Mo Dewji, msimu ujao tenga milioni 500 za ubingwa, baada ya hapo Yanga na GSM hawatakusumbua tena

Mo Dewji, msimu ujao tenga milioni 500 za ubingwa, baada ya hapo Yanga na GSM hawatakusumbua tena

Ni kweli kabisa, mtu anaanzisha uzi kuchafua brand za watu kutokana na ushabiki wa kijinga tu. Maudhui ya uzi ni kuwa GSM na Yanga wanapanga matokeo ya mechi. Shida inakuwa ni mtu aliyetoa hayo madai kifedha hajiwezi hivyo kumshtaki hawezi kulipa chochote, labda umfunge kama "civil prisoner", ambapo ni wewe unabeba jukumu la humhudumia akiwa ndani.
Mbona mnalialia? Hapa kinachoongelewa ni mazingira yanatengenezwa ya timu zaidi ya 8 kuona kuiachia Yanga ishinde dhidi yao ni kulipa fadhila kwao kwa viposho wanavyopewa. Kinachoshauriwa hapa ni kwa Mo Dewji kuwaongezea posho kwa hizi timu ili kuweka mizania sawa ya ushindani katika ligi. Kuna shida kwenye hilo?
Huoni aibu wewe binti kumwambia mwanaume atege m 500 kwani wewe huwezi kuzitenga acha kumpangia binadamu mwenzako matumizi ya pesa zake .[emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]
Kama mwanachama hai wa Simba Sports Club, nina haki ya kuzungumza na kutoa mawazo yangu kwa Mwenyekiti wangu.
 
GSM anadhamini timu nane,katika timu hizo nane,kila moja inapata,vifaa vya michezo,posho,usafiri na pesa kwa kipindi chote cha msimu husika, wewe unakuja na milioni moja yako katika mechi moja,na wakiipokea inamaanisha wamekataa posho,usafiri,pesa na vifaa vya michezo vya msimu mzima jambo linaloweza kuathiri pakubwa msimu mzima,katika hali hiyo timu zitakubali kuchukua hiyo 1m kisha zinafumuliwa kisawasawa na yanga halafu hamna pa kuwapeleka,mkipiga kelele TAKUKURU wapo macho kweli kweli mtaishia korokoroni. wekezeni kwa marefarii tu na mkae mkijua ARAJIGA AHMED hahongwi. Ni hayo tu mkuu SAYVILLE
Unampa GSM credit ambayo siyo yake. Hakuna mdhamini katika ligi anayetoa pesa kwa timu zote kulinganisha Azam Media. Hivyo viposho ni vya kuzichanganya tu hizo timu ili zidhanie zinahitaji kulipa fadhila kwa Yanga.

Kama Singida wanawehuka na kupagawa kisa kuahidiwa milioni 50 waifunge Simba, inakuwaje unaona milioni 100 ni ndogo ili kuifunga Yanga?

Halafu mbona kama umajisnitch. Yaani TAKUKURU wakae kimya kwa hichi GSM anafanya halafu waje kuamka pale mwingine anapoongeza motisha kwa hizi timu? Kwani mkataba wenu na hizo timu unasema hazitakiwi kuifunga Yanga?
 
Una ushauri wa kipumbavu sana. Yanga wana timu nzuri kuliko sisi kwa misimu mitatu mfululizo. Kama sisi simba tumeshindwa kumfunga yanga unategemea Pamba atamfunga Yanga?
Tabora kaifunga uto, ila Tabora hiyo hiyo imefungwa nje ndani na Simba. Azam kaifunga Uto, ila Azam hiyo hiyo imeachia pwenti 4 kwa Simba na kuna uwezekano mkubwa wa uto kutoambulia hata pwenti moja kutoka kwa Azam msimu huu. Hili linakuambia nini kuhusu hoja yako?
 
Unampa GSM credit ambayo siyo yake. Hakuna mdhamini katika ligi anayetoa pesa kwa timu zote kulinganisha Azam Media. Hivyo viposho ni vya kuzichanganya tu hizo timu ili zidhanie zinahitaji kulipa fadhila kwa Yanga.

Kama Singida wanawehuka na kupagawa kisa kuahidiwa milioni 50 waifunge Simba, inakuwaje unaona milioni 100 ni ndogo ili kuifunga Yanga?

