Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Aliondoka Slaa, aliondoka Zito,
Fukuza wote hao wakakate mauno yao huko...
 
Waambieni upuuzi wanaofanya umechosha,watumishi wanahitaji stahiki zao.Na si fedha zitumike kuwanunua wakina Mdee.
 
Analysis on point
 
Wanandungai 19 leo wanaizika chadema rasmi toka chama kikuu cha upinzani na kuwa chama cha mwisho kabsa cha upinzani endapo kamati kuu ya chadema itakuwa Dhaifu mno kuwakumbatia hao walionyesha dharau kubwa kwa Uongozi wa chadema
 
aliondoka Slaa, aliondoka Zito,
Fukuza wote hao wakakate mauno yao huko...
Tatizo kubwa mbowe na Salum mwalimu wamekula bilion 3 za CCM huku pia wakiwinda ruzuku haramu kupitia hao wabunge 19 wa Ndungai, hapo ndipo penye shida kubwa na pia hao wanandungai wameonyesha dharau kubwa kwa Lisu na mnyika kisa wamepewa vicent na Ndungai na kuahidiwa mgao na mbowe mwenyewe, kuna mkanganyiko mkubwa sasa, mbowe kapagawa yupo mafichoni kaenda kuficha pesa aliyochukua toka CCM kwanza, leo kuba mawili chadema idharaulike au iheshimike zaidi
 
Ni kauli iliyoshiba na yenye mantiki.Ambaye haoni ubatili na uhuni uliofanyika na unaoendelea kufanywa ni kwa utashi wake wa kukana ukweli! Dola iko mikononi mwa "WAHUNI".
 
Kwa akili zako CHADEMA ina survive sababu ya ruzuku pekee? More so ruzuku watakayopewa haitozidi 100M kwa mwezi which is peanuts ukizingatia walikua wakipata zaidi ya 2B kwa mwaka. Kwahiyo hta wakiikubali bado haiwezi wasaidia kitu.

Hyo 100M u can simply get from donors na raia kwa mfumo wa michango/kulipia kadi kupitia CHADEMA digital. Na wananchi tutachanga maana tunajua wamekataa hela ya dhulma and itaonyesha seriousness ya chama kuelekea 2025.

Then sio kweli Mbowe kawatuma otherwise asingehitaji kutumia njia za panya. Si mnamuitaga dikteta? Sasa amuogope Mnyika aliyemteua mwenyewe? Amgeitisha press. Angejustify maamuzi kazi kwisha. Ila kudai Mbowe anategemea njia za panya kupitisha maazimio yake ni reasoning ya chini kabisa.

Kma CHADEMA ilivuka kifo cha wangwe,Kesi ya ugaidi wa Lwakatare, kuondoka Zitto na Dk Slaa. Trust me hakuna lingine linaloweza warudisha nyuma ever. Na nchi hii hakuna upinzani nje ya CHADEMA and its more clearer now than ever.
 
Nakubaliana na wewe ila unasahau nguvu ya chama ni wanachama. Sijui unajua athari za kuwafukuza viongozi wa BAWACHA uanachama? Je, chama kitabaki salama kweli?
 
Nakubaliana na wewe ila unasahau nguvu ya chama ni wanachama. Sijui unajua athari za kuwafukuza viongozi wa BAWACHA uanachama? Je, chama kitabaki salama kweli?
BAVICHA ilikua ndio nguzo ya CHADEMA enzi za Heche ila walitimuliwa karibu viongozi wote 8 kuanzia Mchange mpaka mwampambana na Shonza. Na tokea hapo vijana waliongezeka mara dufu leo hii kina mchange wameishia wapi?

Slaa na Zitto walikua na zaidi ya 2m followers wa upinzani. Walivyosepa kuna impact yeyote? As long as CHADEMA ni brand watakuja replacements wengi mnoo.

Kuna kina Khadija Mwago, Aisha Madogga, Mama wa chato, Upendo peneza, Moza ally, Amina Saguti, Esther Chisanga, Lucy Owenya, Asia Msangi, Dorcas Francis, Komba, to name a few...... Hao wana replace roster nzima iliyosaliti bila gap yoyote kuonekana.

