KERO Mochwari Muhimbili nao wanakula kwa urefu wa kamba?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Dah hii nchii inachosha sana sijui kama nitamaliza mwaka huu nikiwepo hapa..

ni kama tupo nchi ya watu ambao hawajakamilika kuwa binadamu kamili.
 
Kazi za Mochwari zinafanyika vizuri tu. Tangaza nafasi za kazi watu wataaply wa kutosha. Si vibaya kumpa asante mfanyakazi wa Mochwari ukizingatia mazingira ya kazi ila isiwe lazima kwa kiwango cha kugomea maiti isizikwe na ndugu kisa hujahongwa.
Yes umeeleza vizuri pia

Ila ntasema tena kwamba sio kila kazi inafanywa na kila mtu kazi nyingine ni wito

Mpe 10k 20k hupungukiwi kitu kwani akiacha kukuhudumia anakua amekaa tu si anaenda kwa watu wengine kuwahudumia pia
 
Nataka nikupe kazi mortuary wewe ndugu mzalendo ufanye mwezi mmoja 600k upo tayari?
Nipo tayari nipe hiyo connection..

Au hilo tangazo liweke vizuri ubandike hapa jf uone vijana tukichangamkia fursa.
Hivi unajua watu wanafanya mishe ngumu kwa ujira wa buku 5 kwa siku??
Ushawahi kufanya kazi viwandani wewe?? Pesa kiduchu masimango debe, sembuse hiyo unawasumbua wafiwa hadi wanakupa rushwa acha utani kijana, au unaogopa maiti??
 
Sawa ukifika wakati utapata
 
We kilaza kweli kweli,kwaiyo rushwa sasa iruhusiwe nchi nzima
Hivi unajuwa maana ya rushwa? Zile siyo rushwa bali ni gharama za kutayarishiwa mwili. Unahitaji sanda, dawa ya kuzuia kunuka na kumuogesha na kumvalisha nguo.

Kama hutaki kutoa ingia ukatayarishe mwenyewe
 
Dah hii nchii inachosha sana sijui kama nitamaliza mwaka huu nikiwepo hapa..

ni kama tupo nchi ya watu ambao hawajakamilika kuwa binadamu kamili.
Kuna mtu tulikutana kwenye comment section huko youtube,aliniuliza mm ni wa wap nikamwambia akasema aliitembelea Tz one time but kuna subhumans hapa!Nilimkasirikia sana lakini kulikuwa na kaukweli kachungu👨
 
Inaonekana rushwa ni utamaduni wa watanzania na haitokuja kuisha.

Kama wewe unadhani wahudumu wa mochwari ni halali yao kutaka rushwa basi elewa pia polisi na wengine wote ni haki yao kutaka rushwa vilevile.

Maana kila mmoja anayo mazingira yake ambayo atakwambia kuwa ni magumu na "akili zake haziko sawa".

Nchi yetu imebarikiwa wajinga wengi.
 
Hivi unajuwa maana ya rushwa? Zile siyo rushwa bali ni gharama za kutayarishiwa mwili. Unahitaji sanda, dawa ya kuzuia kunuka na kumuogesha na kumvalisha nguo.

Kama hutaki kutoa ingia ukatayarishe mwenyewe
We ni tahira fulani,ghalama halisi huwa ni unalipa na unapewa risiti, ila huwa wanataka rushwa tu kwa mambo ya kipuuzi
 
Kwanza pole mkuu kwa msiba.

Tz nchi limeoza Aisee hakuna penye unafuu , nchi imeoza mpaka hongo inaonekana kitu halali na cha kawaida
 
We ni tahira fulani,ghalama halisi huwa ni unalipa na unapewa risiti, ila huwa wanataka rushwa tu kwa mambo ya kipuuzi
Kwani lazima utoe rushwa? Nenda kachukue maiti tenu hivyo hivyo
 
Kila mtu anajilimbikizia Mali kupitia ofisin kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…