Mo Dewji, msimu ujao tenga milioni 500 za ubingwa, baada ya hapo Yanga na GSM hawatakusumbua tena

Mbona mnalialia? Hapa kinachoongelewa ni mazingira yanatengenezwa ya timu zaidi ya 8 kuona kuiachia Yanga ishinde dhidi yao ni kulipa fadhila kwao kwa viposho wanavyopewa. Kinachoshauriwa hapa ni kwa Mo Dewji kuwaongezea posho kwa hizi timu ili kuweka mizania sawa ya ushindani katika ligi. Kuna shida kwenye hilo?
Huoni aibu wewe binti kumwambia mwanaume atege m 500 kwani wewe huwezi kuzitenga acha kumpangia binadamu mwenzako matumizi ya pesa zake .[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
Kama mwanachama hai wa Simba Sports Club, nina haki ya kuzungumza na kutoa mawazo yangu kwa Mwenyekiti wangu.
 
Unampa GSM credit ambayo siyo yake. Hakuna mdhamini katika ligi anayetoa pesa kwa timu zote kulinganisha Azam Media. Hivyo viposho ni vya kuzichanganya tu hizo timu ili zidhanie zinahitaji kulipa fadhila kwa Yanga.

Kama Singida wanawehuka na kupagawa kisa kuahidiwa milioni 50 waifunge Simba, inakuwaje unaona milioni 100 ni ndogo ili kuifunga Yanga?

Halafu mbona kama umajisnitch. Yaani TAKUKURU wakae kimya kwa hichi GSM anafanya halafu waje kuamka pale mwingine anapoongeza motisha kwa hizi timu? Kwani mkataba wenu na hizo timu unasema hazitakiwi kuifunga Yanga?
 
Una ushauri wa kipumbavu sana. Yanga wana timu nzuri kuliko sisi kwa misimu mitatu mfululizo. Kama sisi simba tumeshindwa kumfunga yanga unategemea Pamba atamfunga Yanga?
Tabora kaifunga uto, ila Tabora hiyo hiyo imefungwa nje ndani na Simba. Azam kaifunga Uto, ila Azam hiyo hiyo imeachia pwenti 4 kwa Simba na kuna uwezekano mkubwa wa uto kutoambulia hata pwenti moja kutoka kwa Azam msimu huu. Hili linakuambia nini kuhusu hoja yako?
 
Zabuni Huwa zinatangazwa wazi clubs kutaka wadhamini wa time offer zao

We tuma offer weka pesa nyingi zaidi ya GSM uone kama timu zitakataa pesa yako

Wewe unalazimisha GSM asidhamini timu wakati hata laki mfukoni huna ya kusaidia hizo timu
 
Simba alivofunga mara nne mfululizo kutia ndani kipigo cha mbwa mwizi cha goli 5 alikuwa na udhamini wa GSM
 
Hahahaha,kumbe unajijua eeh
Mimi na wewe nadhani tumemalizana. Umesema unachotaka na mimi nimesema ninachohitaji kusema, tusonge mbele.

Huwa naepuka sana kumuita mtu yoyote mjinga hata tukitofautiana vipi kimawazo na ninapoona mazungumzo yangu na mtu hayana faida au yana chembechembe ya chuki ndani yake sioni faida ya kuendelea na hayo mazungumzo.
 
Pesa atoe wapi wakati yuko kwwnye mchakato wa kuachana na Simba!
 
Acha hoja za kiupuuzi mkuu , Yanga ni bora kuliko timu yoyote katika ligi kuu ya NBC msimu wa tatu mfululizo. Kama una akili hutapinga hili Simba bado tunajenga timu na hilo lipo wazi ndani ya misimu mitatu tukicheza na yanga tunatafuta japo sare kitu ambacho nikigumu pia kwetu kwahiyo Yanga ikiifunga Simba GSM ametoa pesa? Tena bora yanga hui imepoa kuliko Yanga ya Nabi na msimu uliopita. Sema mashabiki wengi ni wajinga hawaelewai kitu kama wewe. Fuatilia Betway wanadhamini timu ngapi Epl au Parimatch then ulete mrejesho
 
Zabuni Huwa zinatangazwa wazi clubs kutaka wadhamini wa time offer zao

We tuma offer weka pesa nyingi zaidi ya GSM uone kama timu zitakataa pesa yako

Wewe unalazimisha GSM asidhamini timu wakati hata laki mfukoni huna ya kusaidia hizo timu
Eti "tuma offer weka pesa nyingi zaidi ya GSM". Nani kakudanganya kuwa GSM anatoa pesa kwa hizo timu kuzidi wanazopata kutoka kwa Azam Media? Je baada ya GSM kuingia kwenye hizo timu, mikataba yao na AZAM Media ilikoma?

Mtu akijitokeza kutoa motisha kama ambavyo NHC, Silent Ocean au ile kampuni ya Aluminium wamefanya kwa wachezaji bora wa timu kuna shida gani? Mbona kila siku tunasikia timu zinaahidiwa zawadi ili ziifunge Simba hatuoni mkipinga hilo?

GSM aendelee na udhamini wa hizo timu na akiweza aongeze timu nyingi zaidi. Sisi tutajalizia kuzipa hizo timu nguvu zaidi ya kupambana.
 
Huyo akili kisoda.
 
Wewe hutaki GSM kudhamini ligi ili iweje?
Hutaki atangaze bidhaa zake?
Ni mashindano wako kibiashara?
Mbona kampuni kampuni nyingi zimeweka udhamini?
Wewe dhamini uone kama timu zitakataa pesa yako
 
Ubora upi huo unaouongelea? Simba bado ipo mashindano ya CAF na Yanga imeishia makundi. Kwenye ligi tofauti ni pwenti 1 ambayo Jmosi inaweza kuyeyuka. Simba ndiyo timu iliyofungwa magoli machache zaidi mpaka sasa. Misimu 2 iliyopita, katika kila kipengele na takwimu ukiacha kuzidiwa pwenti, Simba ilikuwa ndiyo timu bora kuliko zote.
Inafikirisha sana kuona ligi ilikuwa na ushindani zaidi wakati timu zina njaa kuliko kipindi hiki ambacho zinaonekana kuwa na shibe. Niambie mwaka ambao Yanga ilikuwa inazifunga timu goli 5 na 6 kila siku kama miaka hii miwili ya udhamini wa timu 8 za GSM.
Simba alivofunga mara nne mfululizo kutia ndani kipigo cha mbwa mwizi cha goli 5 alikuwa na udhamini wa GSM
Hii hoja ni ya kijinga sana nashangaa sana nikisikia mtu anaitoa. Ukiibia mtihani mmoja halafu mingine sita ukiifanya bila kuibia, haiondoi ukweli kuwa kuna mtihani mmoja umeibia.
kwahiyo Yanga ikiifunga Simba GSM ametoa pesa?
Hii hoja ni ya kijinga sana nashangaa sana nikisikia mtu anaitoa. Ukiibia mtihani mmoja halafu mingine sita ukiifanya bila kuibia, haiondoi ukweli kuwa kuna mtihani mmoja umeibia.
 
Kuna mjinga anasema GSM Itaishtaki Jamii forums kisa
Sasa najiuliza atakaeshtakiwa ni alieandika au Jamii forums
Ukiona wamefika hapo kwenye vitisho inabidi uanze tu kuwaimbia Maji ya Shingo ya Daz Nundaz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…