MNEC Joseph Peneza aozesha binti yake, ampa zawadi ya nyumba ya ghorofa, shamba na milioni 70

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kutoka Mkoa wa Mtwara, Komredi Joseph Mkuyu Peneza, ameandika historia kwa kufanikisha harusi ya binti yake, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, chama, ndugu, jamaa na marafiki, Komredi Peneza alionesha upendo wa hali ya juu kwa binti yake kwa kumpa zawadi ya nyumba ya ghorofa, shamba lenye thamani kubwa, pamoja na kiasi cha shilingi milioni 70 taslimu kama sehemu ya kumuwezesha kuanza maisha mapya ya ndoa kwa amani na ustawi.

Akiwahutubia wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo, MNEC Peneza alieleza furaha yake ya kuona binti yake anaanza safari ya maisha ya ndoa akiwa katika msingi imara wa upendo, heshima na kujitegemea. Alisisitiza kuwa familia ni nguzo muhimu ya jamii, na jukumu la mzazi ni kuhakikisha watoto wao wanaanza maisha ya ndoa kwa baraka na maandalizi mazuri.

“Tumejifunza mengi katika maisha yetu ya chama na uongozi. Leo ni siku ya furaha kwangu kama mzazi. Nataka binti yangu ajue kuwa tunampenda na tunamtakia maisha mema na mafanikio. Hii si tu zawadi, bali ni njia ya kuonesha dhamira ya dhati ya kuijenga familia yenye misingi bora,” alisema Komredi Peneza.

Wageni waalikwa walionesha kuguswa na tukio hilo la kipekee, na wengi walimpongeza Komredi Peneza kwa moyo wake wa upendo na ukarimu. Harusi hiyo imeacha gumzo jijini Dar es Salaam na kuvutia hisia chanya kutoka kwa jamii.

View attachment 3347392
Eti ujasiriamali kwa ajili ya familia ya bi harusi na watoto wake! Hivi sio kwamba watoto wao, yaani wa bi harusi na bwana harusi?
Bwana harusi ametoa mahari kiasi gani?! Au kapewa tu mke?
 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kutoka Mkoa wa Mtwara, Komredi Joseph Mkuyu Peneza, ameandika historia kwa kufanikisha harusi ya binti yake, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, chama, ndugu, jamaa na marafiki, Komredi Peneza alionesha upendo wa hali ya juu kwa binti yake kwa kumpa zawadi ya nyumba ya ghorofa, shamba lenye thamani kubwa, pamoja na kiasi cha shilingi milioni 70 taslimu kama sehemu ya kumuwezesha kuanza maisha mapya ya ndoa kwa amani na ustawi.

Akiwahutubia wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo, MNEC Peneza alieleza furaha yake ya kuona binti yake anaanza safari ya maisha ya ndoa akiwa katika msingi imara wa upendo, heshima na kujitegemea. Alisisitiza kuwa familia ni nguzo muhimu ya jamii, na jukumu la mzazi ni kuhakikisha watoto wao wanaanza maisha ya ndoa kwa baraka na maandalizi mazuri.

“Tumejifunza mengi katika maisha yetu ya chama na uongozi. Leo ni siku ya furaha kwangu kama mzazi. Nataka binti yangu ajue kuwa tunampenda na tunamtakia maisha mema na mafanikio. Hii si tu zawadi, bali ni njia ya kuonesha dhamira ya dhati ya kuijenga familia yenye misingi bora,” alisema Komredi Peneza.

Wageni waalikwa walionesha kuguswa na tukio hilo la kipekee, na wengi walimpongeza Komredi Peneza kwa moyo wake wa upendo na ukarimu. Harusi hiyo imeacha gumzo jijini Dar es Salaam na kuvutia hisia chanya kutoka kwa jamii.

View attachment 3347392
Kama unajua mila zao, huwezi kushangaa maana mwanaume ukioa unahamia kwao na mkeo. Je, utalala nyumbani kwa mama mkwe wako? Mwanaume kuoa wanaita unatumiaka. Angalia hata hapo anayeongea ni mama na baba ameufyata
 
Hiyo familia haina Binti mwingine nimpeleke first born wangu akaoe 😜

Vijana changamkieni Ndoa, ukipata Binti kwao anajiweza kama hiyo familia tangaza Ndoa faster

Sisi Wazee wao hatuchelewi kuwapa viwanja/nyumba/fedha kama zawadi Siku ya harusi yenu 🤗
 
Watanzania tuache wivu! Huyo mwamba kama ni mfanyabiashara kamdhulumu nani? Tumekariri lila mwenye hela ni mwizi? Kama alikuwa TRA ni sawa tu maana nchi la kugawana hili. Ila mwoaji sasa naye akaache ujinga wa michepuko!
 
Back
Top Bottom