Pre GE2025 Mngependa nani awe Kampeni Meneja wa Rais Samia hapo mwakani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ni Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan mpaka 2030.Hapo ndio tutaweka kituo kuangalia sasa tunafanyaje.
Sijui wewe una mawasiliano ya moja kwa moja na Mungu au sijui wewe ni nabii maanake hata dikteta Magufuli naye chawa wake walikuwa wakitamba hivyo hivyo.
 
Ukienda huko vijijini kuna watu wanaishi maisha ya dhiki kwelikweli lkn unakuta mzazi ana watoto 7 hata nguo za kuvaa hawana lkn mwambie huyo mtoto au mzazi naomba nichukue mtoto wako mmoja nikwamwendeleze kwa faida yake au na wewe mwenyewe hapo baadae, wale watoto watakwambia siwezi kumwacha mama au baba, uniache hapahapa.
 
Genius mmoja tu, Kinana
 
Mkuu hivi huwa mnalipwa sh ngapi vyuma vimekaza ,nataka mfuata Msigwa tafadhali
Kazi ni kipimo cha utu.ukitaka pesa fanya kazi kwa bidii , juhudi na maarifa na jishughulishe sana upatapo kazi.mimi silipwi kuwepo hapa jukwaani.
 
Anatakiwa mtu mwenye uwezo wa kububujikwa na machozi ikionekana watu wanataka kumkataa Mama Samia.

Mtu mwenye uwezo huo, si mwingine bali mwanafyale LUCAS MWASHAMBWA.

Tena itakuwa vizuri sasa hivi ungemfuata 'jemedari wa vita', huku ukibubujikwa na machozi, na kumweleza kuwa kuwa unataka uwe meneja mkuu wa kampeni yake, na umjulishe kuwa una machozi mengi na ya kutosha kulia siku zote za kampeni.

Ukifanikiwa kuipata hiyo nafasi, mwisho wa kampeni, unaweza hata kuacha uchawa, ukarudia kwenye utu wako kama binadamu timamu, maana utakuwa na uhakika wa kula, utajenga japo nyumba ya kawaida, na utaweza kununua angalao RAV4.
 
Huko kwa wakulima ndio machawa wamejaa.
Hakuna chawa mkulima.maana mkulima anakula kwa jasho lake mwenyewe na hivyo hahitaji fadhila ya kulishwa.ndio maana wakulima kama mimi ni wasema kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…