MO Dewji anawazidi vipi utajiri Bakhresa na Rostam Aziz?

MO Dewji anawazidi vipi utajiri Bakhresa na Rostam Aziz?

Mo mjanja mjanja tu na sitoshangaa ikija kugundulika amepika takwimu. Tajiri gani viwanda vyake vichafu na vimechoka, magari mengi mabovu na wafanyakazi wake wengi wana hali duni kimaisha.
Mfanyakazi wa Bakhresa na Rostam hiwezi kumfananisha na wa Mo kwa kuangalia hali zao za maisha.
Canter za natairi matatu
 
Huyu jamaa utajiri wake wa magumashi na kiwanda cha juice eti ndo tajiri namba moja.

Ukija kwa Bakhressa
Ana meli, ngano soda kiwanda cha sukari chenyd thamani ya 600 bilions
Azam tv, Azam pesa.

Rostam aziz anayemiliki kampuni ya ndege, caspian tigo Tanzania Taifa gas inakuwaje tunaambiwa huyu mbabaishaji eti ndo tajiri wa tz ama anafanya ubabaifu aonekane hivo.
Uko na mawazo kama mimi, sijawahi kuamini kama mo ana mzidi pesa Bakhressa
 
Hilo mbona lishajadiliwa sana humu na watu wakaliweka sawa.

Hii post ni ya kwenye moja ya hizo thread iliwekwa na mtaalamu Chief-Mkwawa

Hizi ni data chache ambazo zinaweza kukufumbua macho
1. asilimia 5 ya wafanyakazi wote waliopo kwenye formal sector Tanzania ni waajiriwa wa metl, kwa lugha nyengine katika kila watu 20 walioajiriwa kwenye formal sector mmoja ni metl

2. mo ameajiri watu 24,000

3. metl ipo nchi 12 Africa na ipo pia nje ya Africa nchi chache

4. asilimia 3.5 ya pato la taifa linatokana na mo

so hizi ni baadhi ya comparison za mo na bakhresa

-mo wafanyakazi around 24,000 bakhresa around 8,000
-metl nchi 12 na azam nchi 8
-metl pato 1.5 billion na azam pato 800 million

hizo data zote nimetoa about pages ya website zao.
Azam Worldwide - Azam Bakhresa Group
About Us | MeTL

kifupi mkuu mo ana hela kuliko bakhresa na wala hawalingani, maana amemzidi zaidi ya mara mbili.

watu wanashindwa kuamini sababu Bakhresa vitu vyake vyote vipo kwenye brand moja ya azam, ila mo ana viwanda na brand na biashara nyingi sana.

Mo kama mzalishaji
mafuta ya nyumbani
-mafuta maisha
-mafuta safi
-blueband mo margarine
-mafuta mpishi
-mafuta sunflower

vinywaji
-maji ya maisha
-maji masafi
-juice za pride
-soda za mo

nguo
-hakuna kampuni kubwa ya nguo kusini mwa jangwa la sahara kushinda metl. wana viwanda karibia kila mkoa wakitengeneza bidhaa za kanga na vitenge.

Vyakula
-unga wa ngano
-sukari
-korosho (mo cashew)

baiskeli
hapa kuna baisikeli za kawaida na za miguu mitatu za NABICO

mafuta ya magari
kampuni ya mo ya star oil ni moja ya wasambazaji wakubwa wa mafuta. uwezo wa lita milioni 5 kwa siku.

sabuni
-sabuni za royal
-sabuni za taifa
-sabuni za poa

mo kama mfanya biashara anaeagiza vitu nje
-agent wa LG tanzania analeta vitu kama mashine za kufulia, oven, mafridge na bidhaa nyengine za lg
-Agent wa TCL tanzania na TV zake
-analeta mitumba ya nguo
-AC za airlux
-battery za remote
-tractor za kulimia
-na mengine mengi kama big G, biscuit, tambi etc

mo kama muuzaji vitu nje ya nchi
jamaa anauza vitu vingi sana nje ya nchi kama
-katani
-korosho
-mbao
-nta
-choroko
-bidhaa nyengine tulizozitaja juu.

angalia hio diversity then compare na bakhresa.

Watu wanaijua mo energy tu.
 
wafanyakazi wake wengi wana hali duni kimaisha.
Mfanyakazi wa Bakhresa na Rostam hiwezi kumfananisha na wa Mo kwa kuangalia hali zao za maisha.
Unashangaa hilo mkuu, tajiri namba 3 duniani Jeff Bezos mmiliki wa kampuni ya Amazon analalamikiwa kwa kuwalipa mishahara kiduchu wafanyakazi wake. Na hata kumewahi kuwa na mgomo kwa baadhi ya wafanyakazi wake

Ndo mambo ya capitalism unyonyaji haukwepeki
 
Naamini Rostam Azizi ndiye Tycoon namba moja hapa nchini, hawa wengine ni Chawa tu.

Fuatilieni vizuri ukweli mtaujua.

Huyu Mwamba ni level ingine.

Hope one day nitazidi hapo alipofikia.
Ana ela kweli ila kaachwa mbali sana na mo, rostam ana $900bl mo ana $1.5tr kama nmekosea mtanisahihisha....

Inawezekana ana ela kumzidi mo lkn anaficha baadhi ya mali na ac zake zisijulikane
 
Dukani kwangu.

AZAM- Ngano, Azam energy, Azam embe

MO-Mo extra, mo Tambi, mo poa bar soap, mo poa detergent, Mo taifa bar soap, Mo power betery, Mo malta, mo chocolate biscuit, Mo 29, Mo halisi.
Azam ana bidhaa nyingi sana kuliko hizo ulizo taja mkuu na mtaani zipo tuna ziona pia jaribu kufanya 'critical analysis' then uje na hizo comparison ulizo taka kuonyesha hapa.
 
Ee
Ana ela kweli ila kaachwa mbali sana na mo, rostam ana $900bl mo ana $1.5tr kama nmekosea mtanisahihisha....

Inawezekana ana ela kumzidi mo lkn anaficha baadhi ya mali na ac zake zisijulikane
Eenh umekosea,hasa hapo kwenye$ 1.5 tr, ambayo hata musk Hana!
 
Ana ela kweli ila kaachwa mbali sana na mo, rostam ana $900bl mo ana $1.5tr kama nmekosea mtanisahihisha....

Inawezekana ana ela kumzidi mo lkn anaficha baadhi ya mali na ac zake zisijulikane
Hapo kwenye utajiri wa Mo hizo ni billion na sio trillion mkuu
 
Mo mjanja mjanja tu na sitoshangaa ikija kugundulika amepika takwimu. Tajiri gani viwanda vyake vichafu na vimechoka, magari mengi mabovu na wafanyakazi wake wengi wana hali duni kimaisha.
Mfanyakazi wa Bakhresa na Rostam hiwezi kumfananisha na wa Mo kwa kuangalia hali zao za maisha.
Na wewe baba yako ana kiwanda chochote?
 
Huyu jamaa utajiri wake wa magumashi na kiwanda cha juice eti ndo tajiri namba moja.

Ukija kwa Bakhressa
Ana meli, ngano soda kiwanda cha sukari chenyd thamani ya 600 bilions
Azam tv, Azam pesa.

Rostam aziz anayemiliki kampuni ya ndege, caspian tigo Tanzania Taifa gas inakuwaje tunaambiwa huyu mbabaishaji eti ndo tajiri wa tz ama anafanya ubabaifu aonekane hivo.
inakusaidia nini ukijua?
 
Back
Top Bottom