Mnyama Mkubwa Zaidi Aliyewahi Kuishi Duniani aligundulika Tanzania mkoa wa Lindi

Mnyama Mkubwa Zaidi Aliyewahi Kuishi Duniani aligundulika Tanzania mkoa wa Lindi

Kumshafirisha sio tatizo....Ila kumtunza ndio gharama na serikali hii hawezi mudu hizo gharama
Nimecheka sana, yani ghrama ya kumtunza ni ipi?, chakula, fuel or...........
 
Actually hata mji wa kale zaidi umegunduliwa pwani ya kilwa, bado tupotupo tu
 
Maskini mnyama wetu........
Hebu wamlete bana.........tutampenda zaidi......
 
Hii mada yako haiwezi kupata comment sababu watanzania walio kweny social media maada zenye tija hawazitaki , wewe lita udaku wowote utaona page zinavyo kwenda (poor tanzanian )kisha tuna taka maendeleo mmmm hatar

Wewe ni Mkenya...

hahahahahaha, umesema ukweli jameee, hapa hutaona watu kuchangia

Wewe ni Mganda...

Watachangia kwa sababu ya msumari wa jameee, otherwise ni ukweli.

Wewe ni Mrundi...

Stupid fellas!!!!!
 
Najivunia kuwa Mtanzania ukifuatilia science kwa ukaribu utajua Tanzania ni chimbuko la viumbe vingi ikiwemo binadamu wa kwanza.

Tumebahatika sana kuzaliwa Tanzania we should be proud of this.

Yah, sisi wote ni Warangi. Obama, Blair, Malkia, Donald Trump, Mwana Mtoka Pabaya, wooote warangi
 
Shule sio baharini sema niende baharini mkuu

Shule ndo muhimu sababu huko ndo utajua viumbe tofauti wanaoishi baharini, ukiende baharini kabla ya shule unaweza ukakuta watu wanaogelea ukasema nao ni samaki.
 
Pale kalenga kwenye fuvu la mkwawa yule ndugu analalamika na kudai bora waliondoe wakazike lile fuvu la mkwawa sababu hawa jui faida yake.
Mnafikiri hilo dudu likija tanzani tutanufaika zaidi ya kujaa mavumbi vumbi tu.
Nashauri libaki kule, tuongee nao %ya mapato ije Tanzania.
Ila sisi tujikite kwenyeutafitu tupate ndugu zake hawezi kuwa aliku wapeke ake huyu
 
Habari za Jumapili Wakuu,

Kuna makala moja ya kisayansi nilikua naipitia leo na nikashangazwa kugundua kwamba mnyama mkubwa zaidi aliyewahi kuishi duniani anaitwa Giraffatitan.

Huyu mnyama aliishi jurrasic era takribani miaka milioni 150 iliyopita na inasemekana uzito wake ulikua unafika tonne 80 na urefu wake zaidi ya metre 20.

Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba huyu mnyama mabaki yake ikijumuisha fuvu lake yaligundulika Lindi, Tanzania kipindi cha utawala wa kikoloni wa wajerumani hapo mwaka 1909 na 1912.

Mabaki yake sasa yametundikwa Berlin, Ujerumani na yamekua ni kivutio kikubwa cha utalii nchini kule.

Kwanini sasa serikali na wizara inayohusika na utalii wasianzishe kampeni na mijadala ya mabaki ya mnyama huyu kurudishwa Tanzania kwasababu alichukuliwa kwa njia ambayo siyo halali.

India na nchi nyingine wameweza kupigania mali nyingi zilizoibwa kipindi cha ukoloni zirudishwe na zimerudishwa kwanini sasa Tanzania tusiige mfano.

Tanzania ikumbukwe ndo craddle of all civilization, binadamu wa kwanza wameishi hapa miaka milioni iliyopita na wanyama wenye super genes kama. huyu wameishi hapa pia. Ombi langu serikali ifanye jitihadi kurudisha mabaki ya huyu mnyama na wengine wengi. Itakuza utalii wa ndani na kurudisha sense of National Pride ya kujivunia kuwa Mtanzania.

Picha zake hizi hapaView attachment 349837
Tanzania sijui nani alituloga
 
ninachojua ni kwamba kuna asilimia Fulani za mapato ya utalii kutoka Ujerumani yanakuja Tanzania
 
Asanteni Jamiiforums kwa kuuweka huu uzi nilioanzisha kwenye page yenu ya Facebook ni dhahiri utawafikia watanzania wengi na kuwaamsha kutoka usingizini kupigania urithi waliopokonywa isivyo halali na wajerumani.

Kama vipi tuanzishe kampeni SocialMedia yenye hashtag ya bringourgiraffatitanback# au bringourmjusiback# ili ku'raise awareness zaidi.

Ni lazima Mjusi wetu arudishwe awekwe Makumbusho ya Taifa watoto wetu wajivunie kuzaliwa Tanzania.
1464878702181.jpg
 
Kulileta sio tatizo kwani wao si walichukua mifupa wakaenda kuliunganishia huko so mnalifungua na kutia sandukuni linakuja tatizo hiyo mifupa kuitunza isiharibike upesi ndo mtihani.
Kuna jamaa yangu dereva Kuna siku alipita mitaa ya lindi porini basi akakatiza kiumbe ambae alisema hafanani na kenge wala mamba na wanakijiji husema kiumbe hicho hupita nyakati fulani cha mwaka na wakafananisha na mizimu.
Sihitimishi kwa kusema ni dainorsour bali nadhani misitu kama hiyo ina mambo mengi ambayo hayajajulikana bado.
 
Bora abaki tu huko akirudi bongo ndani ya mwezi tu atakua kachoka mbaya kama sio kupotea kabisa. Utunzaji sio sifa yetu.
 
Back
Top Bottom