusha yuko mama mmoja alikuwa fundi cherehani, sasa tunavyoongea ni MILIONEA sababu ya FLP. Mimi
Mwana Mtoka Pabaya ni member wa FLP na nilitambulishwa huko na member wa JF. Hata sasa membership yangu ni hai LAKINI mimi sikuwa na courage ya kuendelea na biashara hiyo, ila ninafaidika kwa punguzo la bei kwa products za FLP kama member.
Kushindwa kwangu kufanikiwa kwenye Network Marketing hakunifanyi niwatukane. Like any other business it take a lot of efforts and enthusiasm to cross the berriers;
I AM NOT COURAGEOUS na nimeshindwa, lkn sisemi kuwa ni mbaya.
La kama unafikiri ni utapeli basi hiyo ni level yako ya ujinga inakuongoza. Mimi sina cha kutolea ushuhuda kiuchumi lakini kitabibu ninacho. Wakati nikijaribu jaribu kufanya hiyo biashara, nilimuuzia jirani yangu dozi ya
gout, amepona na yeye amekuwa member na anafanya biashara hiyo huko kwao Kilimanjaro. Ajabu ni kwamba, yeye amefanikiwa kibiashara kwa kuwa kila aliyemuona na magongo sababu ya gout alitaka kujua ameponaje, kwa hiyo soko lake limekuwa kubwa kwa ajili hiyo.
Ningefurahi kama ungechukua calculator ukazidisha
600,000 kwa siku
365 na kutuandikia jawabu hapa ubaoni. Nafikiri utawasaidia GRADUATES kutambua level yao ya mapato kwa mwaka.