Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni: Katika Mgomo wa wafanyabiashara, kosa la Mwigulu Nchemba ni lipi?

Kama hujajua basi wewe ni moja wa tatizo
 
Huwezi kuwa mfanyabiashara ukaja kumtetea Mwigulu..
Mfumo WA Kodi WA kukadiria unaotoa mwanya Kwa watu wa TRA sio fair..
Mtu anakdiriwa Kodi milioni 350 wakati Kenya Kodi milioni 45 Kwa kontena Hilo Hilo...yote hayo ni policy..na usimamizi na Mwigulu ndo mhusika wa kubadilisha vyote...na kashauriwa kagoma ....

Wewe labda kakutuma uje umsafishe
 
Sasa ni Mwigulu kaleta Hilo? Hizo Sheria zinafungwa na Wataalamu wa uchumi na Kodi na zinapelekwa Baraza la Mawaziri kisha Bungeni,huko Bungeni Kuna wafanyabiashara Sasa kama ni mbaya Kwa nini wasizikatae?
 
Hayo madudu yanamtaka Waziri ashughulikiwe? Hayo si ni mambo ya Polisi,Kamishna wa TRA na Viongozi wa Mkoa?
Mwigulu/Waziri ni mtu wa sera sio mtu wa oparesheni..

Yeye kama waziri angeweza kufix mapema kabisa bila kufikia kwenye mgomo

Na Leo pm ameamua Tu kuficha aibu Yao ndio maana hakuwapa nafasi ya kuongea
 
Ila nimependa wamemnanga sana kwa maneno ya kejeli maana yeye huwa anajidai bingwa wa maneno ya kukararisha.

Kuna mwamba anasema,unajitia Dokta,Dokta wa wapi wewe[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwamba mapolisi wanavyokula Rushwa IGP ajiuzulu na akijiuzulu ndio polisi wataacha kula Rushwa?

Hakuna kosa la Waziri hapo Kuna chuki binafsi Zenye mlengo wa kisaiasa na hapo unaweza Kuta wameshindana huko kwenye biashara.
 
Chawa kazini hivi haujaoana malalamiko ya wafanyabiashara kwamba walikuwa wanakutana naye kwenye vikao na akitoka anaenda kufanya tofauti na walivyoongea
Au hajasikia wafanyabiashara wanavyomnanga
Wanasema wakilalamika anamwambia sijadiliani na waganga wa kienyeji[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]


Sema wafanyabiashara wamejua kumchamba jamaa bila kupepesa macho.
 
Yeye kama waziri angeweza kufix mapema kabisa bila kufikia kwenye mgomo

Na Leo pm ameamua Tu kuficha aibu Yao ndio maana hakuwapa nafasi ya kuongea
Lini walienda Kwa Waziri ikashindikana? Au Kuna sehemu wamesema waliomba appointments Kwa Waziri akakataa?
Kabla ya kwenda Kwa Waziri anatakiwa.kushughulikia malalamiko ya kijinai ni Mkuu wa Mkoa na vyombo vyake, Waziri anashighulika na maswala ya kisera sio operation za watekelezaji wa sera.
 
Ila nimependa wamemnanga sana kwa maneno ya kejeli maana yeye huwa anajidai bingwa wa maneno ya kukararisha.

Kuna mwamba anasema,unajitia Dokta,Dokta wa wapi wewe[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Na hii ndio inamfanyq watu wamchukie personally.. hadi kumbandika vitu😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…