Mo Dewji azidisha utata wa kutekwa kwake baada ya mahojiano BBC

Ukiunganisha dots unapata jawabu.......
 
Hahahaaa..If am not mistaken he also mentioned something like, during the all deal there was a time, he heard a sound like of a chopper zooming around a place where he was kept???.. it means may b the hijackers even they own choppers or what???...very interesting ...only God knows...
 
Mtu mnayetaka kumlisha maneno yenu mnayotaka kuyasikia anasema hana habari kabisa na nyie! Infact hata hatambui uwepo wenu. Hata mnapopatwa na matatizo na vyombo vya dola hana hata sekunde moja ya kuwatetea. Lakini ninyi mnajifanya mnajua haki zake mwenyewe kuliko yeye anavyozijua. Endeleeni kupoteza muda wenu.
 
Kwanza Mo hajawahi Kwenda Kituo chochote cha Polisi kutoa maelezo baada ya kutupwa.Ansasema alipigigia simu Baba yake baada ya kutupwa then akapelekwa nyumbani.... Baada ya hapo Kamanda Mambosasa alimfata nyumbani kwake kunywa chai na akamwacha nyumbani apumzike .......Ata kama Watanzania wana akili ndogo sana lakini sio kwa usani huu.
 
mo mwenyewe katika mahojiano yake yamejaa nashukuru nyingi na mapambio mengi ya kusifu kitu ambacho kinonyesha anawajuwa vizuri walio mteka na bado anawaogopa. yaani alivyo kuwa anaogea akili yake yote ilikuwa inawaza watekaji watachukuliaje interview. kwa maana alikuwa anajuwa kabisa kuwa watekaji walikuwa wanasikiliza interview yake kwa makini. na kila alivyo ulizwa maswali ya kuhusu watekaji alikuwa anayakwepa kiaina au alikuwa anajaribu kurudia statements za police.
 
Kutokana na interview ile aliyofanya na mtangazaji Salim Kikeke wa BBC.

Nilicho-realize ni kuwa, pamoja na masahibu yote yaliyomkuta, ni dhahiri hivi sasa Mo "amelazimishwa" ajiunge kikamilifu na ile "praise and worship team for Magufuli"
 
Tukubali tu ni hivyohivyo, waliingia nchini kupitia Namanga na gari yao pickup yenye namba za msumbiji nao wanaongea kireno na ni wazungu na cctv iliwafuata kuanzia Oysterbay mpaka Kijitonyama wakapotea! Leta chai tunywe.
 
nimeogopa pale aliposema alipotekwa alivuliwa nguo zote akabaki amejifunga khanga tu...hawa jamaaa hawakumpa kifiro kweli
Mmh.......

Usifike huko Mkuu
 
Kimsingi hii script mpya ya Mo imeleta taharuki zaidi kuliko ile ya Mambosasa.
Anyway tuendelee kuenjoy background beat
 
Kimsingi hii script mpya ya Mo imeleta taharuki zaidi kuliko ile ya Mambosasa.
Anyway tuendelee kuenjoy background beat
Unadhani kwa maelezo ya Mo, kuwa alisikia milio ya chopa ikipita juu "ku-patrol" eneo la tukio, hivi unadhani unaweza wahisi kina nani kama washukiwa wakuu wa tukio lile??

Ukiunganisha dots hapo unapata jawabu
 
Hahaha umesahau, "mchana walikuwa wanamfunga mikono nyuma, halafu wanamvua nguo zote kisha wanamfunga mikono kwa mbele, halafu wanamlaza ubavu wa kulia au kushoto..." hakumalizia walikuwa wanamfanyaje mtoto wa kihindi.

Mateka akipatikana huwa wanapelekwa Hospitali, yeye alipelekwa nyumbani kwake, kama vile katolewa guest house.

Mwacheni huyo atakuwa ALIJITEKA in Mambosasa voice.

Alijiteka kistaarabu, anapewa kila kitu anachotaka hahaha.

Alikuwa anapewa simu, je, alikuwa anaongea na nani kwenye hiyo simu ili iweje na anasema no ransom was paid?!

Uongei na ndugu zako, unaongea na nani na hiyo simu...?

Nani alikuwa upande wa pili wa hiyo simu?!

The whole thing is a HOAX.
 
Alafu kesho maafande wanakunywa chai pamoja na Mzee wake pale town huku wakipongezana. Nilichoona kwenye ile Interview ya Kikeke, Mo akiulizwa swali lenye utata anaishia kujibu nashukuru Watanzania kwa kuniombea!
 
