Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

hz biashara znahitaji watu waongeaji sana na waso nakaz za kufanya
 
Nyingine inaitwa Alliance
Kuna mdada mmoja alinishawishi sana juzi kati hapa, wanajiita Alliance Global In Motion, nilikuwa namsanifu kweli kimoyo moyo jinsi alivyokuwa anajitutumua kunishawishi hadi nikamuonea huruma. Masikini aliacha kazi na kuuza laptop yake ili kujiunga,niliumia sana moyoni kwa walichomfanya mdada wa watu
 
Una taarifa zozote kuhusu hii alliance global in motion kwajinsi unavyomuhurumia uyo dada?..Maana mi nimeskia mazuri tuu japo kutoka kwa mtu mmoja tuu. Nikimuuliza changamoto hayuko tayari kusema,hawi muwazi. Ni mafanikio tuu kwake.
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Mi huwa nawachukulia kma waamin wa mashahidi was yehova wanapolazmishga kugawa vitabu vyao vya amkeni
 
Kwanini tuna toneshana madonda ya muda mrefu!!
Laki nane zangu du!!!
Kwa kifupi hii biashara kwa Africa haiwezekani! Japo nilijaribu na kupata faida ya laki moja!. Ila kumpata mtu wa kujiunga kwa bei hiyo ya laki kadhaa kwa Africa! Ngumu sana, zaid sana utaambulia lawama za watu kwa kupoteza fedha zao bila tija.
Kwa kifupi naweza sema ni kamchezo kaujanja ujuanja ambacho hakitangazwi vizuri ujue faida na hasara zake, bali utaambiwa faida zake tu.
Pili bidhaa zake bei ghali sana imewalenga walio na fedha tu, pia usabganyifu mwingi kuwa bidhaa zao hazina kemikali ?
 
Haya mambo muwe waangalifu sana......niliwahi kuingia chaka nikapoteza zaidi ya milioni tatu kwa matarajio ya kupata faida .nilijuta sana nashukuru MUNGU nilisimama upya.kuna Siku nitawaletea UZI Wa ushuhuda humu!!!
Fanya mapema huo uzi ili uwaokoe na wengine
 
Uzi umeeleweka sana maana wengi tumeshakutana na mambo hizo.Lakini kwenye kudharau kipato cha laki sita per month umewatukana walimu na manesi kibao na kuna wengine umewashangaza kbs maana hata nusu ya hiyo hela hawapati kwa mwezi.
 
HABARI ZENU WANDUGU.

kichwa tajwa chahusika,,hili swala la biashara za mitandao e.g. foleverliving n.k zimeshamili sana mjini, lakini kila mara nimekuwa nikikaribishwa na rafiki zangu waliojiunga, binafsi sijawahi kushawishika naona kuna ugumu kutengeneza chain,

kilichonisukuma kuandika huu uzi , juzi kati tena jamaa mmoja kanikaribisha pale mitaa ya posta mpya, kwenye biashara zilezile, tofauti kabisa na nilivyozoea kusikia wao wanasema kiingilio ni USD 2000(5M tsh).swali langu ni kwamba inawezekana kweli kuludisha hyo hela ukichukulia biashar hii kwa sasa kila mtu anaijua??.

ebu wataalamu nipeni uzoefu kabla sijaibiwa 5m.

asante,
Wapelekee tu mkuu usijar.. Mbwa huliwa na mbwa..
 
Naona kuna watu wengi humu wanaongea wasichokijua Ngoja nijaribu kujibu baadhi ya comments nilizoziona humu kwa kadri ya uelewa wangu.

1.Nimeona watu wanapoteza hela

Hii ni biashara kama nyingine Ni kweli kuna watu wanapoteza hela hata mimi nimeona watu wanapoteza pesa kwenye biashara ya duka, daladala, taxi n.k nimeshuhudia baa kubwa na nzuri Kinondoni na hata sinza lakini hazina wateja.

