Pre GE2025 Mngependa nani awe Kampeni Meneja wa Rais Samia hapo mwakani?

Pre GE2025 Mngependa nani awe Kampeni Meneja wa Rais Samia hapo mwakani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ni Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan mpaka 2030.Hapo ndio tutaweka kituo kuangalia sasa tunafanyaje.
Sijui wewe una mawasiliano ya moja kwa moja na Mungu au sijui wewe ni nabii maanake hata dikteta Magufuli naye chawa wake walikuwa wakitamba hivyo hivyo.
 
Naipenda sana CCM na Rais wangu na serikali yetu pamoja na Taifa letu.ndio maana nafanya kazi usiku na mchana kuyasema mazuri na makubwa yaliyofanywa na Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan, Mama Mwenye Moyo wa Upendo, unyenyekevu, uzalendo na huruma kwa watanzania.
Ukienda huko vijijini kuna watu wanaishi maisha ya dhiki kwelikweli lkn unakuta mzazi ana watoto 7 hata nguo za kuvaa hawana lkn mwambie huyo mtoto au mzazi naomba nichukue mtoto wako mmoja nikwamwendeleze kwa faida yake au na wewe mwenyewe hapo baadae, wale watoto watakwambia siwezi kumwacha mama au baba, uniache hapahapa.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa kuwa Mwakani ni uchaguzi Mkuu wa udiwani ,ubunge na Urais. Na kwa kuwa Fomu ni moja tu ya Urais ndani ya CCM kwa ajili na maalumu kwa Mama yetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,na kwa kuwa ndio chaguo la mamilioni ya watanzania kutokana na makubwa aliyoyafanya ndani ya muda mfupi wa uongozi wake na kugusa maisha ya mamilioni ya watanzania.

Niilikuwa nauliza katika kukamilisha ratiba na kutimiza wajibu tu mngependa Nani awe Kampeni Meneja wa Mama yetu Mpendwa? Nasema kukamilisha ratiba na kutimiza wajibu kwa sababu mpaka sasa Rais Samia ndiye kiongozi anayependwa na kukubalika kuliko mtu Mwingine yeyote yule,ni kiongozi ambaye tayari ameshashinda katika mioyo ya watanzania,ni kiongozi ambaye hana wa kumzuia ,wala hakuna mtu mwenye ubavu wala uwezo wala nguvu wala ushawishi wa kuweza kushindana na Rais Samia katika sanduku la kura na mahali pengine popote pale.

Kwangu mimi nilikuwa napendekeza mtu huyo awe ni mtu mwenye kujiamini,mwenye uwezo na pumzi kubwa ya kuweza kuzungumza jukwaani bila kuchoka lakini Mwenye kuzungumza kwa umakini,hoja na mtiririko mzuri.awe ni mtu anayefahamu vyema sana na kwa undani nini chama kiliahidi katika uchaguzi uliopita,nini kimetekeleza na kwa kiwago gani.

Mtu huyu awe na uwezo na umahiri mzuri katika lugha na kuitumia katika namna itakayovuta na kuteka hisia za watu hadi kuwabubujisha machozi ya furaha makundi yote.,awe na uwezo wa kutetea hoja na kuifafanua katika namna ambayo mwananchi wa kawaida hata asiye na Elimu ataelewa vyema sana.awe na uwezo wa kuzungumza kwa utaratibu na kwa sauti yenye kuteka hisia za watu.awe na uwezo wa kuyasoma mazingira kwa uharaka na kubadilika kwa uharaka na kujuwa namna gani ya kupata usikivu wa watu.

Awe na uwezo na ufahamu na maarifa ya kuwaeleza watu ni wapi tumetoka ,wapi tupo na wapi chama kingependa tuelekee na mafanikio ambayo tumeyapata Kama Taifa. Awe ni mtu mwenye ufahamu na uelewa wa masuala mbalimbali. Ajuwe namna ya kucheza na hadhira na kuiteka na ajuwe namna ya kuanza na kumaliza hotuba yake katika namna ya kuvutia.. awe mtu anayeweza kuzungumza katika namna itakayohakikisha hakuna kundi linaachwa nyuma au kutokuguswa kisera.

Lakini pia ni lazima mtu huyo awe muadilifu,mchapa kazi ,asiye na madoa au taswira mbaya kwa watu na jamii kwa ujumla,yeye binafsi awe anakubalika na mwenye uwezo wa kumnadi mgombea wetu kwa uhodari na umahiri wa hali ya juu sana.ikiwa ni pamoja na kubadilika kulingana na mazingira na mahitaji ya eneo au kanda husika .mfano mahitaji ya wakulima wa nyanda za juu kusini ni tofauti na mahitaji ya watu wanaoishi Dar.mfano ukija nyanda za juu kusini wapiga kura watahitaji kusikia habari za pembejeo hususani mbolea,bei ya mazao yao, miundombinu hususani barabara,huduma za kijamii kama vile afya,elimu,maji,n.k.

wakati watu wa Dar masuala ya pembejeo kama vile mbolea siyo kipaombele na hitaji lao la msingi na Muhimu au kero yao.wao watahitaji kusikia habari za upatikanaji wa maji safi na salama, barabara nzuri,usafiri mzuri na kupunguza foleni na nauli jijini kupitia barabara na magari ya mwendo kasi,ajira kwa vijana ,mazingira mazuri kwa wafanya biashara,mikopo kwa vijana,akina mama na watu wenye ulemavu.huduma bora za afya n.k.View attachment 3047760

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Genius mmoja tu, Kinana
 
Mkuu hivi huwa mnalipwa sh ngapi vyuma vimekaza ,nataka mfuata Msigwa tafadhali
Kazi ni kipimo cha utu.ukitaka pesa fanya kazi kwa bidii , juhudi na maarifa na jishughulishe sana upatapo kazi.mimi silipwi kuwepo hapa jukwaani.
 
Anatakiwa mtu mwenye uwezo wa kububujikwa na machozi ikionekana watu wanataka kumkataa Mama Samia.

Mtu mwenye uwezo huo, si mwingine bali mwanafyale LUCAS MWASHAMBWA.

Tena itakuwa vizuri sasa hivi ungemfuata 'jemedari wa vita', huku ukibubujikwa na machozi, na kumweleza kuwa kuwa unataka uwe meneja mkuu wa kampeni yake, na umjulishe kuwa una machozi mengi na ya kutosha kulia siku zote za kampeni.

Ukifanikiwa kuipata hiyo nafasi, mwisho wa kampeni, unaweza hata kuacha uchawa, ukarudia kwenye utu wako kama binadamu timamu, maana utakuwa na uhakika wa kula, utajenga japo nyumba ya kawaida, na utaweza kununua angalao RAV4.
 
Back
Top Bottom