Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni: Rais Magufuli yupo well-informed na fiti sana kichwani kwa kumbukumbu. Ana data hadi za majungu hatarishi ya ndoa!

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni: Rais Magufuli yupo well-informed na fiti sana kichwani kwa kumbukumbu. Ana data hadi za majungu hatarishi ya ndoa!

Pascal Mayalla,
hahahaaaa! kweli Pompeo ni baba lao.

yaani hadi wapiga zumari wa mfalme washaanza kuji distance naye na kuanza ku criticise ofisi yake?!

mazuri yanakuja 2020!!
 
Mkuu katika hilo la kuwafahamu wateule kuna katabia ka jiwe kuchimba makabila ya wateule, kuanzia wazazi wao.

Hii ilianza kama utani wa kawaida ila sasa inaonekana kama ni kigezo cha kupima uwezo wa kiutendaji wa mteule.

Hii tabia kama itaitwa "ukabila" au haitaitwa hivyo ni mbaya kwa mustakabali wa taifa! Siku baada ya siku qualifications za wateule zinaunganishwa na tabia za makabila yao, wahehe, wachaga, wazaramo, wahaya, wasukuma nk..Mtazamo wa haya makabila kama kigezo cha uteuzi unategemea na uelewa wake yeye kuhusu tabia za hayo makabila!!!
 
Taifa limefikia hatua ya hatari kabisa! Mbunge anataka mbunge mwenzie auawe kabla hajarudi nchini, wanasiasa wa CCM wanahamasisha kuua wapinzani wa Ccm kwenye mikutano ya wazi kabisa .....!

Rais anatakiwa apewe sifa kwa kukariri udaku wa wanandoa!! Mbona ni kama tumerogwa,!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
@pascalmayala anahoji ikiwa Rais anataarifa za wateule wake, hizi panga pangua zinatokeaje?

Ndugu pascal salamu.
1. Watu hubadilika, mtu aliyeaminiwa kisha akaamua kubadilika na kufanya hiyana, huitwa mnafiki. Kama Mungu amewaahidi wanafiki adhabu kali, basi wanadamu hatuna budi kuwapiga vita. Rais anapoteua, hakutumi ukasaini mikataba ya ajabu itakayoliingizia taifa hasara, ni wapuuzi wanaoamini kuwa Rais amewateua kwa kuwa anawapenda, hapana, amewateua kwasababu anawaamini, mkimuangusha, hana namna bali kuwatumbua. Hakuna kulindana.

2. Kuna nafasi ambazo zinahitaji uwe na kifua hasa, sasa mtu katumbuliwa uwaziri anataka aitishe press kubwabwaja, tulia, unapostpost utumbo kwenye social networks ili iweje, mbona simbachawene hakupost chochote. Mliopo kwenye teuzi jifunzeni kitu kwa simbachawene na cag wa tra. Ukitaka kuyapata ya moyoni ya mtu, muondolee mkate wake kwa muda.

3. Suala la TBC kukatisha matangazo si ishu ya mhimili uliojichimbia chini zaidi, tbc wanayo tbc2 na tbc safari. Ikiwa tbc one inarusha bunge live, matangazo ya ikulu yanaweza kuhamishiwa tbc2 au tbc safari halafu huku tbc one tukapitishiwa maandishi kwa chini kuwa tbc safari kuna matangazo ya mojakwamoja kutokea ikulu. Mtazamaji atachagua aende ikulu au abaki bungeni.

Ni hayo anko pascal kwa leo.
Iamokay
Negotiator out.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hapo kwenye kukatisha matangazo, hujui rais anaweza tangaza vita, sasa rais huku katangaza hali ya hatari,gizani, wakati tbc inamrusha vijembe kwa wabunge, kipi unahisi ni cha muhimu?!
 
Nadhani unatakiwa umkumbushe vizuri interview aliyoifanya kwa mkurugenzi wa Dodoma jinsi alivyokalishea kwa hekima na busara ila mimi nimeshangaa mtu ana degree ya kilimo anafanyaje kazi takukuru hahahaah kwenye research na investigation au alikua anafanya investigation ya mbegu za rushwa?
 
Kama anapenda information ivyo angetaka kujua askari 10 wanapotezaje maisha na 5 kujeruhiwa katika mazoezi.

Someone has to bear that responsibility lazima kuna uzembe huko.
 
Ule utaratibu wa Bunge liwe na channel yake uliishia wapi? Ungesaidia kuepusha muingiliano huu
 
Wanabodi,

Mnyonge Mnyongeni, Haki Yake Mpeni, Rais Magufuli, kwanza yuko well informed kwa upande wa data za utendaji wa wateule wake wote! kichwani yuko fiti sana katika utunzaji wa kumbukumbu kutoka kichwani, leo katika kuwaapisha viongozi wapya aliowateua hivi karibuni, alikuwa anatiririka na data za mmoja mmoja kwa kutaja sifa zake huku akishusha hadi taarifa za majungu wanazopigwa baadhi ya watendaji wake wazuri, na kwa upande wa watendaji wanawake, rais Magufuli ana data hadi za majungu ya kutaka kuwahatarishia ndoa zao.

Anajua umri wao, anajua elimu zao hadi za watoto wao; hadi anawajua waume zao na kuwapongeza kuwa wake zao ni wachapa kazi waadilifu hivyo wanapigwa vita na majungu, na majungu mengine ni majungu hatarishi kwa ndoa zaa, hivyo amewapongeza hadi waume zao kwa kuwa ni watu wenye misimamo wasiosikiliza majungu hivyo ndoa hizo zimesimama.

