Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hao jamaa wamebobea kwenye lugha ya ushawishi sijapata kuona......yaani unaweza kuacha kazi yako nzuri kwa maneno yao matamu....ndio maana wanawakamata sana wadada.....Wanajua wakisema hautoenda,ila ukienda bila kujua utakutana na watu wana upako wa kushawishi utaletewa watu waliofanikiwa na hiyo bizness mpaka mwenyewe utaona yes hii ndio bizness ila kati ya 100 wanaoingia anaofanikiwa ni m1 tu au hakuna kabisa.
kuna mwanamke mmoja anajihusisha na forever living product,sasa anapotaka kumkamata mtu ili kumuingiza kwenye biashara hii ya forever hasemi moja kwa moja anasema oh kuna biashara flani ya ujasiria mali nzuri tu kwahyo unatakiwa uje sehemu flani tukutane tukupe details zaidi ukimuuliza biashara gani hyo hajibu,anakwambia ww njoo tu,,sasa kwann hawasemi ukweli kuhusiana na biashara hii au wengi hawaipendi biashara hii na ndo maana hutumia mbinu hyo kukamata watu??
Wanajua wakisema hautoenda,ila ukienda bila kujua utakutana na watu wana upako wa kushawishi utaletewa watu waliofanikiwa na hiyo bizness mpaka mwenyewe utaona yes hii ndio bizness ila kati ya 100 wanaoingia anaofanikiwa ni m1 tu au hakuna kabisa.
Biashara gani unatafuta zaidi watu wa kuuza kama wewe badala ya kutafuta wateja wa kuwauzia bidhaa
aisee wengi mmeponda GNLD sasa mtupe altenative pia mana kwa wengne sie hao ni wakombozi wetu
Biashara ya kimbwa sana hii..!hivi wananufaika ..?
Sina uelewa sana na hii, lakini wenyewe wanaita network marketing, kwa maana hao watu unaowatafuta ndio itakuwa network yako ambapo itakapozidi kuongezeka na ndio pato lako litakapoongeezeka, hao watu wakati huo huo wanakuwa wateja wa bidhaa zao, kwa hiyo wewe unaona unatafuta watu kumbe ndio wateja hao,
Pamoja na watu wengi wanaibeza hii biashara lakini iko poa sana, tatizo kubwa linalofanya watu waibeze na kuona ngumu ni kama ifuatavyo
1. Watu wengi wanaoenda kujaribu hii biashara hawana asili ya biashara, kwa iyo hawana sifa km za ushawishi na nyinginezo hivyo inakuwa ngumu sana kwake.
2. Bidhaa zao zina asili moja yaani madawa tu, hii ngumu sana kwa mtu ambaye hausiani na masuala ya afya kupata soko, ndio maana utaona kuna mwingine anasema alinunua akabaki nazo akaamua kutumia mwenyewe, na mwingine akasema yy alinunua akapona gout na network yake inategemea anayemjua amepona gout ambayo ni ndogo.
3 Jinsi ya kutafuta watu/wateja(network) imekaa kimachinga (samahani kwa kutumia neno hili) au wale wa promotion zaidi, ndio hapo ugumu unaanza mtu anajiona graduate halaf leo afanye promotion! !!! haiwezekani.
Hivo ndio vikwazo ambapo watu wanaona ni kma ndoto kufanikisha.
Nimewaona jamaa wengine wapo pale sinza na wao wanafanya network narketing lakini wao bidhaa zao ni nguo, viatu, mabegi na vitu vinavyofanana na hivyo wao unaweka (deposit) elfu hamsini halaf kila unaponunua vitu vyao unapata points na unalipwa posho. kulingana na points zako.
kwa hiyo ukiamua kununua kwa ajili ya kuvaa au kuuza shauri yako.
Na hawa nao tatizo lao km wengine bidhaa zao ni ghali kama wengine.
Na kuna watu nimewaona wamekurupuka huku hawana asili ya biashara nao hao watakuja kuibeza