With time watsahulika tu kma kina Lijualikali na Lwakatare
 
Ikiwa documents zimeghushiwa kwanini wasiende mahakamani ili kupinga uhalali WA kilichotokea?
 
wasipoondolewa uanachama hao warembo
Wanachadema ambao hamukubaliani nao mjiunge chama cha UBWABA
 
Wenawe Mnyika unajisaulisha kipindi kile unaruka ukuta shulee ya loyola ili upate kula si kura leo Halima karuka ukuta bungeni ili nao wapate kula unabweka nini shida nilikuwa simpendi halima Mdee ila kuanzia sasa ni heko kwake hayaaa Huyo Lissu yupo huko Ulaya anakula pancake na nawazungu Mbowe najichana ruzuku tena hili la kuapa wakina Mdee anafaida zake ruzuku nakuchangia kiasi kidogo wabunge ni palepale Wewe mnyika unapakuamkia Asubuhi officini hata kama hakuna cha maana ila upo hapo haya Wakina Mdee wakalee wapi wakaandamane na wasaulike ipo siku utakuja Mshukuru mdeee kacheza karata tatu hata mkizira siewenzenu wala Yaheeh mlizira Corona what Next!!@ Chezea Halima wewe!!

WAMAMAkama wote wameenda kutafuta pesa za maziwa ya Watoto kopo Ya kifuani siku hizi wananyonyo wakubwa Nenda halima wakiwazingua hameni chama tafuteni kichama kidogo kikuzeni kama zzitto
 
Kama ni mfumo
..hao Makamanda ealilishea nini?
Hadi sasa hakuna update ya kikao sio kuhusu Halima ama Mbowe aliyrtajwa na Halima. [emoji23][emoji23]
 
Kwa hili pia nakubaliana na wewe, japo hutaki kusema wazi, wakati unajua kuwa nyuma ya migogoro yote ndani ya chama ni Mbowe. Hata hao uliowataja kuchukua nafasi ya Halima na wenzake (uteuzi wao una baraka ya Mbowe), hawana ubavu wa kumshauri Mbowe hata akifanya vibaya
 
Hpn Mbowe si ni dikteta kma mnavyodai kma alibadili gia kwa Lowassa among all people ashindwe kwa hili la mabinti wachache?
Angeitisha press angedai wanawatuma wadada 19 kupambana katiba mpya ipatikane. Nani angepinga?

Ila Mbowe eti amuogope Mnyika ni ujinga kuamini hilo. Angetaka apeleke viti maalum angempa ultimatum tu majina yapelekwe haikua na haja atumie njia za kihuni hivi.

So ntakua mtu wa mwisho kuamini Mbowe ni coward kiasi hiko
 
Kitendo cha wale wabunge kwenda bungeni na kuapa mbele ya spika maana yake walikuwa na baraka za mkuu kabisa ndani ya chama.

Wale sio watoto wadogo wafanye jambo kubwa kama lile pasipo kuwa na baraka za ndani ya chama.
 
Wakili msomi haya maswali ni mepesi sana ktk mfumo wa nchi yetu,kuna mambo hufanyika na huwezi hata kuwaza kama yanaweza fanyika ,ngoja tuendelee na ngonjera nyingne mana ni mwendo wa bandika bandua tu
Maswali yafuatayo yanapaswa kujibiwa na Mbowe/ Mnyika:

1. Nani amepeleka Orodha ya Majina ya Wabunge wa Viti Maalum NEC?
2. Orodha hiyo imepelekwa kwa njia gani?...
 
Ameandika hivi kupitia Twitter:

Impunity ya kiwango cha juu kabisa katika taifa letu . Hivi inavumilikaje mtu kuwa mahabusu hajafuata taratibu anatolewa gerezani usiku ,anaapishwa gereji,anakuwa mbunge, halafu waliotenda haya bado wapo ofisi za umaa , halafu yeye na spika wanaitwa waheshimiwa 🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…