Mo Dewji: Simba inanipa hasara, ningenunua hata Ndege

Mo Dewji: Simba inanipa hasara, ningenunua hata Ndege

MO: SIMBA INANIIGIZIA HASARA, KAMA SIO SIMBA NINGEKUWA NA NDEGE.

“Simba ni klabu ambayo nimeipenda tangu nikiwa mdogo, naipenda Simba kutoka moyoni, mechi ya juzi tulipofungwa na Raja nimekaa kwenye Gari nimelia"

“Nimewekeza kwenye Simba sio kwaajili ya pesa huu ni mwaka wa sita, tumekubaliana ni Bil. 20 lakini tukifanya mahesabu imefika labda Bil. 50 ambazo nimewekeza, kama nngependa raha au kitu kingine Bil 50 ningenunua hata ndege,”

“Ukiniambia Simba ni Biashara kwangu Hapana, Simba ni Hasara kwangu ndiyo, Simba kifedha inanipa hasara, Kuna wafadhili wengi sana ambao wamekuja na wamepita wengi wao wamefilisika Kutokana na kuwekeza au kufadhili Simba

RAIS wa Heshima na Mwekezaji wa Simba, MOHAMMED DEWJI.

Source @futbalplanet_ [emoji1241]

NB acheni kumwingiza hasara Mo

View attachment 2562675
Kwani uongo?
 
Bado somo halijaingia kabisa kwenye ubongo! Yaani akina Mohamed wengine wakiitwa Mudi, ni sawa! Halafu akina Mohamedi wengine (wenye hela) wakiitwa Mudi, wanaona ni udhalilishaji! Na hivyo wanataka waitwe Mo! 🤔

Sawa kiongozi. Ngoja tu ibakie hivi hivi.
Sijahusisha hela kwenye jina. Ni sawa na Mtu anayemfahamu Mheshimiwa Samia Rais wa Tanzania tangu utoto na labda jina lake la utoto awe analijua. Sasa mbele za watu aseme " kibibi mambo vipi?" haitakuwa sawa.

Kama mtu anaitwa Mo muite Mo na siyo kutanguliza maneno kwamba kina Mo wana hela ila huyu ni Mudi tu kwa kuwa hana hela ila ana janja janja!!
 
MO: SIMBA INANIIGIZIA HASARA, KAMA SIO SIMBA NINGEKUWA NA NDEGE.

“Simba ni klabu ambayo nimeipenda tangu nikiwa mdogo, naipenda Simba kutoka moyoni, mechi ya juzi tulipofungwa na Raja nimekaa kwenye Gari nimelia"

“Nimewekeza kwenye Simba sio kwaajili ya pesa huu ni mwaka wa sita, tumekubaliana ni Bil. 20 lakini tukifanya mahesabu imefika labda Bil. 50 ambazo nimewekeza, kama nngependa raha au kitu kingine Bil 50 ningenunua hata ndege,”

“Ukiniambia Simba ni Biashara kwangu Hapana, Simba ni Hasara kwangu ndiyo, Simba kifedha inanipa hasara, Kuna wafadhili wengi sana ambao wamekuja na wamepita wengi wao wamefilisika Kutokana na kuwekeza au kufadhili Simba

RAIS wa Heshima na Mwekezaji wa Simba, MOHAMMED DEWJI.

Source @futbalplanet_ [emoji1241]

NB acheni kumwingiza hasara Mo

View attachment 2562675
Mtani Kalpana umeiona hii? Mnamfirisi mtoto wa watu..!!! GENTAMYCINE mchangieni mwenzenu, mmemtia hasara vya kutosha..!!
 
Japo najua sio rahisi kuendesha Simba na Yanga na ni kweli wanajitoa sana ila haya maneno sio mazuri kuyatamka
Ye alichukua Simba aiendeshe kibiashara apate faida kama hapati asianze kusimanga poor Mudi biriani
Ndo boss wenu sasa
 
Sijahusisha hela kwenye jina. Ni sawa na Mtu anayemfahamu Mheshimiwa Samia Rais wa Tanzania tangu utoto na labda jina lake la utoto awe analijua. Sasa mbele za watu aseme " kibibi mambo vipi?" haitakuwa sawa.

Kama mtu anaitwa Mo muite Mo na siyo kutanguliza maneno kwamba kina Mo wana hela ila huyu ni Mudi tu kwa kuwa hana hela ila ana janja janja!!
Yaani umemaindi hatari..!! Nilidhani utamaindi kwa kumtia hasara Mudi, lakini unakuja kumaindi Makolokolo haya..!!
 
Moja ya interview ya hivyo kabisa, sio yeye alikuwa analilia mchakato umalizike? hebu atuambie ni wapi walikubaliana na Simba kuwa Bil-20 italipwa kwa mafungu kwa miaka 6? baya zaidi mwandishi habari ni wazi kapewa maswali ya kuuliza maana alijuaje kuhusu 1.5 B iliyotolewa na yeye. Kila kitu kilikuwa set up hii inanikumbusha kuna Rais alikuwa anasema hii kazi ngumu sana silali usiku lakini akimaliza awamu yake yuko mbio kugombania kazi ngumu. Mo umekosea heshima wana Simba
[emoji23][emoji23]
 
Hii kitu inafikirisha sana. Maana yake anataka kusema akiondoka, basi na simba itapotea kabisa kwenye ramani ya soka!

Na ili kuhakikisha haifi/kupotea, basi analazimika kuingia hasara, ili kuikoa!! Kweli akili za mbayuwayu, changanya na zako! Mwenzake kwa upande wa Yanga, hata humsikii akilialia!!
[emoji23][emoji23]
 
Kwa hili sikuungi mkono Mo. Kiongozi anapaswa kujua aongee nini wakati gani mahali gani mbele ya Nani. Maneno yako yanamaanisha uko Simba Kwa kujitolea na siyo Mwekezaji kama Katiba inavyotaka. Sisi tunajua 20b ndo inayokupa haki ya kuwa Mbia pale Simba na siyo mfadhili. Add ons unazotoa Kwa Simba hata kama si sehemu ya mkataba lakini hazipaswi kutangazwa Kwa Kila Mtu na kuonyesha kwamba bila wewe Simba si lolote tena. Umeoa mwanamke halafu Kila siku unamwambia bila wewe ningekuwa Tajiri maana hapa gharama za kukulisha na kukuvisha zingetosha kununua gari?
Fact kabisa
 
Simba mtafute mashamba mkalime mchangie uendeshaji wa timu muache kumfilisi kaka mudi.
f73d412c59068b02bed4f87100643037_1.jpg
 
Back
Top Bottom