Rais mwenye data za namna hii huwezi kumdanganya kitu. Swali linakuja: Kama rais yuko well-informed kiasi hiki na kuna viongozi anawafahamu vizuri hivi na ana data hivi kuhusu wateule wake, sasa inakuwaje katika baadhi ya maeneo kunatokea pangua pangua za muda mfupi as if sometimes huwa anafanya kama guess work mfano CG wa TRA?

Au inakuwaje kwa hawa baadhi ya watendaji wake ambao wanafanya madudu ya ajabu ajabu, lakini rais hapelekewi data hadi sasa Wamarekani ndiyo wanakuja kusaidia kuoneshea madudu ya baadhi wateule wake?!. Au wateule hao hizo tuhuma walituhumiwa na hao Wamarekani ni tuhuma za uongo tuu ndio maana tumezipuuza au kama tuhuma hizo ni kweli, ili serikali kuonyeshea is not part of it, ilibidi by now, iwe tayari imeisha ji distance nazo, inawezekana ukimya huu ni uthibitisho kuwa mtuhumiwa alitumwa hivyo alikuwa anatimiza wajibu wake baada ya kupokea amri halali na yeye kuzitekeleza?!.

By the way, pia naomba kutoa kero za kukatizwa kwa matangazo ya maana mhimili mmoja wa Bunge na kuletewa live za Ikulu kuingilia matangazo ya mihimili mingine!.

Nimefanya kazi RTD na TBC, hivyo nafahamu umuhimu wa kukatisha matangazo yoyote ya kawaida ili kuleta matangazo yoyote ya live ya tukio muhimu zaidi. Hivyo, TBC ipo huru kukatisha matangazo yake ya kawaida wakati wowote na kutuletea matangazo ya live za Ikulu ila katika kufanya hivyo, it's not fair kukatisha live muhimu za Bunge ambazo ni scheduled program ya kipindi cha Maswali na Majibu, ndiocho kipindi pekee, wabunge wetu ambao ni wawakilishi wetu sisi wananchi, wanauliza maswali tuliowatuma, halafu kutupeleka Ikulu kutuosha tukio ambalo sio la dharura na less significant la kuapishwa kwa viongozi wapya.

Usawa wa mihimili Uko Wapi?, au Kila Event ya Mhimili uliojichimbia chini zaidi ni Muhimu Kuliko Events za Mihimili Migine?.

Mihimili mitatu ya Dola, Serikali, Bunge na Mahakama, in principle inapaswa kuwa sawa, iheshimiane na kustahimiliana. Sasa kunapotokea mihimili yote hii mitatu inaendesha matukio yanayostahili kutangazwa live na TBC, ratiba za matukio hayo zipangwe ili hii mihimili iheshimiane. Kitendo cha kukatishwa kwa matangazo ya mhimili mmoja wa Bunge live, kwa ajili ya kuletewa matangazo ya live ya Mhimili mwingine wa serikali pale Ikulu si sawa na si haki hata kama muhimili mmoja umejichimbia zaidi lakini heshima ya mihimili ibaki pale pale!.

Nini muhimu kati ya live ya Bunge na live ya Ikulu?
Umuhimu wa tukio lolote unapimwa kwa significance, ukubwa na udharura.
Kila mtu anajua kuwa wakati wa kipindi cha vikao vya Bunge, TBC inafanya live ya dakika 60 ya kipindi cha maswali na majibu. Kwa vile Bunge ni Mhimili, wapanga ratiba wa shughuli za rais, wanapaswa kuliheshimu Bunge, hivyo kukitokea shughuli za rais zinazohitaji kutangazwa live kipindi cha Bunge, then Bunge lingepaswa kuheshimiwa, shughuli za rais zipangwe kuanza saa 4:00 asubuhi ili tusi disrupt matangazo ya Bunge live.

Japo Rais ndie mtu mkubwa kuliko wote, tukio la kuapisha viongozi wapi siyo tukio muhimu kivile ku-justify kukatika Bunge live ambalo ni la wananchi, kutuletea matangazo ya Ikulu ya mtu mmoja na wateule wake!

It is as if live za Bunge ambazo ziko scheduled zinatangazwa kwa hisani tu; likitokea lolote Ikulu, no matter tukio la Ikulu ni insignificant kiasi gani, matangazo ya Bunge yanakatishwa tunapelekwa Ikulu. Kama wapanga ratiba wa Ikulu wangepanga live ya Ikulu ianze saa 4:00 baada ya live ya Bunge, what does Ikulu stand to lose kwa kuanza saa 4:00?, unless watu kuapishwa nayo ni dharura!.

Najua ni kweli Ikulu ni muhimu, ila kiukweli kilichokuwa kinachofanyika ikulu ukilinganisha na kilichokuwa kinafanyika Bungeni, kile cha bungeni ni muhimu zaidi. Ikulu pia inawajibu wa kuliheshimu Bunge.

Hata hivyo hongera TBC kutuletea matangazo ya live ya ajali ya Walokole Moshi ambayo hii sasa ni live ya dharura kweli.

Nawatakia Jumatatu Njema.

P
Ni aibu kuwa na rais anayefuatilia na kujua mambo ya vyumbani kwa wateule wake lakini hajui mtu anayenyima haki raia wenzake kuishi.
 
Back
Top Bottom