Mo Dewji azidisha utata wa kutekwa kwake baada ya mahojiano BBC

Mo Dewji azidisha utata wa kutekwa kwake baada ya mahojiano BBC

Kuna sehemu alisema alikwenda kuiona hiyo nyumba alipokuwa kipindi kimetekwa ? Najiuliza hiyo nyumba ni ya nani ? Ipo wapi ? Kwa nini wasianze na mmiliki wa nyumba pia. Alikuwa kafungwa macho. Baadae alipokwenda kuona hiyo nyumba baada ya kuachiwa alijuaje ni hiyo nyumba alimokuwepo ?
Mbona una udadisi makini hivi leo?
Ngoja nikupe wazo zuri la mradi utakaokutoa moja kwa moja na pengine kumkaribia Mo mwenyewe.

Hapa kuna 'bonge' la movie. Fanya matayarisho yako kimya kimya kwa kukusanya habari na kuziweka vizuri. Unaweza hata kuandika kiwe kitabu. Hicho kitabu usikichapishe sasas hivi. Kaa nacho tu kwa mda maana umri bado unakuruhusu.

Wakati mwafaka ukifika, tengeneza movie. Shirikiana na Mo, anaweza akakubali kuwa 'steling' wa movie hiyo.

Haya, mradi ndio huo. Utanigawia kidogo 'royalty' kwa hili wazo?
 
Asante. Labda movie. Kitabu wabongo sio wasomaji kihivyo.
 
Hii ni movie ya kutunga, mo nae kapewa kipande cha script ili aendelelee kutudanganya.
si aseme tu ukweli kuwa ni makonda na baba'ke na pesa walivuta ya kutosha. Najua alipewa masharti!
Lakini IPO siku mambo yote yatakuwa hadharani, kwa vile watekaji na waandaji wa movie wote hawana weledi ndio maana wakatuonesha picha za Techno W5 badala ya CCTV camera!
Si ajabu pesa yake ndio imenunua Airbus!
Hahaaaaa......

Pesa yake ndiyo iliyonunua Airbus??

Umenichekesha sana Mkuu, kwa comment yako hiyo
 
Mimi naipenda story yake pale tu aliposema walimvua nguo zote alizokuwa nazo, wakamvisha kanga! Hivi hawakumchoma sindano kweli!! 💉
 
Siku chache zillizopita, mfanyibiashara maarufu nchini Mo, alihojiwa kwa mara ya kwanza tokea kuachiliwa huru mwaka jana na chombo cha habari cha nje, shirika la utangazaji la BBC

Nilisikiliza kwa makini sana clip hiyo na ningependa maswali yafuatayo yajibiwe na viongozi wetu wa serikali

1. Siku ya kwanza baada ya kutekwa kwake, tulimuona Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, akiongea na waandishi wa habari na kutueleza watanzania kuwa mfanyibiashara huyo ametekwa na watu wasiojulikana, lakini wakati huo huo akatueleza kuwa watekaji hao ni watu wa kutoka nje, ambao wanaongea lafudhi kama vile ya kizulu toka Afrika Kusini, je yeye alijuaje kuwa watu hao ni wageni, wakati uchunguzi wa Polisi ulikuwa haujakamilika??

2. Tulimsikia pia mfanyibiashara huyo Mo "akijaribu" kuunga mkono kauli hiyo ya mkuu wa mkoa wa Dar katika mahojiano yake na BBC. Hata hivyo alieleza kwenye clip hiyo kuwa watu hao walikuwa wanataka "lumpsum" na akaendelea kueleza kuwa watu hao waliweza kumuanganisha na mtu mwingine, ambaye hakuwepo kwenye hilo eneo alilokuwa ametekwa na waliongea kuhusu madai yao ya pesa, lakini akazidi kuongea kuwa mtu huyo wa nje, alimpa "option" ya kuweza kuongea kiswahili au kiingereza, hivi inawezekanaje kwa watekaji hao, ambao tuliambiwa kuwa ni wageni wasioweza kuongea hata kidogo kiswahili na kiingereza, waweze kumuunganisha na huyo mtu wa nje ambaye anaongea kiswahili na kiingereza??

3. Tuliambiwa kuwa watekaji hao waliweza kumtelekeza eneo la Ghymkana, bila kumdhuru na wala hawakupata madai yao ya fedha, ilikuwaje walimwacha akiwa hai, iwapo hawajitimiziwa kile walichokitaka??

4. Ilikuwaje watekaji hao wa kigeni waweze kumwachia mateka wao eneo la Gymkhana, ambalo ni la wazi sana, wakati security ya nchi ilikuwa katika kiwango cha juu sana kiusalama??

5. Je kama watekaji hao walikuwa ni wa kutoka nchi za nje, waliwezaje kutoka hapa nchini, wakati nchi ilikuwa katika kiwango cha juu sana cha usalama??

6 Kama kweli waliondoka hao watekaji "wageni" ilikuwaje kwa Rais wetu hakuwatumbua wateule wake wa vyombo vya usalama, kwa kuonyesha uzembe wa hali ya juu wa kuhakikisha usalama wa raia na Mali zao??