Halafu mbona kama umajisnitch. Yaani TAKUKURU wakae kimya kwa hichi GSM anafanya halafu waje kuamka pale mwingine anapoongeza motisha kwa hizi timu? Kwani mkataba wenu na hizo timu unasema hazitakiwi kuifunga Yanga?
Zabuni Huwa zinatangazwa wazi clubs kutaka wadhamini wa time offer zao

We tuma offer weka pesa nyingi zaidi ya GSM uone kama timu zitakataa pesa yako

Wewe unalazimisha GSM asidhamini timu wakati hata laki mfukoni huna ya kusaidia hizo timu
 
Tabora kaifunga uto, ila Tabora hiyo hiyo imefungwa nje ndani na Simba. Azam kaifunga Uto, ila Azam hiyo hiyo imeachia pwenti 4 kwa Simba na kuna uwezekano mkubwa wa uto kutoambulia hata pwenti moja kutoka kwa Azam msimu huu. Hili linakuambia nini kuhusu hoja yako?
Simba alivofunga mara nne mfululizo kutia ndani kipigo cha mbwa mwizi cha goli 5 alikuwa na udhamini wa GSM
 
Hahahaha,kumbe unajijua eeh
Mimi na wewe nadhani tumemalizana. Umesema unachotaka na mimi nimesema ninachohitaji kusema, tusonge mbele.

Huwa naepuka sana kumuita mtu yoyote mjinga hata tukitofautiana vipi kimawazo na ninapoona mazungumzo yangu na mtu hayana faida au yana chembechembe ya chuki ndani yake sioni faida ya kuendelea na hayo mazungumzo.
 
Barua ya wazi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Mohamed Dewji.

Tajiri, nina neno moja kwako.

Msimu huu umefanya mambo makubwa sana pale Simba. Kikosi kinaeleweka, heshima inarudi katika ligi ya ndani na kimataifa.

Kuna uhuni mmoja ambao nafahamu unaujua maana malalamiko haya yamekuwepo kwa misimu kadhaa. Hapa naongelea kitendo cha mwendeshaji na mmiliki asiye rasmi wa Yanga, GSM kudhamini timu 8 katika ligi ya NBC.

Nakupa tahadhari kwamba mpango uliopo ni kuendelea kuongeza timu zinazodhaminiwa na GSM kwa kuzishusha kutoka katika ligi zile zinazokataa udhamini wa GSM na kuzipa udhamini zile zinazopanda. Walifanya hivyo kwa Pamba pale tu ilipopanda.

Pamoja na kwamba upinzani mkali ambao Simba inaupata kutoka haya matawi ya GSM ni faida kubwa kwa Simba kwa kuimarisha uwezo wa timu, ila ukweli unabaki kuwa nafasi ya kuchukua ubingwa wa ndani katika mazingira hayo inakuwa finyu sana. Huo ndiyo ukweli.

Kuna watu wamekuwa wanashauri na wewe utafute timu zako 8 uzipe udhamini ili mgawane pasu kwa pasu na hao GSM ila mimi naona wala hamna haja ya kutumia nguvu kubwa kulikabili hili. Ukituliza akili unaweza kuvuruga kabisa ramani yao ya vita.

Cha kufanya, tafuta kampuni ambayo itakuwa front na wewe simama nyuma yake. Kazi ya hiyo kampuni ni kutoa motisha ya zawadi kwa timu zote za ligi pale zinapocheza na Yanga. Weka kitita cha milioni 100 kwa kila mechi.

Ili kulikabili hilo, Yanga na GSM itabidi na wao waweke mzigo zaidi ya huo ili wachezaji wa hizo timu wakubaliane na hali.

Kumbuka siyo kila mechi utakayoweka dau Yanga itapoteza ila kwanza automatically utakuwa umetoboa mifuko ya hao GSM maana kila mechi utakayoweka dau inabidi na yeye atop up. Wakijifanya kukaza watafilisika.

GSM na Yanga wakiamua kutoweka dau wapambane haki bin haki, watatumia nguvu kubwa sana na lazima watadondosha points.

