Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Kuna dada amenifuata nihudhurie huo mkutano. Baadae nikapewa siri ukihudhuria na kujiunga aliyekupeleka anaongezewa mshahara kwa kutumia umbumbumbu wako. Baadhi ya bidhaa amezileta dukani kwangu wala hakuna hata mteja anayezitaka wala kuziuliza. Ni zaidi ya Escrow.
 

Attachments

  • 1418484704722.jpg
    1418484704722.jpg
    33 KB · Views: 366
Kuna rafiki yangu wa damu jana alikuja kwangu akiomba nimshauri kuhusu mke wake kulazimisha kujiunga forever living. Mke wa huyu jamaa yangu ni nurse na yeye ni mfanyabiashara. Mke wake baada ya kushawishiwa na rafiki yake wa kike ambaye mme wake ndo yupo forever.

Baada ya kukubali kujiunga akakopeshwa hela ya kujiunga, jamaa kamind sana. Maana alishirikishwa akakataa. Me nimemushauri amuache aone maendeleo yake ila jamaa kamind mno mpaka waligombana. Hebu tupeni mawazo yenu tumsaidie kumshauri kama wanajamvi!
 
Usipoteze muda kumshauri mtu asiye na akili, mwenzake anajaribu fursa za kibiashara yeye analeta ujima.
 
Usipoteze muda kumshauri mtu asiye na akili, mwenzake anajaribu fursa za kibiashara yeye analeta ujima.

Si kweli huo ni upuuzi mtupu flp. Ni freemasons. Mke wangu alikuwa huko hamna kitu nimepelekwa amerika kama mzigo na nimegoma kujiunga fanyeni kazi kwa haki..
 
Kuna rafiki yangu wa damu jana alikuja kwangu akiomba nimshauri kuhusu mke wake kulazimisha kujiunga forever living. Mke wa huyu jamaa yangu ni nurse...na yeye ni mfanyabiashara. iMke wake baada ya kushawishiwa na rafiki yake wa kike ambaye mme wake ndo yupo forever. Baada ya kukubali kujiunga aakakopeshwa hela ya kujiunga...jamaa kamind sana. Maana alishirikishwa akakataa. Me nimemushauri amuache aone maendeleo yake ila jamaa kamind mno mpaka waligombana. Hebu tupeni mawazo yenu tumsaidie kumshauri....kama wanajamvi

Hii ipeleke kwenye Jukwaa la Biashara si huku tunajua siasa tu, kule ndo kunawafanya biashara wa kila aina.
 
Hayo ni mawazo yako. Wewe unajua maana Freemason?. Wewe unaangamia kwa kukosa maarifa. Unaposema Freemason uwe na uhakika. Usiwanyima wenzio fursa. Kama hutaki fursa wacha wenzio wachangamkie fursa..
 
Mkamateni na mpelekeni kwa makanisa ya upako akafanyiwe maombi...
 
Ilitakiwa ampinge kabisa huyo mwanamke kwa kushindwa kutii amri bila shuruti. Huyo aliyemuigiza forever tayari ana asilimia ya pesa kwa huyo mdada kiziwi. Hawako karibu na masikini.
 

Attachments

  • 1422889009804.jpg
    1422889009804.jpg
    42.2 KB · Views: 375
Kuna haka kamchezo kengine,nadhani kanahusisha kujiunga na zantel halafu bla blaa blaaa. Nilipigiwa simu jana na dada moja wala sikumuelewa vizuri, mwenye ujuzi atufahamishe hapa pia
 
Pole LIKUDI mimi mwenyewe yalinikuta, dada mmoja yuko GNLD kanialika na kunielezea mafanikio kibao nikajua labda atakuwa na mafanikio balaa.cha kushangaza huyohuyo tena siku nyingine ananipiga mzinga akidai ana mmahitaji mengi ya mtoto anaomba nimsaidie hela.japo nilimpa pesa aliyotaka lakini nikadharau kila kitu alichoniambia kuhusu GNLD.
 
Last edited by a moderator:
Kuna dada amenifuata nihudhurie huo mkutano. Baadae nikapewa siri ukihudhuria na kujiunga aliyekupeleka anaongezewa mshahara kwa kutumia umbumbumbu wako. Baadhi ya bidhaa amezileta dukani kwangu wala hakuna hata mteja anayezitaka wala kuziuliza. Ni zaidi ya Escrow.

Hivi hizi makitu zina TBS?
au wazee wa Chakula na Dawa wamekula Rushwa.
 
Back
Top Bottom