2.Ni utapeli

Kwa kampuni halali iliyosajiliwa huwa hamna utapeli. Jambo la muhimu unapofanya biashara yoyote mtandaoni chunguza kama hiyo kampuni iko regulated yaani kuwe kuna taasisi zinaisimamia. Iwe unafanya biashara ya forex, unanunua mzigo online, iwe betting n.k. kwa mfano Alliance ana Leseni ya Tanzania na nchi mbalimbali ambazo anafanya biashara, pia yuko regulated na MLMIA, Phillipines chamber of commerce, DSAP, SGS, FDA HSA na kadhalika. Epuka kampuni ambayo haiko regulated.

3.Wanajifanya wana hela

Ni kweli wako ambao wanaona ili wakushawishi kuwa hii biashara inalipa basi waigize kuwa wao wenyewe ni mambo safi. Huku ni kutojiamini sio lazima mimi niwe tajiri ndipo na wewe uamini kuwa utafaidika naweza kukuonyesha njia (na hasa pale ambapo na mimi ndio naanza) wewe ukafanikiwa na mimi nikakwama. Naweza kuwa na kitambi lakini nikakufundisha kutengeneza six packs.

3.Ni biashara ngumu

Well kama zilivyo biashara nyingine lazima uweke juhudi. Kama una mawazo kwamba hii ni pesa ya bure bure huwezi kufanikiwa na bahati mbaya baadhi ya waelimishaji wanapotosha kwa kukuambia ni rahisi tu wewe tafuta watu wawili hao wawili walete wawili na hao pia wataleta wawili basi mtandao wako utakuwa mkubwa. Nikuambie ukweli hao mamilionea wana mtandao mkubwa sana wanatumia websites, facebook insta na kila mitandao kutangaza biashara. Wanafanya semina mkoa kwa mkoa na nchi kwa nchi ili kutangaza biashara. Mimi nafamihana kwa ukaribu na mmoja kati ya members waliofanikiwa Alliance yeye akaunti yake ana watu hadi Rwanda Kenya Uganda n.k ukiwa na wanafunzi mkoani ukaandaa semina anafunga safari anakuja kuwafundisha.

4.Wananufaika waanzailishi

Hiyo naamini ina ukweli kiasi ukiwa juu una nafasi zaidi ya kukuta wanaojiunga chini wanakuwa wanakunufaisha, hata hivyo bado swala la juhudi binafsi linahusika yaani sio tu ujiunge halafu uwe dormant halafu utegemee matunda. Hii ndio imenifanya hata mimi nichague Alliance japo nilikuwa nawajua Forever GNLD Trevo n.k Alliance kwa bongo bado ni ya motomoto.

Mwisho Kwenye maisha usiangalie waliofeli angalia waliofaulu. Aliyefail hawezi kuwa role modal wako na iko wazi siku zote kuwa wanaofeli ni wengi kuliko wanaofaulu. Masikini ni wengi kuliko matajiri, wanaothubutu ni wachache kuliko wanaoogopa na kupiga porojo. Be yourself!
 
hiyo alliance inahusika na nini hasa
 
wale wa zaman zamani walikua na trainings za maana kuhusu networking marketing, afya na mambo mengine ya maana ..nakumbuka mama yangu mdogo alikua anaenda south africa mara kwa mara kwa michongo ya gnld nafikiri alikua Ruby cjui na kitu gani nilikua mdogo ila nakumbuk kulikua na shelfu limejaa folders na kanda za GNLD miaka ya 2000 kurud nyuma ...sijui waliishia wapi ingawa nakumbuka walikua na dawa moja ya kuondoa alama mf ukijikata ukipaka unapona wala alama haibaki na dawa za pumu ambazo binafsi zilinisaidia sana..ile ya madoa nilikua nikipigna nikiwekwa ngeu napaka naamka asubuh niko safi ..then ikaja hii forever living nafikiri walikua na ubi na CC Africa mama yangu mzazi aliunganishwa na mke wa Canon mmoja kutoka uingereza alipata mafunzo mengi ya misosi na ARV na mambo mengine ya ukimwi ukimwi akawa anaenda Nairobi naweza kusema hiyo ilikua ni first version ..sasa ikaja hii nyingine ya kisasa asee naona sound sana ambayo wengi ni wamatumbi wanazingua sana.
 
Aisee m siwapend ao jamaa kwanza nikioana anaanza kuniambia izo habar nataman kutapika
 
Back
Top Bottom