Mo Dewji: Karibuni nitaikatia tamaa Simba

Mo Dewji: Karibuni nitaikatia tamaa Simba

Mo ana hoja lakini mbumbumbu wanalalamika
Fanya mabadiliko yawepo
Mo anawekeza pesa yako mfumo wa zamani hapati faida
Timu imeshikwa na wazee hawataki mabadiliko
Mo ni mfanyabiashara anataka faida aweke hela apate hela
Mbumbumbu lawama kibao mpe mangungu asiyetaka mabadiliko
 
Rais wa heshima wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'Mo Dewji'kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema "Transformation ya Simba bado haijakamilika. huu ni mwaka wa 6. Karibuni ntakata tamaa"

Mohammed Dewji aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu Simba miaka minne mfululizo hadi alijiuzulu nafasi hiyo mnamo Septemba 21, 2021.

Wakati akitoa taarifa yake ya kujiuzulu alisema "Nimeachia nafasi hiyo lakini nitaendelea kuwa Simba mpaka siku ya mwisho, sijajiondoa kwenye Simba bado ni mwekezaji mimi kwa sasa mara nyingi sipo nchini Tanzania nakuwa nje"
Kama anataka kuondoka aondoke tutapitia kipindi kigumu wanasimba kitapita tu kwanini atingingishe kibiriti wakati muhimu na nyeti kama huu
 
Mbabaishaji huyu akwende zake tuchangishane hata buku buku kuliko kuendelea na hii aibu.
Kwa kweli Dewji anawakosea Sana Wanasimba. Ni kama hataki kusikia Wana furaha yeye lazima alete Jambo la kuvuruga. Hivi suala kubwa kama Mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa timu ni ya kuuliza mitandaoni? Hizi timu za Kariakoo zimebeba itikadi, Imani na furaha ya watu wengi. Kutibua furaha Yao bila mpangilio ni kuwapa faida upande wa pili kuwazodoa watu wako.
 
Mfadhili lialia na mwekezaji domo kaya MO, amewaonya washabiki Simba wakiendelea kumvunjia heshima kutokana tweet yake.Atawaacha wachezaji huko waliko pre season bila kulipa gharama.na kusababisha kuzuiwa mabegi yao na watarudi kwa miguu.hapendi ujinga wakati hawana mchango .ada za kadi uawanahama hazifiki hata milioni 20.wanaongea Nini?
 
Hao ndio Wawekezaji wa Bongo halafu Mbunge wa Nzega Vijijini Dr Kigwangalla akiwaponda Wawekezaji Uchwara mnamrushia maneno makali makali

Sasa huyu na DP World nani ana afadhali?😃

Watanganyika bado tuna Ututusa mwingi sana, imagine Makolo anakabidhiwa Bandari katika Sera ya Uwekezaji wa ndani

Mungu wa mbinguni atupe salama!
 
Hao ndio Wawekezaji wa Bongo halafu Mbunge wa Nzega Vijijini Dr Kigwangalla akiwaponda Wawekezaji Uchwara mnamrushia maneno makali makali

Sasa huyu na DP World nani ana afadhali?😃

Watanganyika bado tuna Ututusa mwingi sana, imagine Makolo anakabidhiwa Bandari katika Sera ya Uwekezaji wa ndani

Mungu wa mbinguni atupe salama!
MO ni tapeli anaishi kitapeli sn
 
Back
Top Bottom