Wakati ule, kulikuwa na doria kila kona ya Dar.
Kuna maswali mengi, ambayo wengi hawajiulizi. Ilikuwaje baada ya kupatikana kwake pale sehemu alipotelekezwa, hawakufahamishwa polisi ili waje pale kumchukua, au kumpeleka kwake? Ilikuwaje hao wazazi wake watoke huko kwao, bila kuwafahamisha polisi kuwa mtoto wao yupo sehemu fulani, bali wakaenda moja kwa moja mpaka sehemu ya tukio wao tu? Pia, hebu tujiulize, hao wazazi, walikuwa na ujasiri gani wa kuondoka na mtoto wao, usiku huo wa manane bila kuwafahamisha polisi na kurudi nyumbani kwao? Hebu tujiulize, kama wangekutana na doria ya polisi njiani, wakasimamishwa, na hao polisi kumuona huyo Mo kwenye gari, wangeaminiwa kuwa wao (hao ndugu zake) sio wao ndio walikuwa wamemficha sehemu na kwa wakati huo wanamuhamisha sehemu nyingine?
Hesabu za haraka za bila kumung`unya maneno, akina Mambosasa wanajua Mo alikuwa wapi, na kwa madhumuni gani.