Mngeta, Mlimba: Wananchi walioshindwa kununua mita za maji kutozwa 10,000 kwa mwezi kuanzia Julai, 2021

Mngeta, Mlimba: Wananchi walioshindwa kununua mita za maji kutozwa 10,000 kwa mwezi kuanzia Julai, 2021

lukoma

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2013
Posts
2,995
Reaction score
2,246
Kumekuwa na ukandamizaji, unyanyasaji na upigaji mkubwa sana wa pesa katika kata za mchombe na Mngeta kupitia mradi wa maji Lukicha! Pesa ya mfadhili pamoja na 10m alotoa Mh. Lwakate -marehemu imetumika kujenga katangi kadogo hata 5m hazifiki!

Mbali ya upigaji huu mkubwa wa ujenzi wa tangi la maji, wameanza upigaji mpya kupitia gharama za maji kwa mwezi. Kuanzia mwezi July, 2021 wananchi ambao wameshindwa kununua mita wametakiwa kulipa 10,000/= kutoka 5,000/= kwa mwezi gharama za awali ambazo hata hivyo wananchi hawakuwatayari kulipa kutokana na sababu zifuatazo:

Kabla ya upanuzi na uboreshaji mradi kupitia mfadhili, mradi huo ulikuwa chini ya wa wananchi, kupitia michango yao ndiyo waliohusika kujenga tangi, kuchimba mitalo na kutandika mabomba. Mpaka hivi sasa bado tatizo likijitokeza wananchi hulazimishwa kujitolea lakini cha kushangaza wakati wa kujadili gharama za maji kamamlaka kadogo kanachoitwa Lukicha ambacho kamepora mradi kutoka kwa wananchi hawawashirikishi wananchi wenye mradi wao.

Gharama ndogo ya uendeshaji, maji yametegwa katika mto Mchombe ambapo yanaporomoka yenyewe bila kutumia umeme. Tangi la maji halitibiwi kwa dawa hivyo hayako salama. Maji yanayotoka ni machafu hata kipindi ambacho sio cha mvua, kuna siku au wakati maji yanatoka machafu yanayoambatana na takataka kama majani na vipande vya miti na wadudu kama earth worms kwa sababu sehemu waliyotega maji hakuna hata chujio. Hivyo, hakuna haja ya kuwa na gharama kubwa kwani maji haya ni sawa tu na yanayotiririka mtoni.

Elimu finyu ya mita kwa wananchi, hakujawahitolewa elimu/uhamasishaji wa kutosha juu ya umuhimu na matumizi ya mita kwa wananchi zaidi ya ufafanuzi/maagizo yanayotolewa na viongozi wa kijiji wakati wa mikutano ya vijiji ambayo hulenga utekelezaji zaidi kulikokutoa elimu. Hii hupelekea wananchi kuona kama mita za maji ni mzigo kwao kuliko faida.

Ubovu wa mita na hakuna uhakika wa upatikanaji, wananchi wachache waliowekewa mita za majaribio imeleta hofu kwa wananchi kwani kwa matumizi ya kawaida tu gharama ilifika mpaka 60,000/= kwa mwezi. Wao (Mamlaka) wenyewe walikiri kuwa mita zilikuwa mbovu lakini cha ajabu wameanza tena kuwalazimisha wananchi kuunua mita bila kuwatoa hofu kama mita kwa sasa ni nzuri. Liko duka moja tu ambao mita hizi hupatikana, hii hupelekea gharama kuwa kubwa na hata kama mbovu hakuna mbadala wake.

Bodi na mamlaka hawana mikakati yeyote ya uboreshaji wa maji zaidi ya kutafuna tu hela inayopatikana. Pia hawana ubunifu wowote wa kuendeleza mradi, kifupi bodi na mamlaka ya maji ni wadumavu.

Kuongeza gharama badala ya kufunga mabomba. Adhabu inayotolewa kwa mwananchi anaeshindwa au anayekataa kuweka mita kimatiki haikubaliki. Kama mwananchi ameshindwa kununua mita ni bora wakafunga bomba kuliko kuongeza gharama kwa mwezi kwani mwananchi atashindwa kulipa na gharama/deni litaongezeka wakati hana uwezo.

Uamuzi wa wananchi, baadhi ya wananchi wameamua kuacha kutumia maji ya mabomba na kutumia maji mbadala ya visima na mto waliyokuwa wanatumia awali kabla ya maji ya mabomba kupatikana.

Wito kwa mamlaka za juu husika, waziri wa maji, TAKUKURU, mkuu wa mkoa na waandishi wa habari kufika Mngeta kufuatilia kwa karibu unyanyasaji wa wananchi na upigaji wa pesa huu.
 
Back
Top Bottom