Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Karim Mandonga ndio "Mike Tyson" wa ngumi za Tanzania kwa sasa

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Karim Mandonga ndio "Mike Tyson" wa ngumi za Tanzania kwa sasa

Muda bado, lakini ndo bondia kipenzi cha wengi kwa sasa Tz, anatisha kwa tambo na maneno ya kuogofya mpinzani.
Leo huko Songea alikuwa na mashabiki kibao, yaani kuna shabiki kampa ofa ya kutembelea Jeep huku akiongea na mashabiki wake akiwa juu mithili ya Magufuli akiongea na umati wa wananchi.

Mandongo inatakiwa leo apigwe tena, hii itasaidia kuongeza brand yake kuliko akishinda pambano lake usiku huu.
Kapigwa tena mtu wenu
 
50 cents aliwahi kusema mwaka 2003 na mnukuu " in hood they say there is no business like ho business but on hollywood they say there is no business like show business"

P.I.M.P _ 50 cent Feat Snoop Dog Dogy.
 
Mimi ni shabiki kindaki ndaki wa huyo jamaa ila leo kaniangusha sana.bora ata lile pambano la morogoro alilopigwa ngumi jiwe moja akakaa.Ila huyu jamaa nahisi kuna kilevi anatumia sio bure.Au ngumi sio mchezo wake anafanya kama fan tu ndo maana hayuko serious.Anatukwaza mashabiki wake.
 
Akianza kushinda ataharibu brand yake na watu watamzoea kuwa anashinda mapambano. Watamuona wa kawaida. Unajua Tanzania inatakiwa ujitoe akili ufanye ujingaujinga ndio unapiga hela kwelikweli. Au awe ana balansi kidogo anashinda mapambano lakini pia anapiga mikwara mizitomizito kisha Anapigwa. Yaani nahisi atakuwa bondia namba moja duniani ambaye anapata hela ndefu kwa kupigwa [emoji1787]

Watu huku kwenye vibanda wengi wanamsubiria mandonga. Hata pambano kuu limezimwa. Hata watu hawana time nalo.
Hakuna kitu kama hicho.kwasababu haya mapambano yanafadhiliwa na mapromota.sasa sidhani kama kuna promota atakayekubali huo ujinga.Huyo bwana hana zaidi ya mapambano mawili mbele baasa ya hapo kila mpenda masumbwi atamdharau hata atoe tambo vip.Mashabiki wote tunapenda vitu vizuri kutoka kwa wake tunaowashabikia.
 
Muda bado, lakini ndo bondia kipenzi cha wengi kwa sasa Tz, anatisha kwa tambo na maneno ya kuogofya mpinzani.
Leo huko Songea alikuwa na mashabiki kibao, yaani kuna shabiki kampa ofa ya kutembelea Jeep huku akiongea na mashabiki wake akiwa juu mithili ya Magufuli akiongea na umati wa wananchi.

Mandongo inatakiwa leo apigwe tena, hii itasaidia kuongeza brand yake kuliko akishinda pambano lake usiku huu.

We ndo ulimchulia lkn bora angeshinda sasa anapotea kabisa mzee [emoji28][emoji28]
 
Watanzania ni watu wa kudandia vitu Wala hakuna anayempenda huyo mandonga hata wanaopenda boxing yenyewe wanahesabika.....MTz akishaona kitu kinatrend mtandaoni na yy anaunga tela anafuata mkumbo

Kamata mfuata mkumbo mmoja muulize round moja ya boxing ina dk ngap Kama hujashangazwa na majibu yao

Manzi wangu sio mshabiki wa vitasa kabisa lakini ilibidi anilazimishe twende baa tukamuangalie Mandongo [emoji23][emoji23]

Sidhani kama upo sahihi kusema wanafuata mkumbo kwa trend za mitandaoni....... ndio dunia ya sasa ilivyo all over the World na sii Bongo tu

Mandonga anakipaji cha kujibrand kwa tambo zake za ki comedian, ukimuona anavyotamba kwenye social media na historia yake lazima utatamani kuona atafanya nini ulingoni

Sikuamini nilichokiona, pambano la mandongo ndio lilikua linasubiriwa kwa hamu kubwa na washabiki “wapya” wa ngumu ambao kimsingi walikua wengi kuliko washabiki kindaki ndaki wa boxing ambao walikua wana shauku na pambano mama

Usibeze kupaji cha mandonga katika kuvutia watu kumuangali kwa majigambo kwa mgongo wa wabingo tunafuata mkumbo wa trend
 
Sasa na wewe usiwe kilaza hapa Jf ni the home of the Great Thinkers. Nimesema Karim Mandonga ndio " Mike Tyson" wa ngumi za Tz kwa sasa , sijasema ni Mike Tyson. Mike Tyson is not the same as " Mike Tyson"

Wakati wa utawala wake Mike Tyson alipendwa sana na mashabiki wa ngumi duniani. Haimaanishi Mike Tyson ndio alikuwa bondia bora hell no.

Wakati wake kulikuwa na mabondia wa ukweli kama " The Real Deal" ambae mimi nasema ndio bora kabisa kuwahi kutokea kwenye uso wa dunia ukiachana na " Utatu mtakatifu wa mabondia" i.e Mohamed Ali, George Foreman na Joe Frazier.

But wakati wa Tyson, Tyson aliimbwa yeye tu. It was as if he was the only boxer.

Kama asingekuwa exposed na Evander hiyo mwaka 96 basi up to this time bado runge amini Mike ndio bondia bora wa wakati wote.

Back to Mandonga. Mandonga ametokea kupendwa sana na watu.

Huwezi amini sasa hivi bar zote Tz zimejaa kila mtu anataka kumtazama Mandonga.

Taifa zima limesimama kila mtu anataka kumshuhudia Mandonga akifanya vitu vyake.

Mangonga ni " Mike Tyson" katika aspect ya kupendwa na watu.

50 cents aliwahi kusema mwaka 2003 na mnukuu " in hood they say there is no business like ho business but on hollywood they say there is no business like show business" na mimi naongeza yangu " In Tanzania Boxing there is no business like Karim Mandonga".

Karim Mandonga mbele kwa mbele
Karim Mandonga mbele kwa mbele[emoji23]

LIKUD watakuja kumuua ujue
 
IMG-20220731-WA0004.jpg
 
Ngumi alizokuwa anapiga Tyson unazifananisha na za bondia gani dunia.ambao tumewaona.
 
Muda bado, lakini ndo bondia kipenzi cha wengi kwa sasa Tz, anatisha kwa tambo na maneno ya kuogofya mpinzani.
Leo huko Songea alikuwa na mashabiki kibao, yaani kuna shabiki kampa ofa ya kutembelea Jeep huku akiongea na mashabiki wake akiwa juu mithili ya Magufuli akiongea na umati wa wananchi.

Mandongo inatakiwa leo apigwe tena, hii itasaidia kuongeza brand yake kuliko akishinda pambano lake usiku huu.
haha, Mkuu naona utabiri wako ulitimia.
 
Back
Top Bottom