Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Siku chache zillizopita, mfanyibiashara maarufu nchini Mo, alihojiwa kwa mara ya kwanza tokea kuachiliwa huru mwaka jana na chombo cha habari cha nje, shirika la utangazaji la BBC
Nilisikiliza kwa makini sana clip hiyo na ningependa maswali yafuatayo yajibiwe na viongozi wetu wa serikali
1. Siku ya kwanza baada ya kutekwa kwake, tulimuona Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, akiongea na waandishi wa habari na kutueleza watanzania kuwa mfanyibiashara huyo ametekwa na watu wasiojulikana, lakini wakati huo huo akatueleza kuwa watekaji hao ni watu wa kutoka nje, ambao wanaongea lafudhi kama vile ya kizulu toka Afrika Kusini, je yeye alijuaje kuwa watu hao ni wageni, wakati uchunguzi wa Polisi ulikuwa haujakamilika??
2. Tulimsikia pia mfanyibiashara huyo Mo "akijaribu" kuunga mkono kauli hiyo ya mkuu wa mkoa wa Dar katika mahojiano yake na BBC. Hata hivyo alieleza kwenye clip hiyo kuwa watu hao walikuwa wanataka "lumpsum" na akaendelea kueleza kuwa watu hao waliweza kumuanganisha na mtu mwingine, ambaye hakuwepo kwenye hilo eneo alilokuwa ametekwa na waliongea kuhusu madai yao ya pesa, lakini akazidi kuongea kuwa mtu huyo wa nje, alimpa "option" ya kuweza kuongea kiswahili au kiingereza, hivi inawezekanaje kwa watekaji hao, ambao tuliambiwa kuwa ni wageni wasioweza kuongea hata kidogo kiswahili na kiingereza, waweze kumuunganisha na huyo mtu wa nje ambaye anaongea kiswahili na kiingereza??
3. Tuliambiwa kuwa watekaji hao waliweza kumtelekeza eneo la Ghymkana, bila kumdhuru na wala hawakupata madai yao ya fedha, ilikuwaje walimwacha akiwa hai, iwapo hawajitimiziwa kile walichokitaka??
4. Ilikuwaje watekaji hao wa kigeni waweze kumwachia mateka wao eneo la Gymkhana, ambalo ni la wazi sana, wakati security ya nchi ilikuwa katika kiwango cha juu sana cha tahadhari ya kiusalama??
5. Je kama watekaji hao walikuwa ni wa kutoka nchi za nje, waliwezaje kutoka hapa nchini, wakati nchi ilikuwa katika kiwango cha juu sana cha tahadhari ya usalama??
6 Kama kweli waliondoka hao watekaji "wageni" ilikuwaje kwa Rais wetu hakuwatumbua wateule wake wa vyombo vya usalama, kwa kuonyesha uzembe wa hali ya juu wa kuhakikisha usalama wa raia na Mali zao??
7. Hivi watanzania kutokana na "scenario" nzima hiyo tuki-conclude kuwa watekaji hao wali-collude na watu wa serikali, tutakuwa tumekosea kweli??
Tungependa kuwaeleza watawala wetu kuwa watanzania siyo wajinga kiasi hicho cha kudanganywa kadri mnavyotaka!