Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Wale waleee
 
acha dharau.....kwa wengine LAKI SITA kwa mwezi ni nyingi....wewe unapata kwa siku ndio mgawanyo wa maisha....na dharau zako hujui tofauti ya LOOSER na LOSER........
Naona na wewe ni mmoja wao wanauza hivyo viproduct fake
 
Jaribu Trevo sasa utashangaa kabisaaa yani afya ajabu, unafunguka kama Yesu ndio amekugusa tatizo ana kwa ana, ila ni virutubisho vya matunda tu

Hivi kabla ya hizi biashara watu hawakua wanaishi? Acheni wizi na kutumika banaa. Hii kitu ya kishenzi sana, honestly I hate it
 
Naona na wewe ni mmoja wao wanauza hivyo viproduct fake

Biashara ya uchuuzi haina mana kwa uchumi wa nchi.Bidhaa zao nı ghali na ni kwa sababu profit inagawanywa sana.Inaweza kuwafaa pengne wenye maduka ya dawa na vipondozi.Tunatakiwa kujifunza namna ya uzalishaji bidhaa wenyewe, hii ya kuwa madalali wa bidhaa za watu haina tija.
 
Nimekusouma kaka, next time nitajirekebisha and sinta post thread yoyote hapa JF kwa kumix Swahili and Kiingereza.

Forever living walitupa vipeperushi kuwa kuna semina ya ujasiliamali tukawaambia ni kampuni gani maana kwenye vipeperushi haijaonyesha wakasema utakuja kujua kufika waanza blah blah nyiiiingi ,mmoja akasema alikuwa anafanya kazi bot na alikuwa akipata mshahara wa mil.5kaacha kwa sasa anaingiza alot of money .katikati ndo waka display kuwa ni living firever watu km nusu tulinyenyuka tukaondooka nilikasirika sana kupotezewa muda wangu
 
Watu wa forever living jamani wanatengeneza pesa. I know some people in and out, those people make millions of money. Nao wajua mimi binafsi kwasababu wengine walikuwa my classmates chuoni wanamake kuanzia 6.5 million na kuendelea mpaka 50 millions wengine per month. Mimi nae ni member sema hiyo biashara imenishinda na niliingia kwa laki 7.5 mwaka jana. Kwahiyo I no longer do it, Nafikiri sina uwezo wa ushawishi wa kufanya watu wajoin businesses. Msiangalie watu waliofeli kama sisi, kama unataka kufanya hii busness tafuta watu ambao wamefanikiwa mbona wapo wengi tuu. Nataka kuwaambia tu wana jamii forum hamna wizi wowote unaofanyika pale, in this busness unatakiwa tuu ujitume na uwe na uwezo wa kuingiza watu kwenye hii busness, hamna ufreemason wowote kama watu wanavyosema.
 
Watanzania Wengi Wanahitaji elimu Ya Biashara...!!!
Network Marketing ni mfumo wanaotumia makampuni ya Njee kuingiza Bidhaa zao nchini..!!
Bidhaaa yenyewe Ghali; wangapi watanunua..?? Hivi kweli uchumi wa Nchi utakuwa kwa kufanya Imports ya hizi products kutoka njee....Serikali ipige marufuku tu kabisa kuingiza Bidhaa hiz;nyingi hazina viwango wala Ubora.
 
Habari zenu wana jukwaa
Kwa kipindi kifupi sana nimeona vijana wengi na ndugu zangu wengi wakiingia katika dimbwi hili LA forever network marketing
Kutokana na ushauri mwingi niliopata kuwa in WIZI, je kuna ambaye anajua wizi huu unafanyikaje?
 

JF utaipenda tuu!
 
Wadau mwenzenu nimekuwa nafuatwa na watu wa Forever Living tena kwa mialiko mithili ya kadi za harusi. Kwa muda sasa naletewa vipeperushi na baada ya kuona siitikii wito imefikia hatua wanatumwa mabinti kuniletea hiyo mialiko. Tatizo kubwa ambalo limenifanya kuwa mzito kuitikia huu wito ni Uzi uliowahi kuletwa hapa jamiiforum ambapo wachangiaji wengi walionyesha wasiwasi na hii kampuni. Juzi nililetewa na Dada mmoja kitabu cha watu mbalimbali waliojiunga Forever na kupata mafanikio makubwa hadi akili ikawa kama nimepigwa ganzi na hadi sasa huenda nikajiunga lakini kabla ya kujipeleka huko naomba ushauri kwa mara ya mwisho.
 

Attachments

  • 1432810759889.jpg
    78.7 KB · Views: 487
  • 1432810800369.jpg
    64.6 KB · Views: 458
Kajiunge mkuu,baada ya mwezi utakuwa bilionea kama Mengi,au Bahresa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…