Ukishapata mechi zako 5 ambazo Yanga itapoteza, unafunga mahesabu yako. Kinachobaki ni Simba kucheza mechi zake kama ambavyo imefanya msimu huu. Sitegemei Simba ikicheza kwa nidhamu kama iliyoonyesha msimu huu inaweza kupoteza point 15 ndani ya msimu mmoja.

Nina uhakika ukifanya hivi msimu mmoja au miwili kuna watu akili zitawakaa sawa.

Ubaya Ubwela.
Pesa atoe wapi wakati yuko kwwnye mchakato wa kuachana na Simba!
 
Tabora kaifunga uto, ila Tabora hiyo hiyo imefungwa nje ndani na Simba. Azam kaifunga Uto, ila Azam hiyo hiyo imeachia pwenti 4 kwa Simba na kuna uwezekano mkubwa wa uto kutoambulia hata pwenti moja kutoka kwa Azam msimu huu. Hili linakuambia nini kuhusu hoja yako?
Acha hoja za kiupuuzi mkuu , Yanga ni bora kuliko timu yoyote katika ligi kuu ya NBC msimu wa tatu mfululizo. Kama una akili hutapinga hili Simba bado tunajenga timu na hilo lipo wazi ndani ya misimu mitatu tukicheza na yanga tunatafuta japo sare kitu ambacho nikigumu pia kwetu kwahiyo Yanga ikiifunga Simba GSM ametoa pesa? Tena bora yanga hui imepoa kuliko Yanga ya Nabi na msimu uliopita. Sema mashabiki wengi ni wajinga hawaelewai kitu kama wewe. Fuatilia Betway wanadhamini timu ngapi Epl au Parimatch then ulete mrejesho
 
Zabuni Huwa zinatangazwa wazi clubs kutaka wadhamini wa time offer zao

We tuma offer weka pesa nyingi zaidi ya GSM uone kama timu zitakataa pesa yako

Wewe unalazimisha GSM asidhamini timu wakati hata laki mfukoni huna ya kusaidia hizo timu
Eti "tuma offer weka pesa nyingi zaidi ya GSM". Nani kakudanganya kuwa GSM anatoa pesa kwa hizo timu kuzidi wanazopata kutoka kwa Azam Media? Je baada ya GSM kuingia kwenye hizo timu, mikataba yao na AZAM Media ilikoma?

Mtu akijitokeza kutoa motisha kama ambavyo NHC, Silent Ocean au ile kampuni ya Aluminium wamefanya kwa wachezaji bora wa timu kuna shida gani? Mbona kila siku tunasikia timu zinaahidiwa zawadi ili ziifunge Simba hatuoni mkipinga hilo?

GSM aendelee na udhamini wa hizo timu na akiweza aongeze timu nyingi zaidi. Sisi tutajalizia kuzipa hizo timu nguvu zaidi ya kupambana.
 
Ata viongozi wa Simba wanakuona ni mbumbumbu katika hoja yako.

GSM ali ingia mkataba na Tff kuwa mdhamini mwenza na NBC kwa Bilon moja kama afanyavyo NBC.
Timu zilinufaika pia kwa kupata vifaa vy michezo.

Simba ndio ilikua kinara wa kupinga GSM ku dhamini ligi na waka gomea kucheza pale kwa mkapa kama yanaendelea kuwepo matangazo ya GSM.

Baada ya mgomo uo Tff ikawaomba radhi GSM kwa yaliyo tokea na GSM wakajiondoa kwenye udhamini uku wakiwa wamesha gawa sehemu ya vifaa vya michezo kwa timu zinazo shiriki ligi ua NBC.

Baadhi ya Timu zikaenda kuomba udhamini ili kuweza kuimarisha bajeti zao za msimu.

Chakushangaza baadhi ya mashabiki wa Mbumbumbu fc mmeanza kulia kuhusu udhamini wa GSM wakati nyinyi Simba mli ugomea!!

Tengenezeni timu ya ushindani la si hivyo mtaendelea kulalamika mpaka 2030.
Izo kelelezenu ata ao Tff wana waona ma Mbumbumbu tu.
Huyo akili kisoda.
 
