Mo Dewji ulikosea sana 'Kumsifu' vile hadharani Kocha Mgunda

Mo Dewji ulikosea sana 'Kumsifu' vile hadharani Kocha Mgunda

Kikosi Cha Simba ata kiwe kamili hakina uwezo wa kupata matokeo chanya Kwa Azam au Yanga alicho ongeza Mgunda ni hamasa tu. Kikosi ni chakawaida, ata kama waseme baada ya wiki tatu warudiane Simba anastahili afungwe.

Ivi we Una James Akaminko, Ndala, Sospeter Bajana, Migunamiguna kulia Kipre, kushoto Lyanga nje una Nado juu una Dube, Kola na Mbombo Unafungwa vipi na Simba!!
Mpira wa Tanzania unachupri nyingi.
Kwa hyo yanga alistahili kumfunga AZAM au ndio tuamini hvyo hvyo wenye akili ni wawili yanga
 
Mgunda ni kocha mzuri ila ushikaji ndio utamdondosha, Boko, Nyoni na Mkude wanapewa nafasi zaidi kishikaji, jana upande wa Nyoni ulikuwa kama shimo mipira inapitishwa, una beki 2 wawili , Israh Mwenda na Kapombe pia kapona tayari, kwa nini umtumie Nyoni ili kumtafutia game time tu.

Unamuingiza Boko, wakati nje una Sakho, unaowezo wa kumtumia Phiri 9, na Sakho 10, ushikaji kwenye kazi utaishi kuleta matatizo tu.
Sasa sakho angefanya Nini mule?
 
Mgunda ni kocha mzuri ila ushikaji ndio utamdondosha, Boko, Nyoni na Mkude wanapewa nafasi zaidi kishikaji, jana upande wa Nyoni ulikuwa kama shimo mipira inapitishwa, una beki 2 wawili , Israh Mwenda na Kapombe pia kapona tayari, kwa nini umtumie Nyoni ili kumtafutia game time tu.

Unamuingiza Boko, wakati nje una Sakho, unaowezo wa kumtumia Phiri 9, na Sakho 10, ushikaji kwenye kazi utaishi kuleta matatizo tu.
Kapombe na Israel wote wagonjwa wana mjeraha option ilikuwa kumtumia kapama upande wa kulia nyini acheze na mkude eneo la kiungo maana AZAM Jana walitengeneza mashambulizi mengi kupitia kwa erasto nyoni
 
Endelea na propaganda zako uchwara za Nabi anafukuzwa. Shida ya huyu pimbi yeye Ni full unafiki na uchochezi hata wapenxi wenzako wa Simba SC wanakudharau Sana Ila ujitambui tu.
 
Mwekezaji wa Simba SC Mo Dewji usichokijua pamoja na utajiri wako ni kuwa 90% ya Wajumbe wa Bodi ya Simba SC ni wapigaji watupu na wengi wao ni wasaliti kutokana na kutumika kwao kutoka upande wa pili.

Mo Dewji baada ya wewe kumsifia mno vile Kocha Mgunda na kuahidi kuwa ungekutana naye Ili mzungumze na ikiwezekana umpe yimu (Simba SC) moja kwa moja, hapa ndipo uliharibu.

Mo Dewji watu wanaokuzunguka ndani ya Simba SC hawataki Mgunda apewe timu moja kwa moja kama unavyotaka kwani wanajua Mgunda akiwa Kocha Mkuu wao hawatapata ile 10% yao na isitoshe Kocha Mgunda ni mzawa na mjanja (mtoto wa mjini) hivyo wanajua kuwa atawakatalia tu.

Hivyo basi Mo Dewji tambua ya kuwa hata matokeo ya jana (Simba SC kufungwa na Azam FC) ni sehemu ya mkakati wa kimafia na kihujuma kutoka kwa hao wana Simba SC (Wazee wa 10%) ili Kumharibia Kocha Mgunda na uondoe imani naye.

Na mchakato wa kumpata na kumleta Kocha Mkuu wa kigeni ufanyike na kama kawaida yao akija wao wapate (wale hiyo 10% yao), ambayo ndiyo inawaweka mjini pamoja na zile 10% wanazozipata kutoka kwa wachezaji mizigo wa kigeni na hata wa kizawa.

Mo Dewji kama kawaida yangu GENTAMYCINE bingwa wa kupata taarifa ngumu na za ndani kabisa ambazo kwa 99.9% huwa ni sahihi (kweli) ni kwamba, hata katika mechi ya Jumapili dhidi ya Mtibwa Sugar FC kama hakutokuwa na umakini mkubwa na kukabiliana na hawa mafia na wasaliti kuna uwezekano mkubwa Simba SC ikafungwa tena au kutoka sare/Suluhu Ili tu kuendelea kumharibia Kocha mzawa Mgunda kisha aje Kocha wa kigeni (hasa Mzungu) na ule utamaduni wao wa kula 10% uendelee na maisha yao yaendelee.

Kazi kwako tu sasa kuyafanyia kazi!
Mtahaha sana
 
We jamaa utakua haupo vizuri kicwani humo..... haki ya mungu.
 
Hivyo basi Mo Dewji tambua ya kuwa hata matokeo ya jana (Simba SC kufungwa na Azam FC) ni sehemu ya mkakati wa kimafia na kihujuma kutoka kwa hao wana Simba SC (Wazee wa 10%) ili Kumharibia Kocha Mgunda na uondoe imani naye
Wote tumeangalia mpira jana simba alizidiwa kila kitu azam kastahili kabisa ushindi hujuma ziko wapi mzee baba.
 
Inawezekana Kuna huo 'umafia' unaosema lakini je, hao 'mamafia' ndio wanapanga kikosi? Mechi ya Jana Mgunda amefeli kwenye uchaguzi wa kikosi na kupelekea kufeli kimbinu.
Azam.ana timu nzuri kushinda simba.. nitajie mchezaji mmoja wa simba aliekosekana angeweza kubadilisha matokeo jana, kwa sasa simba ana timu ya kawaida sana ni mashabiki hawataki kukubali huo ukweli mchungu
 
Gentamycin, kama tu hamuwezi kukubali kwamba kufungwa ni sehemu ya mchezo, mtaendelea kutafuna uchawi.

Kuna shida sana upande wa mashabiki upande wa hizi timu mbili. fahamu Azam pia anataka matokeo. Azam sio timu ya kubeza, ,ametoka kupoteza shirikisho, amepoteza kwenye ligi, so ameingia akiwa na ari zaidi ya kupata matokeo
Pamoja na sababu zingine zote ila ukweli ni kwamba azam ana timu nzuri kushinda simba mimi jana nilivyoangalia line ups na subs timu zote mbili nikajua azam anashinda nikamuua simba kwa mhindi
Screenshot_20221028-144300_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom