Mobimba nye nye nye,Lemutuz na Mo Dewji wafanya mazungumzo kwa masaa 13,wakubaliana kumwaga mabilioni

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Wiki inayoelekea ukingoni huenda ikawa wiki bora kuliko zote kwa vijana baada ya matajiri vijana wa kitanzania kufanya mazungumzo kwa zaidi ya masaa 13.
Lemutuz ambaye anatwaja kama muajiri mkubwa nchini katika eneo dogo la mraba (employee/sq ft),akiwa ameajiri vijana 8 katika mita za mraba nne na Mo Dewji ambaye anatajwa kama muajiri mkubwa kwa ujumla, mazungumzo hayo ambayo ajenda yake bado haijawa wazi hasa lkn wachunguzi wa mambo wanadai inawezekana walijadili masuala ya kumwaga mabilioni kwa vijana ili kuwaondoa mitaani.
Baadhi ya vijana waliobahatika kutoa maoni yao walipongeza hatua hiyo kubwa huku wengine wakisema ni nadra sana kuona Lemutuz akifanya mazungumzo na mtu asiye na digrii 3 kwa masaa mengi kiasi hicho.
 
Kijana ana miaka zaidi ya 50 ni kijana wa aina gani huyu?!
 

Kwani Le Mutuz kijana? Kama kijana basi hata JK ni kijana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…