MNEC Joseph Peneza aozesha binti yake, ampa zawadi ya nyumba ya ghorofa, shamba na milioni 70

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kutoka Mkoa wa Mtwara, Komredi Joseph Mkuyu Peneza, ameandika historia kwa kufanikisha harusi ya binti yake, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, chama, ndugu, jamaa na marafiki, Komredi Peneza alionesha upendo wa hali ya juu kwa binti yake kwa kumpa zawadi ya nyumba ya ghorofa, shamba lenye thamani kubwa, pamoja na kiasi cha shilingi milioni 70 taslimu kama sehemu ya kumuwezesha kuanza maisha mapya ya ndoa kwa amani na ustawi.

Akiwahutubia wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo, MNEC Peneza alieleza furaha yake ya kuona binti yake anaanza safari ya maisha ya ndoa akiwa katika msingi imara wa upendo, heshima na kujitegemea. Alisisitiza kuwa familia ni nguzo muhimu ya jamii, na jukumu la mzazi ni kuhakikisha watoto wao wanaanza maisha ya ndoa kwa baraka na maandalizi mazuri.

“Tumejifunza mengi katika maisha yetu ya chama na uongozi. Leo ni siku ya furaha kwangu kama mzazi. Nataka binti yangu ajue kuwa tunampenda na tunamtakia maisha mema na mafanikio. Hii si tu zawadi, bali ni njia ya kuonesha dhamira ya dhati ya kuijenga familia yenye misingi bora,” alisema Komredi Peneza.

Wageni waalikwa walionesha kuguswa na tukio hilo la kipekee, na wengi walimpongeza Komredi Peneza kwa moyo wake wa upendo na ukarimu. Harusi hiyo imeacha gumzo jijini Dar es Salaam na kuvutia hisia chanya kutoka kwa jamii.

images (7).jpeg
 
Kashaija ukila na kipofu usimshike mkono. Hao ndio wanaoifaidi nchi hii kodi kubwa kubwa wazikwepa vizuri tu kwa mgongo wa unec. Hela zinaenda kwenye chama na sio serikalini
Sasa hapo kodi zimeliwaje?
Kuna wafanyabiashara wengi wamepewa u-NEC kutokana na michango yao minono kwenye chama.
 
Hizi emoji zingekuwepo na zinazoenesha mshangao wa..., Aisee, Doh! Ujinga, wizi! Sawa n.k huko

Zilizopo hazikidhi kwa ilipofikia dunia na watu jinsi mikasa inavyozidi kuendelea
 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kutoka Mkoa wa Mtwara, Komredi Joseph Mkuyu Peneza, ameandika historia kwa kufanikisha harusi ya binti yake, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, chama, ndugu, jamaa na marafiki, Komredi Peneza alionesha upendo wa hali ya juu kwa binti yake kwa kumpa zawadi ya nyumba ya ghorofa, shamba lenye thamani kubwa, pamoja na kiasi cha shilingi milioni 70 taslimu kama sehemu ya kumuwezesha kuanza maisha mapya ya ndoa kwa amani na ustawi.

Akiwahutubia wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo, MNEC Peneza alieleza furaha yake ya kuona binti yake anaanza safari ya maisha ya ndoa akiwa katika msingi imara wa upendo, heshima na kujitegemea. Alisisitiza kuwa familia ni nguzo muhimu ya jamii, na jukumu la mzazi ni kuhakikisha watoto wao wanaanza maisha ya ndoa kwa baraka na maandalizi mazuri.

“Tumejifunza mengi katika maisha yetu ya chama na uongozi. Leo ni siku ya furaha kwangu kama mzazi. Nataka binti yangu ajue kuwa tunampenda na tunamtakia maisha mema na mafanikio. Hii si tu zawadi, bali ni njia ya kuonesha dhamira ya dhati ya kuijenga familia yenye misingi bora,” alisema Komredi Peneza.

Wageni waalikwa walionesha kuguswa na tukio hilo la kipekee, na wengi walimpongeza Komredi Peneza kwa moyo wake wa upendo na ukarimu. Harusi hiyo imeacha gumzo jijini Dar es Salaam na kuvutia hisia chanya kutoka kwa jamii.

View attachment 3347392
Kama ni mtoto alielewa vyema na kumtanguliza Mungu atafanikiwa sana,kila la kheri kwa wanandoa Hawa!
 
Hata wewe unao uwezo wa kukwepa kodi tena kisheria, ndio maana kuna tax avoidance & tax evasion. Operate kazi zako kupitia NGO au kampuni.
Hawa watu wanajua mianya ya kukwepea.
Kashaija ukila na kipofu usimshike mkono. Hao ndio wanaoifaidi nchi hii kodi kubwa kubwa wazikwepa vizuri tu kwa mgongo wa unec. Hela zinaenda kwenye chama na sio serikalini
 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kutoka Mkoa wa Mtwara, Komredi Joseph Mkuyu Peneza, ameandika historia kwa kufanikisha harusi ya binti yake, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, chama, ndugu, jamaa na marafiki, Komredi Peneza alionesha upendo wa hali ya juu kwa binti yake kwa kumpa zawadi ya nyumba ya ghorofa, shamba lenye thamani kubwa, pamoja na kiasi cha shilingi milioni 70 taslimu kama sehemu ya kumuwezesha kuanza maisha mapya ya ndoa kwa amani na ustawi.

Akiwahutubia wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo, MNEC Peneza alieleza furaha yake ya kuona binti yake anaanza safari ya maisha ya ndoa akiwa katika msingi imara wa upendo, heshima na kujitegemea. Alisisitiza kuwa familia ni nguzo muhimu ya jamii, na jukumu la mzazi ni kuhakikisha watoto wao wanaanza maisha ya ndoa kwa baraka na maandalizi mazuri.

“Tumejifunza mengi katika maisha yetu ya chama na uongozi. Leo ni siku ya furaha kwangu kama mzazi. Nataka binti yangu ajue kuwa tunampenda na tunamtakia maisha mema na mafanikio. Hii si tu zawadi, bali ni njia ya kuonesha dhamira ya dhati ya kuijenga familia yenye misingi bora,” alisema Komredi Peneza.

Wageni waalikwa walionesha kuguswa na tukio hilo la kipekee, na wengi walimpongeza Komredi Peneza kwa moyo wake wa upendo na ukarimu. Harusi hiyo imeacha gumzo jijini Dar es Salaam na kuvutia hisia chanya kutoka kwa jamii.

View attachment 3347392
Ukitishia anga zao kwanini wasikuue, ni matajiri kuliko wafanyabiashara.
 
Back
Top Bottom