covid 19
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 6,967
- 17,452
Dah hii nchii inachosha sana sijui kama nitamaliza mwaka huu nikiwepo hapa..Ni mikoa yote tu, miaka kadhaa nyuma, kuna huyo mwingine tuli mtaarifu mchana kuwa tuna tegemea kupokea maiti ya ndugu yetu inaingia usiku kutoka Dar, katika wilaya moja ya Mkoa wa iringa. Akatuambia yeye hata kuwepo zamu yake inaisha saa tisa na nusu kwa hiyo akampigia ambae atakuwa zamu akampa taarifa kuwa kuna maiti inategemea kuingia ule usiku akasema sawa. Tukafanya malipo ya siku mbili kwamba akifika atakaa huo usiku na kesho yake. Tuna tegemea kuzika kesho kutwa yake.
Sasa baada ya maiti kuingia huo usiku pamoja na msafara tumefika mochwari, hakuwepo kwa sababu tulikuwa tumepewa namba yake mchana ikabidi tumpigie kwa kujua labda alikuwa maeneo yaleyale ya hospital, cha kushangaza tuna mpigia simu anasema ni kweli yuko zamu ila kuna sehemu ameenda kwa hiyo tumtoe katika jeneza tumu weke kwenye sakafu ya mochwari, kwa sababu kuna baridi sana maiti haita haribika yeye atakuja kumhifadhi asubuhi. Ndugu na jamaa waliyo kuwepo pale mochwari, walichukia sana kusikia ndugu yao awekwe kwenye sakafu akae mpaka asubuhi ndo aje kuhifadhiwa.
Tuka muomba sana, atuelekeze alipo kwa sababu tuko na magari tumfuate ule usiku ila alikataa katakata kutuelekeza alipo, na mwisho wa siku alituzimia simu, kwa hiyo tukapata adhabu yakukaa na maiti ikiwa kwenye jeneza hadi asubuhi na ile baridi mpaka alivyorudi saa 12 asubuhi. Kuja kuongea nae vizuri ni kama alitaka hongo ili aje kumhifadhi halafu aendelee na mambo yake.
ni kama tupo nchi ya watu ambao hawajakamilika kuwa binadamu kamili.