Mkuu wewe unaweza kufanya jambo hili?
Mimi naweza.
Sioni kama ni sahihi kumlaumu Sonofobia kwa hali ilipofikia.
Mimi nimeshauri sijalaumu mkuu,na ushauri ni mawazo ambayo una hiyari uyachukue ama uyawache.
Unamlaumu ilihali hujui hali yake yake ya uchumi?
Kwa nini aje kuomba ushauri kwa watu ambao hawajui hali yake ya kiuchumi,asingekuja hapa kuomba ushauri kwa sabau hakuna anayejua hali yake ya kiuchumi hapa kinyume na alivyoelezea yeye.
Nani anagharamia masomo yake?
Yeye ndo anajua nani anagharamia masomo yake,sisi kazi yetu ni kumshauri kwa mujibu wa alivyojipambanua.
Hali ya familia yake ipoje?
Yeye ndio anajua,sio mimi wala wewe mkuu.
aache familia ikiwa inakufa njaa,
Wewe ndio unasema kuhusu kufa njaa,UNAJUA KUFA NJAA WEWE ?
mimi nimesema kulala njaa,usinilishe maneno mkuu,unaweza kulala njaa na bado ukawa mzima kesho yake.
Au unadhani hapa tanzania hakuna familia zinalala njaa na wazazi wao wakiwa wapo hapo nyumbani ?
Kuna wakati tujaribu kuwa na staha kwenye mambo ya msingi.
Wewe Ndio unakosa staha kwa kunishambulia maoni ambayo nimetoa huku ukitambua fika kwamba hatufanani mawazo,sijui ulitaka wote tutoe wazo moja ?
Bado ushauri nilioutoa siutengui maadamu tu kutoa ushauri ni uhuru wangu na ushauri huo sikuutoa kwa kukurupuka,nimetoa nikiwa na akili timamu kabisa.
hapa sio kumwambia mwenzio aache familia inakufa njaa.
Wewe ndio nakusikia ukisema kuhusu familia kufa njaa mkuu,binafsi sijawahi kutamka hayo maneno.
My take ; asipuuzie hiyo fursa ahakikishe anaitumia vyema kama anaamini kwambahuko anakoenda fursa zitafunguka.
Period.