Kutokana na interview ile aliyofanya na mtangazaji Salim Kikeke wa BBC.

Nilicho-realize ni kuwa, pamoja na masahibu yote yaliyomkuta, ni dhahiri hivi sasa Mo "amelazimishwa" ajiunge kikamilifu na ile "praise and worship team for Magufuli"
Ni kweli, jamaa kila mara ni kumsifu mtukufu wa Chato utadhani amekaririshwa.
Hahahahaha! Hii nchi ya hovyo sana
 
Ni kweli, jamaa kila mara ni kumsifu mtukufu wa Chato utadhani amekaririshwa.
Hahahahaha! Hii nchi ya hovyo sana
Amelazimishwa kujiunga na "praise and worship team for Magufuli"

Ama sivyo ataishi kama shetani.......

Amelazimika kusalimu amri
 
Ukimsikiliza kwa makini sana na kutazama body language wakati akiulizwa baadhi ya maswali MO Dewji katika mahojiano na BBC utagundua kabisa Mo Dewji alikuwa ametunga uongo mwingine, tena uongo wa kulishwa maneno.

Kwa mfano.
1/Mo alisema watekaji walimfunika uso wakati wote alipokuwa mikononi mwao, na hapo hapo anatuambia haya
-Idadi kamili ya watekaji ilikuwa watu kadhaa! Aliwezaje kuwahesabu?
-Watekaji walikuwa wameshika bunduki na walikuwa mara mara wakimtishia kumuua kwa bunduki. Aliwezaje kuziona au kujua kwa hakika kuwa ni bunduki?

2/Anasema watekaji walitaka wapewe pesa ndio wamuachie. Sasa maswali makubwa mazito yanaibuka...
-Kwanini hasemi kiasi walichokitaka?
-Kwanini hasemi dhamira yake ilikuwa ni nini? Je, alikuwa tayari kutoa pesa au kutokutoa pesa?

-Kwanini hasemi kama pesa ilitolewa ama la ili yeye kuweza kuachiwa?

-Angewezaje kuwapa pesa, ikiwa yupo mikononi mwao?

-Kwanini walikuwa wakimtishia kumuua yeye ikiwa dhamira yao ilikuwa ni kupewa pesa na yeye hakuwa na pesa mkononi na hakukuwa na namna ya kuweza kuzileta hizo pesa?

3/Mo Dewji anasema alikuwa mateka kwa siku 11 mfululizo, na siku zote hizo alikuwa amefungwa uso, mikono na miguu kabla ya kuachwa akiwa katika hali hiyo hiyo usiku wa manane maeneo ya viwanja vya Gymkhana. Sasa maswali tata yanaibuka...

-Alijuaje watekaji wamekimbia na kumtekeleza muda mchache tu baada ya kuachwa pale Gymkhana wakati alikuwa kufungwa uso?

-Aliwezaje kupata nguvu, ujasiri na mbinu za kuweza kujifungua kamba alizofungwa mara moja baada ya kutelekezwa usiku?

-Kwanini maelezo ya kupatikana kwake yanatofautiana mnoo na polisi?

4/Mo Dewji anasema watekaji walijipanga, wakamvizia na walikuwa na dhamira kamili. Sasa embu tujiulize haya maswali...

-Kwanini yeye na ndugu zake waliamua kukaa kimya kabisa kwa muda mrefu toka alipopatikana huku wakisita kabisa kulizungumzia suala lake? Wanamuogopa nani?

-Kwanini Mo Dewji hataki kuhoji kusua sua kwa upepelezi wa kesi unayohusu kutekwa kwake?

-Kwanini hataki kuzungumzia suala la CCTV camera zilizokuwepo maeneo yale aliyotekwa ili kupunguza utata?

-Kwanini analipongeza jeshi la polisi na serikali ya awamu ya tano kuweza kupatikana kwake, huku akikiri wazi wazi kuwa ni mbinu na juhudi za watekaji wenyewe zilizopelekea kuachiwa kwake akiwa mzima na salama?
 
Hii ni movie ya kutunga, mo nae kapewa kipande cha script ili aendelelee kutudanganya.
si aseme tu ukweli kuwa ni makonda na baba'ke na pesa walivuta ya kutosha. Najua alipewa masharti!
Lakini IPO siku mambo yote yatakuwa hadharani, kwa vile watekaji na waandaji wa movie wote hawana weledi ndio maana wakatuonesha picha za Techno W5 badala ya CCTV camera!
Si ajabu pesa yake ndio imenunua Airbus!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…