Eti "tuma offer weka pesa nyingi zaidi ya GSM". Nani kakudanganya kuwa GSM anatoa pesa kwa hizo timu kuzidi wanazopata kutoka kwa Azam Media? Je baada ya GSM kuingia kwenye hizo timu, mikataba yao na AZAM Media ilikoma?

Mtu akijitokeza kutoa motisha kama ambavyo NHC, Silent Ocean au ile kampuni ya Aluminium wamefanya kwa wachezaji bora wa timu kuna shida gani? Mbona kila siku tunasikia timu zinaahidiwa zawadi ili ziifunge Simba hatuoni mkipinga hilo?

GSM aendelee na udhamini wa hizo timu na akiweza aongeze timu nyingi zaidi. Sisi tutajalizia kuzipa hizo timu nguvu zaidi ya kupambana.
Wewe hutaki GSM kudhamini ligi ili iweje?
Hutaki atangaze bidhaa zake?
Ni mashindano wako kibiashara?
Mbona kampuni kampuni nyingi zimeweka udhamini?
Wewe dhamini uone kama timu zitakataa pesa yako
 
Hivi vijana wa mangungu uwa mnafikiria kwa kutumia nini? Kwa akili zako tu finyu ubora wa kikosi cha Simba unalinganisha na ubora wa kikosi cha yanga kwenye kupambania matokeo popote pale? Iwe kwa mchezaji Mmoja Mmoja Simba mna kikosi Gani cha kubattle na yanga nyie? Yanga anapata matokeo kutokana na quality yake na sio pumba ulizoziandika hapa za gsm sijui anafanyaje na kutokubali mnazidiwa pakubwa kiubora na yanga na mkawekeza kwenye propaganda za maji taka na mkashindwa kufanya usajili wa maana kuboresha kikosi mtakuwa mnatoa milio Kila siku iendayo kwa mungu,,wenzako wanasajili kina pacome wewe unaenda kuwaleta kina mutale alafu utegemee kupata ubora ule ule walionao wenzako si utahaira huo!
Ubora upi huo unaouongelea? Simba bado ipo mashindano ya CAF na Yanga imeishia makundi. Kwenye ligi tofauti ni pwenti 1 ambayo Jmosi inaweza kuyeyuka. Simba ndiyo timu iliyofungwa magoli machache zaidi mpaka sasa. Misimu 2 iliyopita, katika kila kipengele na takwimu ukiacha kuzidiwa pwenti, Simba ilikuwa ndiyo timu bora kuliko zote.
Kila mtu ashinde mechi zake. We shinda zote uone kama hutapata ubingwa.

Unafungwa na Yanga unasingizia GSM, ukiongoza ligi UBAYA UBWELA.

Singida anafungwa na YANGA, unaanza kuwapangia kikosi. Kama kikosi ni ishu kwenu kwanini nyie mliburuzwa? SHINDA MECHI ZAKO ZOTE UTAKUWA BINGWA
Inafikirisha sana kuona ligi ilikuwa na ushindani zaidi wakati timu zina njaa kuliko kipindi hiki ambacho zinaonekana kuwa na shibe. Niambie mwaka ambao Yanga ilikuwa inazifunga timu goli 5 na 6 kila siku kama miaka hii miwili ya udhamini wa timu 8 za GSM.
Simba alivofunga mara nne mfululizo kutia ndani kipigo cha mbwa mwizi cha goli 5 alikuwa na udhamini wa GSM
Hii hoja ni ya kijinga sana nashangaa sana nikisikia mtu anaitoa. Ukiibia mtihani mmoja halafu mingine sita ukiifanya bila kuibia, haiondoi ukweli kuwa kuna mtihani mmoja umeibia.
kwahiyo Yanga ikiifunga Simba GSM ametoa pesa?
Hii hoja ni ya kijinga sana nashangaa sana nikisikia mtu anaitoa. Ukiibia mtihani mmoja halafu mingine sita ukiifanya bila kuibia, haiondoi ukweli kuwa kuna mtihani mmoja umeibia.
 
Kuna mjinga anasema GSM Itaishtaki Jamii forums kisa
Sasa najiuliza atakaeshtakiwa ni alieandika au Jamii forums
Ukiona wamefika hapo kwenye vitisho inabidi uanze tu kuwaimbia Maji ya Shingo ya Daz Nundaz
 
Back
Top Bottom