7. Hivi watanzania kutokana na "scenario" nzima hiyo tuki-conclude kuwa watekaji hao wali-collude na watu wa serikali, tutakuwa tumekosea kweli??

Tungependa kuwaeleza watawala wetu kuwa watanzania siyo wajinga kiasi hicho cha kudanganywa kadri mnavyotaka!
Yote hiyo ilikua kuzima ishu ya lisu antpass
 
Kwanza Mo hajawahi Kwenda Kituo chochote cha Polisi kutoa maelezo baada ya kutupwa.Ansasema alipigigia simu Baba yake baada ya kutupwa then akapelekwa nyumbani.... Baada ya hapo Kamanda Mambosasa alimfata nyumbani kwake kunywa chai na akamwacha nyumbani apumzike .......Ata kama Watanzania wana akili ndogo sana lakini sio kwa usani huu.
Ukiwa tajiri hata ukamataji utakuwa tofauti, ulishaona tajiri kabeba tanganyika jet ile ya kuminywa suluali juu na kutembelea vidole? Wao hufuatwa kwa busara, sasa uwe kapuku vibao utakula vyakutosha
 
Ukiwa tajiri hata ukamataji utakuwa tofauti, ulishaona tajiri kabeba tanganyika jet ile ya kuminywa suluali juu na kutembelea vidole? Wao hufuatwa kwa busara, sasa uwe kapuku vibao utakula vyakutosha
Wewe hujasikia kuwa Mo alifungwa na kamba mikono yote na kuzibwa mdomo wake na kitambaa pamoja na kuvuliwa suti yake na kupewa khanga kujihifadhi??

Huyo ni miongoni ya matajiri wakubwa duniani, kwa mujibu wa gazeti la Forbes, unaposema matajiri hawateswi, je huyo Mo hakuteswa kwa mawazo yako??
 
Fumbo mfumbie mjinga... mwerevu atalifumbua, hilo sakata lipo katika hali hiyo...

Cc: mahondaw
 
Bora angeendelea kukaa kimya maana anazidi kuiweka uchi serikali, inaonekana kalazimishwa kumsafisha jiwe.
 
Kawaida ya move la kihindi huwa linaacha maswali mengi,ni kama bongo move
 
Kasema aliachwa jirani na ofisi za EU siyo kule viwanjani......ndio akajikokota taratibu hadi hotelini ambako baba yake alienda kumchukua!

..maeneo karibu na ofisi za EU kuna walinzi.

..na kwanini alikwenda kujisalimisha hotelini badala ya kwenda wizara ya mambo ya ndani ambapo ni karibu zaidi na pana mapolisi.

..na watekaji watakuwa wajinga kiasi gani kwenda kumbwaga eneo lenye ulinzi wa Polisi na wa makampuni ya ulinzi 24/7?
 
Inaonyesha wazi kuwa huyu aliye-plan hii movie amebugi step. OVA
 
Wamejichanganya hao,upangaji wa tukio,uongo lazima ujitenge
 
Kuna sehemu alisema alikwenda kuiona hiyo nyumba alipokuwa kipindi kimetekwa ? Najiuliza hiyo nyumba ni ya nani ? Ipo wapi ? Kwa nini wasianze na mmiliki wa nyumba pia. Alikuwa kafungwa macho. Baadae alipokwenda kuona hiyo nyumba baada ya kuachiwa alijuaje ni hiyo nyumba alimokuwepo ?

MMMMMMMMM....M.OOIIIIIIKKKKKKKNB. B
 
mo mwenyewe katika mahojiano yake yamejaa nashukuru nyingi na mapambio mengi ya kusifu kitu ambacho kinonyesha anawajuwa vizuri walio mteka na bado anawaogopa. yaani alivyo kuwa anaogea akili yake yote ilikuwa inawaza watekaji watachukuliaje interview. kwa maana alikuwa anajuwa kabisa kuwa watekaji walikuwa wanasikiliza interview yake kwa makini. na kila alivyo ulizwa maswali ya kuhusu watekaji alikuwa anayakwepa kiaina au alikuwa anajaribu kurudia statements za police.
Huenda hata huyo aliyekuwa akiwasiliana naye, baada ya kupewa simu na watekaji, akawa ana-demand "Ramsom" ili Mo aachiwe huru akawa ni Jiwe mwenyewe!

By Zitto's voice "The United Republic of Gangsters"
 
..maeneo karibu na ofisi za EU kuna walinzi.

..na kwanini alikwenda kujisalimisha hotelini badala ya kwenda wizara ya mambo ya ndani ambapo ni karibu zaidi na pana mapolisi.

..na watekaji watakuwa wajinga kiasi gani kwenda kumbwaga eneo lenye ulinzi wa Polisi na wa makampuni ya ulinzi 24/7?
Amesema wahudumu wa pale hotelini wanamjua.....ndio maana walipomwona tu kabla hajasema chochote walimpigia simu baba yake!
 
Back
Top Bottom